Kwa 'body language' tu ya Mama azungumzapo huhitaji Akili Kubwa kujua ya kwamba...

Business as usual ndio tunalolitarajia mkuu.

Mama kaanza na gia kubwa ila naomba asipoteze muelekeo tu.

Muda ndio kila kitu na kila la kheri kwake mama.
 
mitano tena kwa mama
 
zege la nyasi
mama ameusoma mchezo,kwamba ili afike mbali anahitaji kuiga mazuri ya mafahali hawa wawili na kuyaacha mabaya yao.

mathalani:
a)jk alikuwa
1)mwanadiplomasia mzuri,
2)mwanademokrasia
3)mjengaji uchumi
4)mzembe katika ufuatiliaji
5)asiye na msimamo

b)jpm alikuwa
1)mfuatiliaji mzuri
2)asiyependa uzembe na uvivu
3)asiyeyumbishwa ovyo
4)mzalendo kwa nchi
5)jaziba isiyojenga
6)dikteta
7)asiyependa demokrasia na diplomasia

mama achagua sifa zimfaazo kati ya hizo hapo juu.
 
Mama anaongea kama kiongozi, wakati huohuo kama mama, kweli ni mapema ila kwa uanzaji wake, sifa tumpe.
Kiongozi kama nchi ya wavivu,watu wenye majungu, maneno mengi kuliko utendaji kama Tanzania haitaji kiongozi awe kama muuza lamba lamba.

Muda ndio mwalimu.
 
May the Soul of our Hero JPM rest in eternal peace. Let the people talk, but let them keep some words within themselves.. You may praise her at the moment..but mark my words..you are going to regreat..what i saw yesterday, i can say it was a total embarrasment in her regime.
You can not be guided by social media comments when it comes to select or not an individual in a very sensitive possition.
May our beloved country shine in everywhere.
 
Mosi mimi sio mtoto ,pili ninafanya biashara na ni mhanga wa sera kimeo za Magufuli. Hakuna uhuru wa kijinga as long as sheria zilizopo zimetungwa kwa kulinda haki zetu wote sio kwa watawala tu.
 
Ila wapitisha mizigo na wau flow mita bandarini ili wasilipecvodi ni sawa. Ndio maana ya msemo huu kama hukuzingatia kilichopelekea maamuzi hayo .
Tatizo nyie ni waaribifu kama wew ni mpinzani wa Mama pole yako ila tuliowengi karibia nchi nzima tunayaona matumaini mapya kwa mama Samia na kwa hali hii naomba Mama aongezewe ulinzi
 
Mosi mimi sio mtoto ,pili ninafanya biashara na ni mhanga wa sera kimeo za Magufuli. Hakuna uhuru wa kijinga as long as sheria zilizopo zimetungwa kwa kulinda haki zetu wote sio kwa watawala tu.

Good, pambana na yaliyombele yako. yaliyopita ni historia.
 
Tatizo nyie ni waaribifu kama wew ni mpinzani wa Mama pole yako ila tuliowengi karibia nchi nzima tunayaona matumaini mapya kwa mama Samia na kwa hali hii naomba MAMA AONGEZEWE ULINZI

Wewe si wa kwanza wako wengi wanao niona hivi mwisho wa siku hurudi na kusema jamaa aliliona hili mapema tungalimsikia na kufuata ushauri wake.
 
Huna hoja bora ungenyamaza. Hapo ni chuki binafsi tu kwa jpm kwa kudhibitiwa kwako dhidi ya maslahi ya umma. Kama sio cheti feki kutumbuliwa na kadhalika.
Kubambikiwa kesi, kodi, kuvunjiwa nyumba......utachoka tu kujitoa fahamu kama mafarisayo.
 
Hakuna kitu kitabadilisha maisha kuwa Bora zaid Kama hutojishughulisha na kufanya jambo kwa juhudi na ubunifu vinginevyo utazidi kunyooshea watu vidole na kuamini kuwa unalogwa au unaonewa kumbe the problem is you

Ni kweli kabisa kuwa, msingi wa mafanikio na maisha bora kwa mtu yeyote ni kufanya kazi kwa bidii..

Lakini kwa upande mwingine lazima ujifunze na utambue uwepo na umuhimu wa serikali..

Serikali yoyote ina jukumu kubwa la kipekee sana ku - facilitate au kuhakikisha kuwa watu wana mazingira bora na rafiki kwa ajili kufanya shughuli zao kwa ajili ya kujipatia mkate wao wa kila siku...

Kwa mfano ni wajibu wa serikali;
å Kutoa uongozi bora na siasa safi kwa taiga na watu wake. Kuna sehemu imesemwa, ustawi wa taifa lolote unahitaji uongozi bora na siasa safi.

å kusambaza huduma za kijamii e.g umeme, maji, afya, nk nk nchini kote kwa usawa

å Kuweka mazingira bora na rafiki ya ufanyaji biashara, kilimo, uchimbaji madini nk nk

å Kuweka mifumo rafiki ya kodi kwa watu wote ktk sekta zote

å Kuhakikisha mazingira ya kiusalama na amani kwa watu wote ili wafanye shughuli zao bila bughudha

å Kuhakikisha kuwa mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengine ni mazuri ili kuwezesha watu kuvuka mipaka ya kitaifa kwa urahisi ili wafanye shughuli zao nk nk

KWA HIYO;
¶ Personal efforts ktk kujitafutia riziki zetu za kila siku ni muhimu sana lakini serikali ina nafasi ya 90% kufanya kila mtu ktk taifa lake afurahie maisha kwa kuwa na mahitaji yote muhimu...

¶ Ndiyo maana katika maandiko matakatifu (Neno la Mungu - Biblia) mahali fulani imeandikwa;

"....mtu mwovu atawalapo, watu (wananchi) huugua...."

Kama watu wanaugua tu, maana yake wana njaa na wanaumizwa na uongozi uliopo..

Ndivyo ilivyokuwa Tanzania ya Magufuli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…