Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Wakuu habari za asubuhi.

Ni matumaini yangu mmeamka salama siku hii ya pasaka.

Nina mpango wa kununua gari kwa bajeti ya Tshs 10M - 12M. Nipo mkoani na ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari. Nina familia ya watu 6 yani wife watoto 3 na house girl.

Matumizi yangu ni kuendea kazini, kuwapeleka watoto shule, kwenda kanisani Jumapili na familia, kwenda mjini kununua mahitaji, na mara moja kwa mwaka kwenda kuwasalimia wazee kijijini.

Kutoka mahali ninapoishi hadi kazini kuna umbali wa 2Km rafu road, kwenda shuleni 3Km (1km rafu, 2Km rami), mjini 4Km (1Km rafu, 3Km rami), kanisani 2Km rafu road na kijijini kwa wazee ni 1150Km, takribani 70 rafu road baada kutoka mkoani.

Naomba ushauri kwa bajeti tajwa hapo juu naweza kupata gari gani inayoendana na matumizi yangu? Nikipata inayotumia mafuta kati ya 10Km - 15km/1Lt inaweza kunifaa.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Kwa gari ya familia kubwa kwa brand ya Toyota, zitakazokufaa ni Wish, Spacio, Sienta, na Raum. Ila bajeti yako ipo chini. Ungeongeza angalau ifike 14mil utapata kwa kuagiza. Miaka 5 iliyopita kwa bajeti hiyo ungeweza kupata Raum nzuri tu. Ila kwa sasa angalau uwe na 14mil kwenda juu. Corona ilileta mabadiliko. Freight charges zimepanda kutoka $800 hadi $1800.

BTW, nimeangalia Beforward asubuhi hii, Sienta ya 2004 (7 seater) ni $2994 (7mil) na ushuru wake ni 5.2mil. Hapo bado charges za bandari, clearance, na service ya kuanzia.
😳😳 kumbe ushuru unaweza kulingana na bei ya gari?
 
Hiyo hela yote Ukilimia matikiti heka 20 unapata faida million 90
Tatizo sina muda wa kuingia shamba, ukiweka watu wa kusaidia wanaiba hela zote hata matikiti matikiti sitayaona
 
Biashara ya matikiti inalipa braza
Biashara za kilimo ninazoziamini, na ambazo nimeshuhudia majirani zangu zinawatoa live bila kusimuliwa na watu wengine au motivational speaker, ni nyanya na vitunguuu tu. Kwa mwaka wanalima mara 4, hela haiishi ndani.
 
😳😳 kumbe ushuru unaweza kulingana na bei ya gari?
Zingine zinalingana au kukaribiana na bei za kuagizia. Gari nilizoona zina ushuru kidogo ni Honda Crossroad tu. Zingine zote ushuru wake ni mkubwa
 
😳😳 kumbe ushuru unaweza kulingana na bei ya gari?
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.
 
Kwanza gari ya kwanza si ya kuagiza tafuta expert ununue gari nzuri kwa mtu au nenda yard kachague kabla hela yenyewe hujaipunguza, last year niliona Passo nzuri sana new model kwa 12m hope haijapanda sana. Wewe funga safari Dar kuna hizo option zote 2. Ila epukana na yard za uswahilini utaweza uziwa used za watu au iliyobadilishwa spare parts, nenda maeneo ya kinondoni kwa watu wa kishua huko at least uhakika. After that utaweza kusave hela yako nyingine taratibu ununue gari ya kijanja. Gari kama Cami I don't think kama inaweza masafa marefu ya kutembelea wazee kijijini.
 
Naomba kujua yard za magari zilizopo Dar na Dodoma nione aina ya magari yaliyopo na bei zao
 
Ongeza 1M agiza Carina TI
Huwezi pata 7seater kwa hiyo budget za ya kupigwa
Au uamue kumvua mtu Wish au Sienta thou kwa hayo mazingira zitakutesa.

Ningekuwa mimi ndo wew ningevumilia kidogo nkajichanga ikafika 16 afu nkavuta Honda CrossRoad[emoji119]

Kwa maelezo yako yanaangukia kene iyo Honda basi
Honda crossroads mkuu unazijua vzr spare zake nk? Maana iko kwenye ramani zangu naikubali kinyama
 
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.
Daaah hii nchi ngumu mno , huu ndiyo wizi 1st degree
 
Sio kulingana tu, hadi kuzidi bei ya gari. Kama unaweza, ingia Beforward angalia Nissan Teanna ya 2014 yenye ref. no. BN253859. CIF ya gari ni $5027 (approximately 11.9mil). Ukiingia TRA, ushuru wa hilo gari ni 26,633,723.

Hio kawaida sana

Kuna Jeep nliona CIF $3500 tu

Kodi bongo ikuwa 30m[emoji23]

Ilibidi nicheke tu yaani TRA kuna magari wameyawekea vikwazo kama urusi kwa mmarekani
 
Zingine zinalingana au kukaribiana na bei za kuagizia. Gari nilizoona zina ushuru kidogo ni Honda Crossroad tu. Zingine zote ushuru wake ni mkubwa
Daah asee ni kweli, nimeenda kuchungulia inaushuru nusu na wenzie wa specification kama zake, sijui TRA wamejisahau ama wamebaini tatizo la kiufundi.
 
Mazda Demio labda

Siku hata IST haishikiki inacheza hadi 15m huko
 
images.jpeg.jpg
 
Naomba kujua yard za magari zilizopo Dar na Dodoma nione aina ya magari yaliyopo na bei zao
TOYOTA RAUM NEW MODEL

Year 2003
Cc 1500
NEW BACK LIGHTS

BEI: 14.5 Mil

IMG-20230418-WA0043.jpg
IMG-20230418-WA0046.jpg
Registration free
IMG-20230418-WA0045.jpg
IMG-20230418-WA0044.jpg
 
Back
Top Bottom