Yupo karibu kurudi kwani alienda wapi?
Achana na maneno ya wengine hao kina Petro tumia uelewa wako tu wa kawaida. Kwani wewe huna akili za kufikiria na kujiuliza hadi Petro aseme“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
”
— 2 Petro 3:9 (Biblia Takatifu)
Kama umeishatubu na kuokoka, utapajua tu mbinguni ni wapi, maana karibu Yesu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni. Yesu alipokuwa anakaribia kupaa mbinguni alisema kuwa nyumbani mwa Baba yake mna makao mengi, hivyo anaenda kutuandalia makao ili Yeye alipo na sisi tuwepo. (Yn 14:2)Mbinguni ndio wapi chief
Mbinguni tutakula si kwa sababu ya njaa, bali kwa furaha na uzuri wa uzima wa milele. Kama vile Adamu na Hawa walivyokula matunda katika Bustani ya Edeni kabla ya dhambi kuingia, vivyo hivyo mbinguni tutafurahia matunda ya uzima bila njaa wala kiu. Ni sehemu ya baraka na utimilifu wa maisha ya milele tuliyoahidiwa na Mungu.Mbinguni hakuna njaa wala kiu
Mbinguni tutakula matunda.
Unakula ili iweje wakati hakuna njaa
Sijasoma ulichoandikaKama umeishatubu na kuokoka, utapajua tu mbinguni ni wapi, maana karibu Yesu atakuja kutuchukua na kutupeleka mbinguni. Yesu alipokuwa anakaribia kupaa mbinguni alisema kuwa nyumbani mwa Baba yake mna makao mengi, hivyo anaenda kutuandalia makao ili Yeye alipo na sisi tuwepo. (Yn 14:2)
Acha nikumegee ngaa kidogo uzuri wa maisha ya mbinguni. Soma hapa
Mbinguni tutakula si kwa sababu ya njaa, bali kwa furaha na uzuri wa uzima wa milele. Kama vile Adamu na Hawa walivyokula matunda katika Bustani ya Edeni kabla ya dhambi kuingia, vivyo hivyo mbinguni tutafurahia matunda ya uzima bila njaa wala kiu. Ni sehemu ya baraka na utimilifu wa maisha ya milele tuliyoahidiwa na Mungu.Mbinguni hakuna njaa wala kiu
Mbinguni tutakula matunda.
Unakula ili iweje wakati hakuna njaa
Hakika, Mungu anaendelea kuwavumilia wanadamu, maana hapendi mtu yeyote apotee.“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
”
— 2 Petro 3:9 (Biblia Takatifu)
Kiongozi hapo unatafuta ligi na wafia dini. Hawa jamaa huwawezi kwa kuviamini vitabu vyao vya riwaya vya miaka 2000 iliyopitaKwahiyo hayo uliyoyataja kuwa yatatokea kudhihirisha ujio wake tuyaite dhambi za wanadamu au neno linatimia?
Kama Alisema yatatokea na yametokea it means Yako nje ya uwezo wa mwanadamu, Yako planned. Kwanini tunalaumiana wanadamu na tunaitana watenda dhambi kwamambo ambayo Yako planned tayari?
Biblia inasemaje? Kulikuwa na sababu yoyote ujio wake uambatane na hayo uliyoyataja hapo?
Naamini katika Mungu asiye na ubaya au uzuri. Mungu ambaye ana encopmas kila kitu na kila mtu Mungu hajuumba ubaya au uzuri Kwa ajili ya kuingia dhambini au kuwa watakatifu. Aliumba kila kitu kwa ajili ya balance ya ulimwengu.Hakika, Mungu anaendelea kuwavumilia wanadamu, maana hapendi mtu yeyote apotee.
Hata hawa wafuatao walipoandika nyuzi zao kuhusu pisi kali, sio kwamba Mungu hakuwaona, aliwaona ila anaendelea kuwavumilia ili na wao waokoke.
