Hakuna kitu kitabadilisha maisha kuwa Bora zaid Kama hutojishughulisha na kufanya jambo kwa juhudi na ubunifu vinginevyo utazidi kunyooshea watu vidole na kuamini kuwa unalogwa au unaonewa kumbe the problem is you
Ni kweli kabisa kuwa, msingi wa mafanikio na maisha bora kwa mtu yeyote ni kufanya kazi kwa bidii..
Lakini kwa upande mwingine lazima ujifunze na utambue uwepo na umuhimu wa serikali..
Serikali yoyote ina jukumu kubwa la kipekee sana ku - facilitate au kuhakikisha kuwa watu wana mazingira bora na rafiki kwa ajili kufanya shughuli zao kwa ajili ya kujipatia mkate wao wa kila siku...
Kwa mfano ni wajibu wa serikali;
å Kutoa uongozi bora na siasa safi kwa taiga na watu wake. Kuna sehemu imesemwa, ustawi wa taifa lolote unahitaji uongozi bora na siasa safi.
å kusambaza huduma za kijamii e.g umeme, maji, afya, nk nk nchini kote kwa usawa
å Kuweka mazingira bora na rafiki ya ufanyaji biashara, kilimo, uchimbaji madini nk nk
å Kuweka mifumo rafiki ya kodi kwa watu wote ktk sekta zote
å Kuhakikisha mazingira ya kiusalama na amani kwa watu wote ili wafanye shughuli zao bila bughudha
å Kuhakikisha kuwa mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengine ni mazuri ili kuwezesha watu kuvuka mipaka ya kitaifa kwa urahisi ili wafanye shughuli zao nk nk
KWA HIYO;
¶ Personal efforts ktk kujitafutia riziki zetu za kila siku ni muhimu sana lakini serikali ina nafasi ya 90% kufanya kila mtu ktk taifa lake afurahie maisha kwa kuwa na mahitaji yote muhimu...
¶ Ndiyo maana katika maandiko matakatifu (Neno la Mungu - Biblia) mahali fulani imeandikwa;
"....mtu mwovu atawalapo, watu (wananchi) huugua...."
Kama watu wanaugua tu, maana yake wana njaa na wanaumizwa na uongozi uliopo..
Ndivyo ilivyokuwa Tanzania ya Magufuli...