Kwa 'body language' tu ya Mama azungumzapo huhitaji Akili Kubwa kujua ya kwamba...

Naomba nikwambia serikali ndio kila kitu kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani Ila ujue kila mwanasiasa anapalilia shamba lake na watu wake sisi wengine tujikite kwenye shughuli zetu za kilasiku tufanye kazi kwa bidii na tulioe Kodi naamini katika kufanya kazi kwa bidii ndani ya taifa ambalo haliweki siasa katika kila Jambo
 
Una mawazo kama yangu mkuu
 
Kiongozi kama nchi ya wavivu,watu wenye majungu, maneno mengi kuliko utendaji kama Tanzania haitaji kiongozi awe kama muuza lamba lamba.

Muda ndio mwalimu.
Awamu iliyopita hata wale ambao sio wavivu na kuoendekeza majungu walifunga biashara, kufilisika na wengine kukimbia, hapakuwa na nafuu, amekuja huyu wacha tumpe muda, wavivu watabaki na hali zao na wenye kujituma watanufaika na kujituma kwao.

Muuza lamba lamba alishaenda zake, maana kelele zilikuwa nyingi kumbe tunaibiwa kama kawaida.
 
Kutawala kunakuwa rahisi sana kama una UPENDO wa dhati na unao watawala (waongoza)
Panapo kosekana Upendo panajulikana, kama kwa aliyetenguliambleleyahaki
 
Kwenye ulimwengu wa roho ninafikiri majina yana sehemu yake . Jina la Pombe Magufuli. kwa kiasi fulani mambo yaliharibika. Mama Suluhu. Pamoja na kwamba ni mapema mno kmsifu lakini kutokana na Jina lake ameanza kuleta suluhu ya mambo mengi yaliyokuwa hayana suluhu.
 
Kwa namna alivyoeleza suala la TRAkubambikia watu kodi kubwa nk, tunaanza kuona kumbe kuna mahali walitofautiana; sura ya tofauti zilizokuwepo kati yao inaanza kuonekana.
Lisu alipolisema hili kwenye kampeni, kuna watu walichachamaa kuwa anataka kurudisha nchi nyuma; sasa kalisema mwenyewe.
Watanzania tujifunze kujisimamia!
 
Mungu acheni anitwe Mungu..hua ana namna yake ta kutatua kero za watu wake.

#MaendeleoHayanaChama

Uko sahihi Ndugu Mimi nina Kiongozi Mmoja wa Dini tena anayeheshimika sana Tanzania aliniambia nisilie bali niseme tu Asante kwani kuna Jambo baya sana Mwenyezi Mungu katuepusha nalo Watanzania wengi na huenda lingetugharimu pakubwa na tungejuta ( tungejutia ) kabisa.
 
Hakuna kitu kitabadilisha maisha kuwa Bora zaid Kama hutojishughulisha na kufanya jambo kwa juhudi na ubunifu vinginevyo utazidi kunyooshea watu vidole na kuamini kuwa unalogwa au unaonewa kumbe the problem is you

Tupishe wala hujaelewa vyema huu Uzi.
 
 

Mimi tokea tu alipoapishwa najiona nina Amani ya ghafla, furaha huku nikijiona nina Milioni katika Akaunti yangu Benki wakati iliyopo ni Hela ya Kutunza Kitabu ( Akaunti ) tu Tsh 5,000/=
 

Tunajua ni lazima tu utakuwa Umechukia Mama kuwa Rais kwani ulikuwa Ukifaidika mno Kifisadi na Kiukanda na huyo Mkanda Mwenzenu aliyelazimishwa Kulala kilazima na Israeli ili Watanzania tulioteseka nae tupate Unafuu kupitia Mama Mpendwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…