Ayatollah the Bird
Fene
de Gunner
Monomer
Ramtz Jr
kyagata
Wong Fei
MIXOLOGIST
"Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?" (Rum 2:4)
Sijasoma pia🚮“Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha BWANA; hawakukubali mashauri yangu, wakayadharau maonyo yangu yote.” (Mithali 1:29-30)
Wewe nikikujibu kwa kukupa vifungu haitakusaidia, maana tayari umeishasema Biblia ni kitabu cha riwaya. Ngoja nikukutanishe na wasomi hawa wenye PhDs za nguvu, labda mtaelewana:Kiongozi hapo unatafuta ligi na wafia dini. Hawa jamaa huwawezi kwa kuviamini vitabu vyao vya riwaya vya miaka 2000 iliyopita
Ndugu yangu, hoja yako ya kumtaja Prof. Francis Collins kama ngao ya kutetea ukweli wa kihistoria au wa kisayansi wa maandiko ya kale inafahamika kitaaluma kama Appeal to Authority (Kuhalalisha hoja kwa kutumia jina la mwanajumuiya mashuhuri). Kimsingi, PhD ya mwanasayansi mmoja haina mamlaka ya kugeuza imani ya kidini kuwa ukweli wa kisayansi.Wewe nikikujibu kwa kukupa vifungu haitakusaidia, maana tayari umeishasema Biblia ni kitabu cha riwaya. Ngoja nikukutanishe na wasomi hawa wenye PhDs za nguvu, labda mtaelewana:
Hawa ni wasomi/wanasayansi walio hai ambao wamekiri wazi imani yao katika Kristo:
Francis S. Collins — PhD in Physical Chemistry; MD in Medicine
Huyu aliongoza Human Genome Project. Human Genome Project (HGP) ulikuwa mradi mkubwa wa kimataifa wa kisayansi wa kuchora na kubaini mpangilio wa DNA ya binadamu.
Francis alikuwa atheist kijana lakini alipofikia umri wa miaka 27 alibadilika akawa Mkristo baada ya kuchunguza suala la imani kwa kina. Huyu amesema wazi kwamba haoni mgongano wa lazima kati ya kuwa mwanasayansi makini na kuwa Mkristo.
John C. Lennox — DPhil (PhD) in...
- Setfree
- biblia iq kubwa kitabu kubwa wasomi wenye
- Replies: 115
- Forum: Habari na Hoja mchanganyiko
Kusema kwamba Biblia ni “kitabu cha riwaya” sio hoja ya kutosha kuamua kama ni ya kweli au si ya kweli. Umri wa kitabu hauamui ukweli wa yaliyomo; kinachotakiwa kuchunguzwa ni ushahidi wa kihistoria, maandishi, manuscript, muktadha na ushuhuda wa watu wa wakati huo.Kiongozi hapo unatafuta ligi na wafia dini. Hawa jamaa huwawezi kwa kuviamini vitabu vyao vya riwaya vya miaka 2000 iliyopita
Ndugu yangu, nashukuru kwa kuleta hoja hizi ambazo sasa zimehama kutoka kwenye kumsujudia mtu mmoja (Appeal to Authority) na kuingia kwenye mjadala halisi wa kitaaluma wa Akiolojia, Historia, na Uhakiki wa Maandishi ya Kale (Textual Criticism).Kusema kwamba Biblia ni “kitabu cha riwaya” sio hoja ya kutosha kuamua kama ni ya kweli au si ya kweli. Umri wa kitabu hauamui ukweli wa yaliyomo; kinachotakiwa kuchunguzwa ni ushahidi wa kihistoria, maandishi, manuscript, muktadha na ushuhuda wa watu wa wakati huo.
Kwanza, ujue kuwa Biblia sio kitabu kimoja kilichoandikwa miaka 2,000 iliyopita na mtu mmoja. Ni mkusanyiko wa vitabu vingi, vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali katika vipindi tofauti, kwa aina mbalimbali za uandishi, na mazingira tofauti ya kihistoria.
Pili, sehemu kubwa ya Biblia inaeleza mambo yanayoweza kuchunguzwa kihistoria kama vile: watu, wafalme, falme, maeneo, desturi na matukio. Kwa hiyo sio sahihi kuiweka Biblia yote kwenye kundi la “riwaya” bila kwanza kuchunguza mambo hayo.
Tatu, hata kuhusu Yesu, tunao ushahidi wa kuwepo kwake duniani kutoka kwenye vyanzo vya kale visivyo vya Kikristo vinavyomzungumzia Yesu na kazi alizozifanya alipokuwa duniani.
Kwahiyo mkuu, nakushauri uisome tena Biblia, uichunguze katika muktadha wake wa kihistoria, kisha ulinganishe madai yake na ushahidi unaopatikana, halafu ndio uje hapa ulete ushahidi wako kwamba Biblia ni kitabu cha riwaya. Vinginevyo utakuwa unajidhalilisha mwenyewe, ukitamka tu maneno yako hayo mbele ya wasomi kama Francis Collins.
Hawa ni wasomi/wanasayansi walio hai ambao wamekiri wazi imani yao katika Kristo:
Francis S. Collins — PhD in Physical Chemistry; MD in Medicine
Huyu aliongoza Human Genome Project. Human Genome Project (HGP) ulikuwa mradi mkubwa wa kimataifa wa kisayansi wa kuchora na kubaini mpangilio wa DNA ya binadamu.
