Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

😳😳 kumbe ushuru unaweza kulingana na bei ya gari?
 
Hiyo hela yote Ukilimia matikiti heka 20 unapata faida million 90
Tatizo sina muda wa kuingia shamba, ukiweka watu wa kusaidia wanaiba hela zote hata matikiti matikiti sitayaona
 
Biashara ya matikiti inalipa braza
Biashara za kilimo ninazoziamini, na ambazo nimeshuhudia majirani zangu zinawatoa live bila kusimuliwa na watu wengine au motivational speaker, ni nyanya na vitunguuu tu. Kwa mwaka wanalima mara 4, hela haiishi ndani.
 
😳😳 kumbe ushuru unaweza kulingana na bei ya gari?
Zingine zinalingana au kukaribiana na bei za kuagizia. Gari nilizoona zina ushuru kidogo ni Honda Crossroad tu. Zingine zote ushuru wake ni mkubwa
 
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.
 
Naomba kujua yard za magari zilizopo Dar na Dodoma nione aina ya magari yaliyopo na bei zao
 
Honda crossroads mkuu unazijua vzr spare zake nk? Maana iko kwenye ramani zangu naikubali kinyama
 
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.
Daaah hii nchi ngumu mno , huu ndiyo wizi 1st degree
 
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.

Hio kawaida sana

Kuna Jeep nliona CIF $3500 tu

Kodi bongo ikuwa 30m[emoji23]

Ilibidi nicheke tu yaani TRA kuna magari wameyawekea vikwazo kama urusi kwa mmarekani
 
Zingine zinalingana au kukaribiana na bei za kuagizia. Gari nilizoona zina ushuru kidogo ni Honda Crossroad tu. Zingine zote ushuru wake ni mkubwa
Daah asee ni kweli, nimeenda kuchungulia inaushuru nusu na wenzie wa specification kama zake, sijui TRA wamejisahau ama wamebaini tatizo la kiufundi.
 
Mazda Demio labda

Siku hata IST haishikiki inacheza hadi 15m huko
 
Naomba kujua yard za magari zilizopo Dar na Dodoma nione aina ya magari yaliyopo na bei zao
TOYOTA RAUM NEW MODEL

Year 2003
Cc 1500
NEW BACK LIGHTS

BEI: 14.5 Mil

Registration free
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…