Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Katika upumbavu ambao sijawahi kuukubali ni ile kauli ya marehemu pale Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha kwamba yeye na Kikwete walishaongea kuwa akitoka JK ni zamu yake kuwa Rais kama vile walikuwa na hatimiliki ya hii nchi. Wewe Bams umeandika ushuzi mtupu. Tanzania ni ya watu wote. Kama una vigezo vilivyowekwa kikatiba ruksa kuutaka urais. Hakuna dhuluma yoyote aliyofanyiwa marehemu Lowassa. Na hata kama alidhulumiwa basi ilikuwa sahihi kabisa kwasababu alishakufuru kwa kudhani yeye tu ndo anastahili kuwa Rais. Hayo mambo ya laana hakunaga kwenye siasa.
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Kikwete ana damu mikononi mwake ya watu wengi sio Edward Lowassa tu bali hata yule mwandishi wa Habari MWANGOSI aliyeuawa huko Iringa na polisi kwa amri ya Kikwete! He will have to pay for all his evils kama sio hapa duniani basi huko kungine!😭😭
 
Kwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?

Cha ajabu wanaolia Lia na hili na Chadema...kama Lowassa aliona Ccm wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema unawajua sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?

Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Mbona unaingiza kitu ambacho hakuandika? Amesema Lowassa alichaguliwa lakini Kikwete akamdhulumu! Je, Mungu ndiye aliyemwambia Kikwete azuie Lowassa asiwe rais?
 
Katika upumbavu ambao sijawahi kuukubali ni ile kauli ya marehemu pale Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha kwamba yeye na Kikwete walishaongea kuwa akitoka JK ni zamu yake kuwa Rais kama vile walikuwa na hatimiliki ya hii nchi. Wewe Bams umeandika ushuzi mtupu. Tanzania ni ya watu wote. Kama una vigezo vilivyowekwa kikatiba ruksa kuutaka urais. Hakuna dhuluma yoyote aliyofanyiwa marehemu Lowassa. Na hata kama alidhulumiwa basi ilikuwa sahihi kabisa kwasababu alishakufuru kwa kudhani yeye tu ndo anastahili kuwa Rais. Hayo mambo ya laana hakunaga kwenye siasa.
Wewe mzenj mambo ya huku Tanganyika huwezi kuyajua! Bila Lowassa Kikwete asingepata Urais; mipango yote ya kampeni iliratibiwa na Lowassa!
Nyie wazenj pambaneni na hali yenu kuamua kama Rais wenu Hussein Mwinyi ni Mzanzibari au sio!
 
Wewe mzenj mambo ya huku Tanganyika huwezi kuyajua! Bila Lowassa Kikwete asingepata Urais; mipango yote ya kampeni iliratibiwa na Lowassa!
Nyie wazenj pambaneni na hali yeni kuamua kama Rais wenu Hussein Mwinyi ni Mzanzibari au sio!

Sasa yeye EL aliweza kumfanya JK akawa Rais,yeye alishindwaje kujipa Urais? au hata kuusimika mfumo wake mpaka Leo?
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
CCM imebeba dhambi nyongi sana kupitia viongozi wake

Huyu mzee ni kinara wa dhambi hizo
 
Sasa, kama Lowassa alimwambia Kikwete anataka kujiuzulu, Kikwete akakataa, lakini Lowassa akalazimisha kujiuzulu, huoni Lowassa kajitakia mwenyewe kupigwa chini kwa kulazinisha kujiuzulu?

Ulitegemea vipi Kikwete aendelee ku support mbio za Urais za Lowassa baada ya Lowasssa mwenyewe kulazimisha kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond?

Yani ulitaka Kikwete ampigie kampeni ya urais Lowassa aliyeshindwa Uwaziri Mkuu kwa kashfa?

Huoni kwamba Lowassa ndiye aliyemsaliti Kikwete hapo kwa kulazinisha kujiuzulu na kumuachia manyanga Kikwete, wakati labda alihitajika kupambana akiwa upande wa serikali?

Mtu aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na msukosuko wa kashfa, unajuaje akipata urais na kupata msukosuko wa kashfa hatajiuzulu tena?

Lowassa alipewa mtihani wa uongozi, akashindwa. Kikwete akaona huyu kashindwa, twende na wengine.

Hata mimi ningemshangaa sana Kikwete kama angempigia kampeni Lowassa kwa sababu ni tafiki yake tu.
umeandika mawazo yangu matupu niliyokua nataka niyaandike pia.
EL alibugi hapo.
 
Laana ya Lowassa na JPM Kwa JK itampeleka Kwa haraka sana.

Hahaha, wewe umejuaje kama laana zao na sio laana za JK ndio zimewaondoa?

Mnayemuona ni mshenzi inawezekana wala sio mshenzi ila ndio vile tena " akuanzaye mmalize" yeye akimaliza anaonekana mkorofi.

Yapo mengi Kitaa huku ambayo nayo yanaonyesha huyo huyo JK ametafutwa akalipa kisasi Kwa hao wote kama defensive na wahusika wakakaa wao.
 
Nakumbuka Ridhiwani akaibuka na ile kauli yake Rais hatoki kaskazini, ili kuthibitisha baba yake ameshamchinjia baharini Lowassa.

Bahati nzuri umma wa watanzania ukaja kuwathibitishia vinginevyo, pale ndio walipotambua maamuzi yao sebuleni kwao, sio kitu mbele ya umma wa watanzania ukiamua kwenda na mtu wao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hahaha, wewe umejuaje kama laana zao na sio laana za JK ndio zimewaondoa?

Mnayemuona ni mshenzi inawezekana wala sio mshenzi ila ndio vile tena " akuanzaye mmalize" yeye akimaliza anaonekana mkorofi.

Yapo mengi Kitaa huku ambayo nayo yanaonyesha huyo huyo JK ametafutwa akalipa kisasi Kwa hao wote kama defensive na wahusika wakakaa wao.
Upumbavu mkubwa
 
Back
Top Bottom