Kilicho muhimu siyo vyama vya siasa, siyo CCM, CHADEMA au ACT au chama kingine chochote BALI ni
kwa Taifa letu kuwa na viongozi wazuri na mifumo mizuri ya kiutawala.
Sina shaka kabisa Rais Samia ni kiongozi mstaarabu anayejua thamani ya utu wa mwanadamu. Anayetakbua kuwa kazi ya kiongozi ni kuwajengea mazingira watu wa makundi yote, ya kuweza kuijenga nchi yao, kuyajenga maisha yao na ya familia zao. Wananchi wana haki ya kuyafurahia maisha yao hapa Duniani kwa muda ambao Muumva wetu alitupangia alimradi hatuvunji sheria tulizozitengeneza.
Mh. Rais Samia ana uwezo wa kuliunganisha Taifa. Umoja katika Taifa letu ndiyo utakaoushinda umaskini.
Rais asisahau kujenga mifumo imara ya kiutawala ambayo italilinda Taifa dhidi ya watawala wabaya ambao wanaweza kuja kutokea hapo baadaye.
Tuachane na siasa za chuki, tumkosoe Rais wetu, tumshauri inapobidi, lakini kumpa ushirikiano ni jambo jema zaidi. Na hili livuke mipaka ya imani na ushabiki wa vyama. Taifa letu ni muhimu kuliko CCM, CHADEMA au ACT.
Mungu wetu, umjaze hekima Rais huyu mwanamke wa kwanza katika Africa Mashariki. Aongozwe na upendo wa kweli kwa Taifa lake. Ajue kuwa wanaomshangilia, wanaomsifia, wanaomkosoa, hata wanaomkejeli, wote ni watu wake.