Francis alikuwa atheist kijana lakini alipofikia umri wa miaka 27 alibadilika akawa Mkristo baada ya kuchunguza suala la imani kwa kina. Huyu amesema wazi kwamba haoni mgongano wa lazima kati ya kuwa mwanasayansi makini na kuwa Mkristo.
John C. Lennox — DPhil (PhD) in...
- Setfree
- biblia iq kubwa kitabu kubwa wasomi wenye
- Replies: 115
- Forum: Habari na Hoja mchanganyiko
Umeanza vibaya intro yako. Kusoma seminari sio kigezo cha kuijua Biblia au kumjua Mungu.Ndugu yangu, nashukuru kwa kuleta hoja hizi ambazo sasa zimehama kutoka kwenye kumsujudia mtu mmoja (Appeal to Authority) na kuingia kwenye mjadala halisi wa kitaaluma wa Akiolojia, Historia, na Uhakiki wa Maandishi ya Kale (Textual Criticism).
Kabla sijaingia kwenye hoja zako, naomba nikuondolee hofu moja: Unaponishauri "nikaisome tena Biblia," labda hujui muktadha wa mtu unayejadiliana naye. Mimi nimekulia kwenye malezi ya kidini kama mfia dini tangu nikiwa mtoto mdogo, na nimesoma Seminari hadi ngazi ya Falsafa. Naijua Biblia, na misingi ya kiimani vizuri sana kutoka ndani ya mfumo wake. Mabadiliko yangu kuwa mhakiki (critic) wa maandiko haya hayajatokana na ujinga au kutosoma, bali yametokana na kusoma kwa kina na kuruhusu fikra tunduizi (critical thinking) na mantiki ya kifalsafa viongoze utafutaji wangu wa ukweli.
Hivyo basi, niko tayari kukujibu kwa vigezo hivyo hivyo ulivyovitaja:
1. Kuhusu Muundo wa Biblia (Mkusanyiko wa Vitabu)
Ni kweli kabisa, na nakubaliana nawe kuwa Biblia sio kitabu kimoja bali ni maktaba (anthology) ya vitabu vilivyoandikwa na watu tofauti kwa nyakati tofauti. Lakini kitaaluma, ukweli kwamba kitabu ni mkusanyiko wa maandiko ya kale haufanyi yaliyomo ndani yake kuwa ukweli wa kihistoria otomatiki. Kila andiko ndani ya mkusanyiko huo linapaswa kupimwa kwa vigezo huru vya kihistoria. Hata vitabu vya ngano za Wagiriki wa kale (Homer's Iliad and Odyssey) ni mkusanyiko wa maandiko ya waandishi tofauti, lakini bado yanabaki kuwa fasihi na ngano za kale (mythology).
2. Kuhusu Ushahidi wa Kihistoria na Akiolojia
Unasema Biblia inataja wafalme, maeneo, na falme za kweli. Hili halipingiki. Akiolojia imethibitisha maeneo kama Babeli, Yerusalemu, na wafalme kama Koreshi au Nebukadreza. Lakini hapa ndipo unapofanya kosa la kimantiki linaloitwa Fallacy of Composition (kuchukua ukweli wa sehemu ndogo na kuuaminisha kwenye ujumla wake).
Kitaaluma, uwepo vya maeneo au watu wa kweli kwenye kitabu haufanyi matukio ya miujiza yaliyomo kuwa ya kweli:
- Kitabu cha Troy kinataja mji halisi wa Troy na watu halisi, lakini hiyo haithibitishi kuwa mungu Zeus au Achilles walikuwepo na kufanya miujiza ya miungu.
- Riwaya za kihistoria (Historical Fiction) kama Sherlock Holmes zinataja mji halisi wa London na barabara halisi ya Baker Street, lakini hiyo haimfanyi Sherlock Holmes kuwa mtu halisi wa kihistoria.
- Akiolojia na historia ya kisasa (kupitia wasomi kama Prof. Israel Finkelstein) imethibitisha kuwa matukio makubwa ya msingi wa imani ya Biblia—kama vile Gharika la Nuhu, Mnara wa Babeli, Utumwa wa Misri, na Tukio la Kutoka (Exodus)—hayana ushahidi wowote wa kiakiolojia nchini Misri au rasi ya Sinai. Hii ina maana sehemu hizo ziliandikwa kama fumbo au ngano za kitheolojia (theological myths), sio historia halisi.
3. Kuhusu Ushahidi wa Yesu Nje ya Biblia
Ni kweli, wanahistoria wengi wa mambo ya kale (akiwemo Prof. Bart Ehrman mwenye PhD ya Theolojia kutoka Princeton) wanakubali kuwa kulikuwa na mhubiri wa Kiyahudi aliyeitwa Yesu (Yeshua) aliyetokea Nazareti. Vyanzo vya nje kama Flavius Josephus na Tacitus vinataja uwepo wake na kuuawa kwake.
