Kwa dalili zote hizi, bado tu huamini kuwa Yesu Yu karibu kurudi?!

Kwa dalili zote hizi, bado tu huamini kuwa Yesu Yu karibu kurudi?!

Siku 1000=siku moja!
Ndio, mbinguni siku 1000=siku 1.
Kwanini?
Jibu rahisi hili hapa:
Mbinguni hakuna kilio, hakuna njaa, hakuna magonjwa, hakuna kuzeeka, hakuna hofu ya kifo, hakuna vita, hakuna ajali, ni shangwe na nderemo tena bila kuchoka maana huko hakuna kuchoka, hakuna chochote kibaya.
Kwa maisha hayo ya raha ni sahihi kabisa kuona siku 1000=siku 1.
 
Ndio, mbinguni siku 1000=siku 1.
Kwanini?
Jibu rahisi hili hapa:
Mbinguni hakuna kilio, hakuna njaa, hakuna magonjwa, hakuna kuzeeka, hakuna hofu ya kifo, hakuna vita, hakuna ajali, ni shangwe na nderemo tena bila kuchoka maana huko hakuna kuchoka, hakuna chochote kibaya.
Kwa maisha hayo ya raha ni sahihi kabisa kuona siku 1000=siku 1.
Unamaanisha mbinguni ni sehem flani hivi physical?
 
Tunaishi katika kizazi ambacho dalili alizozitaja Yesu za kuja kwake zinadhihirika mbele ya macho yetu wazi wazi. Yesu alipoulizwa kuhusu ishara za kuja kwake na za mwisho wa dunia, alitaja mambo yafuatayo:
1. Watu wengi watakuja kwa Jina lake wakisema wao ni Kristo.
Katika nchi mbalimbali wameishatokea watu waliojiita wao kuwa ni Kristo.
2. Kutakuwa na vita na tetesi za vita. Taifa litaondoka kwenda kupigana na taifa jingine. Dalili hii kila anayefuatilia "news" ameiona ikitimia. Mataifa sasa yanajiondokea tu na kwenda kupigana na mataifa mengine bila kujali hata sheria za UN.
3. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. Tumeshuhudia njaa kali katika maeneo mbalimbali na matetemeko yenye nguvu sana hadi kufikia kipimo cha 9.5 Mmw, na kuangamiza maelfu ya watu katika nchi mbalimbali.
4. Kutakuwa na magonjwa mazito(pestilences). Nani asiyekumbuka Covid-19 ilivyosababisha vifo vya takriban watu milioni 18 duniani kote. Nani hajasikia Ebola inavyotikisa maisha ya watu pamoja na Ukimwi, kisukari, kansa na magonjwa mengine sugu.
5. Maasi yataongezeka na upendo wa wengi utapoa. Huku na kule tunaona maasi na vitendo vingi viovu vikifanyika mchana kweupe mbele ya camera.
6. Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi. Nani asiye na habari jinsi wagonjwa na wenye matatizo wanavyodanganywa kuwa watapona wakinunua chumvi, mafuta na udongo!
7. Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Kwa sasa Injili inahubiriwa kwa viwango vya juu sana kwa njia ya TV, redio, magazeti, mitandao ya kijamii na hata kwa njia ya smartphones! Soma Mathayo 24, Marko 13 na Luka 21 upate maelezo zaidi kuhusu dalili hizo.

Sio Yesu peke yake aliyesema kuhusu mambo ya siku za mwisho. Kitabu cha Danieli kinaeleza pia matukio ya nyakati za mwisho. Danieli ameandika katika sura ya 12:4 jinsi nyakati za mwisho watu watakavyoenda mbio na maarifa kuongezeka. Maarifa yameongezeka kwa kasi sana. Leo hii kila mtu ni shahidi jinsi maarifa ya AI yalivyoongezeka na kuwaacha watu wengi midomo wazi.

Paulo pia alionya kwamba siku za mwisho zitakuwa za hatari; watu watajipenda wenyewe na kupenda fedha. Katika nchi kadhaa tumeona watu wakitimuliwa na kurudishwa makwao bila huruma. Soma dalili nyingine katika 2 Timotheo 3:1-5 na 2 Timotheo 4:3-4.

Petro pia alituasa kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka, wakisema: “Iko wapi ahadi ya kuja kwake?" Humu humu JF kuna nyuzi za watu wanaodhihaki ujio wa Yesu kwa maneno kama haya: "Tangu Yesu aseme kwamba atakuja, mbona imepita miaka mingi hajaja?" Wanasahau kwamba kwa Mungu siku elfu ni kama siku moja tu. Hivyo kama mtu anafikiri Yesu amekawia kuja, basi ajue hilo kuwa kwa Mungu, tangu Yesu alipopaa hadi leo, zimepita kama siku mbili tu. Soma 2 Petro 3:3-8 utaelewa zaidi.

