Kwa 'body language' tu ya Mama azungumzapo huhitaji Akili Kubwa kujua ya kwamba...

Kwa 'body language' tu ya Mama azungumzapo huhitaji Akili Kubwa kujua ya kwamba...

Hapa nakubaliana na wewe Asilimia 💯 maana nawaambia watu bila kufanya kazi hela hamtaipata wala kuonekana, mara ooh hayupo aliekuwa anabania hela, nawaambia nyie mnacheza yani mchezo bado ni ule ule

Wanafiki katika Jamii huwa hamkosi pia.
 
1. Baba Mbabe alikuwa hamshirikishi na huenda hata alitamani Kuachana nae.

2. Ushauri wake ulikuwa ukipuuzwa na kudharauliwa na Baba.

3. Hali ngumu ya Maisha imemkwaza Mama japo Baba aliona anatukomesha.

4. Aliwaamini sana Waliodharauliwa na Baba ambao walikuwa Weledi kuliko aliyowateua Yeye Baba.

5. Kuna Siri nyingi za Upigaji wa Miradi ya Baba ila alishindwa Kumwambia kwakuwa alishagundua anadharaulika nae.

6. Baba Kukitenga sana Kisiwa anakotoka Mama kulimkwaza akiamini hata Kisiwa pia kina Haki ya Keki Tamu na Nono ya Ardhi ya Tanzania.

7. Mama ameiva vyema Kidiplomasia na Kiustaraabu japo ana Ukali wa Kiumakini tofauti na Baba aliyekuwa na Ukali, Kukomoa, Chuki na Ujeuri wa Kibabe.

Ni mapema mno Kumpongeza Mama ila tusikatae kuwa dalili ya Mvua ni Mawingu na ' Body Language ' ya Mama inaonyesha kuwa Kilio cha Ugumu wa Maisha ya Watanzania ( Vyuma Kukaza ) hata na Yeye (Mama) inamuuma.

Hivyo Kipaumbele chake sasa ni Kuturudishia Tabasamu lililopotea katika Sura za Watanzania tokea tarehe 25 Oktoba, 2015 hadi 17 Machi, 2021.
Hata akiingia rais mwingine itakuwa hivyo
 
Kuna ushahidi akina mama hulemaza watoto. Kwa lugha anayotumia ni dhahiri kutakuwa na viongozi watakaolemaa

Aliyekuambia Kuiongoza Familia Kiukali ndiyo Kuilea vyema nani? Hebu tupisheni hapa Wanafiki na Wapuuzi wakubwa nyie. Rais wa Tanzania sasa ni Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan na siyo mwingine na kama kweli mlikuwa mnampenda aliyeondoka na nyie ondokeni mumfuate huko aliko Mapumzikoni sasa.
 
Wabongo ndio wanapenda sana mambo haya kupetiwa petiwa....
mkimpata mtu anayewachana live kwa ukweli na kuwakaripia mnapokosea mnalia lia

Kama ulikuwa ukimpenda sana na Wewe Fariki kwa Makusudi ili uzikwe ukapige nae Stori huko aliko na akupe na Cheo kama ukitaka ili uendelee Kumpenda.

Tanzania ya sasa ipo chini ya Mama yetu Mpendwa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na ninamkubali kuliko Maelezo kwakuwa namjua siyo Mshamba na Mpumbavu.
 
Nimesikiliza hotuba yake.Tone ni too soft na hii itawafanya watendaji wa-relax sana.Nahisi pia kwamba watendaji wataachiwa wafanye maamuzi mengi wao bila close monitoring.Hii ni hatari,kwa mustakabali mzima wa taifa,unless wao wenyewe wako committed to their people and development of the country.Maneno "kayaangalieni haya' yanakosa msisitizo na authority na yana akisi wasi wasi wangu.Tusubiri,ila I can sense danger.

Swala la kuunda kamati ya wataalamu ya ushauri wa C-19 ni nyeti sana.Kamati hii inahitaji wataalamu wenye weledi mkubwa kuhusu maswala yote ya COVID na the so called Covid vaccine,what it is and the true agenda behind it.Jinsi wanavyoweza kupata contents zilizopo ndani ya the C-19 gene therapy au kinachoitwa kwa makosa vaccine,kitu ambacho ni muhimu, watajua wao,ila ni muhimu kujua kama kweli hivyo therapy inafaa kwa matumizi ya wanadamu.Already we know kwamba haifai kufuatana na vifo na madhara mengi ambayo yame ripotiwa kwa watu ambayo wamepata hiyo DNA modifying therapy.

Niseme wazi,akina Bill Gates,Rockefeller, Rothschild, Anthony Fauci,WHO na the World Economic Forum macho yao yote sasa yataelekezwa kwenye members wa kamati hiyo,and how to influence the final decision of the committee.Ni muhimu kwa hiyo kila mmoja wao akafuatiliwa kwa ukaribu ili asije akatumiwa kuingiza nchi mkenge.Fedha nyingi sana itatembea hapo,ili ku-influence maamuzi!Niseme in advance,hapa napo I can sense danger.In short I am not optimistic!

Watu hawa wanahitaji pia wawe na ufahamu wa the inner workings of underground societies na agendas of the NWO.Bila kujua yote haya tutaingizwa mkenge sana.Wataalamu hawa pia wanatakiwa kuwa true nationalists and lovers of mother Tanzania.This is basic.

In summary,nini "nahisi" kiko mbele yetu👉A Possible reserval of whatever Magufuli stood for,which will be a disaster for mother Tanzania and Tanzanians.

Maelezo marefu halafu ni Pumba tupu.
 
Binafsi nimefurahia sana hotuba ya mama...Yaani naiona Tanzania mpya kabisa kama kila kitu kitafuatwa kama alivyosema mama.

Watanzania tumuombee sana na kumsupport.

Kwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan anavyofanya sasa na kila nikiota naona kaletwa Kutufuta Machozi ya Tabu, Dhiki, Manyanyaso na Shida Watanzania hata nikiambiwa nimlinde 24/7 bila Mshahara na ninavyompenda Generalist nipo tayari kufanya hivyo muda wowote ule.
 
Waliosema kufa usifiwe inabidi watafakari tena kauli yao, maana mwendazake ni kama kauli hii imeanza mpita kando
 
Wee ipyana, kila zama na kitabu chake. Pambana na yaliyo mbele yako.
Sema kwa sababu ninyi ni watoto, je kuna raha na uhuru wa kijinga ambao watu waliupata katika kipindi cha kikwete??? lkn walimtukana kila uchao. Hivyo usifikiri huyu mama atakuwa analeta chakula mezani kwako, au kujaza pesa mifukoni mwako, bado wewe binafsi unahitaji kuwa na nidhamu na kujituma kulingana na malengo yako na Mwenyezi Mungu alivyokujalia.

Kwanini umeamua kutaja Jina lake lote?
 
Back
Top Bottom