Kwa Chuki zetu, Wivu wetu na Roho mbaya zetu Waswahili tutamsema sana, ila kwa sasa Tanzania hakuna Kipa bora na Mahiri kama Aishi Salum Manula

Hahaa wazazi wako wapo vizuri kwa kuhifadhi kumbukumbu ,hao wote nimewashuhudia uwanjani live ,enzi hizo luninga ni issue.
Mkuu hongera sana kwa kuwaona hao manguli 👊....

Ninachowashukuru wameyahifadhi magazeti yote ya zamani katika zile waraka ngumu zisizoingiza maji na mavumbi.....

Wakati wa likizo toka niko shule ya msingi kazi yangu nikusoma magazeti hayo ya Uhuru ,Mfanyakazi , Mzalendo,Majira ,Rai ,Rai ya Mwema n.k....

Kwa hiyo nimewasoma wachezaji wengi ijapokuwa sijawahi kuwaona kama akina Razzak Yusufu Carecca ,Sahau Kambi ,Lunyamila ,Malota Soma ,Edward Chumila ,Mwakuruzo ,Sanifu Lazaro ,Said Mwamba ,Masatu George , Kenneth Mkapa na yule Mkapa mwingine daaah yaani ukisoma habari zao kipindi hicho cha utoto mwili unasisimka kama unawaona vile ha ha ha ha 🤣
 
Aiseee yaani unavyowataja kama nawaona Salum Kabunda "NINJA" ,Sanifu Lazaro "TINGISHA" ,Said Sued "SCUD" ,Said Mwamba "KIZOTA"
 
Wewe ndo unataka kuleta chokochoko muacheni kijana
 
Aiseee yaani unavyowataja kama nawaona Salum Kabunda "NINJA" ,Sanifu Lazaro "TINGISHA" ,Said Sued "SCUD" ,Said Mwamba "KIZOTA"
Daaah ya kale dhahabu mkuu 😍

Kuna mmoja anaitwa Gagarino eti nasikia hajapata kutokea.....nipe sifa zake.....
 
Aiseee yaani unavyowataja kama nawaona Salum Kabunda "NINJA" ,Sanifu Lazaro "TINGISHA" ,Said Sued "SCUD" ,Said Mwamba "KIZOTA"
Nasikia Chambua alitakiwa aende Afrika ya kusini wazee wake wakamwambia abaki Yanga na Lunyamila alifanya mtihani wa form 4 kambini kwa Stars hivi ni kweli ama "gahwa" tu?!! 🤣🤣
 
Nasikia Chambua alitakiwa aende Afrika ya kusini wazee wake wakamwambia abaki Yanga na Lunyamila alifanya mtihani wa form 4 kambini kwa Stars hivi ni kweli ama "gahwa" tu?!! 🤣🤣

Yes ni Kweli mkuu kina sekilojo wa kishua,Edibily Jonas Lunyamila anatoka school anaingia uwanjani na ukaupigwa mwingi hatari.
 
Yes ni Kweli mkuu kina sekilojo wa kishua,Edibily Jonas Lunyamila anatoka school anaingia uwanjani na ukaupigwa mwingi hatari.
Hataree Sana mkuu

Zamani kulikuwa na watu haswa naskia ndugu zetu Simba walifanya "janjajanja" wakakosa Kombe la CAF kwa kupigwa nyumbani(Kichwa cha mwendawazimu) 🤣🤣

Waliahidiwa gari za KIA 🤣
 
Hataree Sana mkuu

Zamani kulikuwa na watu haswa naskia ndugu zetu Simba walifanya "janjajanja" wakakosa Kombe la CAF kwa kupigwa nyumbani(Kichwa cha mwendawazimu) 🤣🤣

Waliahidiwa gari za KIA 🤣

Enzi hizo Gari za KIA ndio habari ya Mjini ,KIA ilikuwa New Version ya gari za Chai Maharage!!
 
Aiseee yaani unavyowataja kama nawaona Salum Kabunda "NINJA" ,Sanifu Lazaro "TINGISHA" ,Said Sued "SCUD" ,Said Mwamba "KIZOTA"
Ukitaka kumuona Sanifu Lazaro Tingisha nenda Buguruni Stendi sasa ni Kondakta wa Mabasi ya Mbagala - Buguruni ila najua utalia tu kwa Kusikitika.
 
Balaaa.....

Hussein Masha naskia ndio kiungo wa mwisho fundi....hatujapata kama yeye hadi sasa....
Kwasababu tu Marehemu Hamis Tobias Gaga ( alias Gagarino ) alikuwa Mlevi wa Bia na Gongo ndiyo maana hatumtaji kuwa alikuwa Kiungo Bora kabisa tena mwenye Kipaji cha hali ya Juu kuwahi kutokea hapa Tanzania.

Kwa mliozaliwa Juzi ni kwamba Udambwi Udambwi alionao Clatous Chama na alikuwa nao Augustine 'Jay Jay' Okocha Marehemu Gaga 'Gagarino' alikuwa akiufanya mara Mbili yao.

Acheni mzaha Gaga alikuwa Fundi hasa.

Cc: Jumbe Brown
 
Air manula alikuwa man of the match pia tusisahau mashabik wa mpira wa miguuu huwa wanahitaj ushindi ulitaka uwanyamazishe shinda match bas
 
Kuna mjerumani alitaka kumchukua kumpeleka kwao akachezea Kila akifatwa anakimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…