Yesu alisema kuja kwake kutafanana na jinsi ilivyokuwa siku za Nuhu. Walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, wakiendelea na maisha yao ya kawaida. Nuhu aliwatahadharisha kuwa gharika inakuja lakini walimpuuza, kisha gharika iliwaijia ghafla wakaangamia. Ndivyo ilivyo hata leo, watu wakimsikia mtu anahubiri Injili wanasema amerukwa akili. Wataendelea hivyo hivyo hadi siku Yesu atakapokuja ghafla kwa siku na saa wasiyodhani.

"Kwa maana kama vile zilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” (Mathayo 24:37)

Ndugu yangu, Mungu anakupenda, na hafurahii ukiangamia. Ndio sababu anaendelea kukuvumilia na kukuita uje kwa Yesu, utubu dhambi zako na kukubali Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Kumbuka, Yesu pekee ndiye njia ya kutufikisha Mbinguni (Yn 14:6).

Usisubiri siku ya kuja kwa Yesu ifike, ndio utubu. Utakuwa umechelewa. Yesu akija, kufumba na kufumbua atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu na wanaoishi maisha matakatifu. Wanaoendelea kufurahia dhambi wataachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia hii. Jiweke tayari ndugu, muda ubakio si mwingi (Mathayo 24:44).

Ikatae sauti ya shetani inayokuambia kwamba eti mtu hawezi kuokoka akiwa duniani. Ikatae sauti ya mwovu ibilisi inayokuambia kwamba eti Biblia ni kitabu tu cha kutungwa. Kitabu gani cha kutungwa kinachoweza kutabiri mambo yatakayotokea miaka 2000 ijayo? Biblia iliandikwa miaka mingi iliyopita, leo hii tunaona unabii wa kitabu hiki ukitimia katikati yetu.

Nakusihi tena, usiendelee kushupaza shingo yako. Tubu huo uzinzi; na pia kama ulimuacha mke wako au mume wako halali wa kwanza ukaoa au kuolewa mara ya pili, tambua mbele za Mungu unahesabiwa mzinzi. Tubu na umrudie mwenzi wako wa kwanza. Tubu dhambi ya ulevi na ushoga. Tubu dhambi ya uongo na matusi. Tubu dhambi ya wizi. Tubu na uache kupiga punyeto. Tubu mawazo machafu ya kutaka kulipiza kisasi waliokutendea mabaya. Tubu dhambi zako zote, Mungu atakusamehe na kukusafisha udhalimu wote.

Na hata wewe uliyeamua kumfuata Yesu, kama bado hujaitimiza haki yote(yaani kubatizwa katika maji mengi) usiwe mkaidi, wala usitafute visingizio. Kumbuka aaminiye na kubatizwa ndiye atakayeokoka (Mk 16:16).

Kama uko tayari sasa kutubu na kuokoka, fuatisha sala ya toba katika post #2.
Mungu akubariki.
Ahsante kwa kutukumbusha juu ya majira na nyakati. Barikiwa sana
 
Kupaa-mbinguni.jpg

"...Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja namna iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni." (Matendo ya Mitume 1:11)
 
Yupo karibu kurudi kwani alienda wapi?
Alienda mbinguni kutuandalia mahali. Kabla hajapaa kwenda mbinguni alisema hivi:
"Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." (Yohana 14:2-3)
 
Uumbaji wa mwanadamu ni nini?
Ni Mungu kuamuamua kuishi Duniani.

Mungu kuhama Mbinguni na kuishi Duniani ndio huelezea ama kutafsiri uumbaji.

Binadamu ni hekalu au nyumba au sehemu au "host" ambapo Mungu anakaa.

Yesu ni udhihirisho wa namna nyingine ya Mungu katika Maumbo ya mwili.

Ukisoma Injili ya Tomaso, kuna shairi linasema Ufalme wa Mungu upo katika namna ambayo watu hawauhuoni, ukifunua blah n blah ......na nini sijui...

'Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu....'

God's Light, God's Word, God's ....

Thank you
Satan
 
Kama uko tayari kutubu na kumpokea Yesu atawale maisha yako, tafadhali omba sala hii ya toba kwa moyo wa dhati:

"Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na nimeamua kuziacha kabisa. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen"

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu hadi Yesu atakapokuja. Usiache pia kujiunga na Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ili ujifunze jinsi ya kuenenda katika maisha mapya ya wokovu. Ubarikiwe sana
Hiki kizazi unachokihubiria ni sawa na kile cha Sodoma na Gomora.

Usistaajabu wakija pm kukutongoza badala ya kupokea neno.
 
Hiki kizazi unachokihubiria ni sawa na kile cha Sodoma na Gomora.

Usistaajabu wakija pm kukutongoza badala ya kupokea neno.
Wakija pm ntalikemea kwanza pepo la uzinzi liwatoke, baada ya hapo itakuwa rahisi sana kuwaongoza sala ya toba😎
 
Back
Top Bottom