Lakini mtego wa kitaaluma uko hapa: Wanahistoria hao hao wa kujitegemea wanaeleza kuwa ushahidi wa kihistoria unaishia kwenye uwepo yake kama mwanadamu wa kawaida na mwanaharakati wa kidini. Hakuna chanzo hata kimoja cha kihistoria kisicho cha Kikristo cha karne ya kwanza kinachothibitisha miujiza yake, uzazi wa bikira, au kufufuka kwake. Matukio hayo yanabaki kwenye uwanja wa imani ya kidini (theology) na fasihi, sio kwenye ukweli unaoweza kuthibitika kihistoria (historical facts).
Hitimisho
Kusema Biblia ina "fasihi ya riwaya au ngano" sio tusi wala kujidhalilisha, bali ni uainishaji wa kitaaluma wa aina za uandishi wa kale (literary genres). Kama mtu niliyepitia masomo ya falsafa na theolojia ya Seminari, najua vizuri sana kuwa Biblia ina aina nyingi za fasihi: Mashairi (Wimbo Ulio Bora), Hekima (Mhubiri), Ngano za Kiungu au Mythologies (Mwanzo 1-11), na Riwaya za Kitheolojia (kama vitabu vya Esta na Yona).
Hivyo basi, mimi sio yule anayetakiwa "kusoma tena Biblia" kwa sababu nimeshaisoma kiimani, kisha nikaisoma kitaaluma kwa jicho la kiuchambuzi (critical thinking). Wewe ndiye unayetakiwa kutoka kwenye usomaji wa kiibada tu (devotional reading) na kuingia kwenye Uhakiki wa Kihistoria na Kitheolojia (Historical-Critical Method) ili uone jinsi wasomi wanavyoichambua. Mjadala wangu na wewe haupo kwenye mihemko, upo kwenye taaluma thabiti.
Anarudi kutoka mbinguni alikoenda kutuandalia makao. Hivyo anarudi kuja kutuchukua ili tukaishi katika makao hayo. Siku hiyo waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kuungana na watakaokuwa hai, kisha watakatifu wote miili yetu itabadilishwa, na "kuvikwa" hali ya kutokufa, kisha tutanyakuliwa kumlaki Bwana hewani. Yote hayo yatafanyika kama kufumba na kufumbua.Anarudi kufanya nini na kutoka wapi wakati ukifa unawekwa kwenye makazi ya milele? Ni suala la kkutumia commonsense wala halihitaji PhD katika theolojia wala philosophia.
Ngano za abunwas. Mara yuko hapa. Mara yumo mioyoni mwa wati, mara mbinguni. Upuuzi na uzwazwa mtupu. Kwani lazima aje? Mbona alisema kuwa hakutumwa ila kwa makabila 12 ya israel? Simpo. Ajabu, hata hao wayahaudi aliodai alitumwa kwao walimkataa na wala hawamngoji kama mazwazwa wetu watumwa wa kiakili wa kujitakia.Anarudi kutoka mbinguni alikoenda kutuandalia makao. Hivyo anarudi kuja kutuchukua ili tukaishi katika makao hayo. Siku hiyo waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kuungana na watakaokuwa hai, kisha watakatifu wote miili yetu itabadilishwa, na "kuvikwa" hali ya kutokufa, kisha tutanyakuliwa kumlaki Bwana hewani. Yote hayo yatafanyika kama kufumba na kufumbua.
Wenye dhambi wataachwa duniani. Na kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijatokea tangu kuumbwa kwa dunia. Mungu akusaidie utubu dhambi zako na kumwamini Yesu ili usikose kuingia mbinguni. Amen
Yohana 14:2–3; 1 Wathesalonike 4:13–17; 1 Wakorintho 15:51–52; Mathayo 22:30; Mathayo 24:21, 40–41; Matendo 17:30; Yohana 3:16.
Kwa habari zaidi: soma uzi huu:
Kama kuna habari tunayopaswa kuisikia tena na tena ni habari ya Ujio wa Bwana Yesu Kristo. Hilo ni tukio la hakika na la kutisha kwa wasiomwamini, lakini lenye furaha kuu kwa waaminio. Maandiko yanathibitisha wazi kuwa Yesu atakuja mara ya pili kama alivyokwenda mbinguni. Malaika waliwaambia wanafunzi: "Huyu Yesu, aliyetwaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomwona akienda mbinguni" (Matendo 1:11).
Yesu mwenyewe alisema: "Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." (Yohana 14:3). Yesu...
- Setfree
- hali yesu
- Replies: 11
- Forum: Habari na Hoja mchanganyiko