Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Nimeona huko X jamaa wanamuwakia moto huyu mzee, yaani walikuwa wanamsubiri aongee tu waluke naye.

Kuna picha nimeiona kwa karibu mzee anazeeka kwa hatua za haraka sana, mara nyingi dhuruma huwa haipiti hivi hivi, inakutafuna ukiwa hujijui, muangalie yule dokta pale JKIC anavyoliwa!.
Mengine ni dua za kuku tu kwa Mwewe.
 
Huoni kwamba hili ni jambo jema sana la uwajibikaji kiongozi yeyote hata ikiwa ni Rais kujiuzulu pale inapoonekana ameshindwa kutimiza majukumu yake sawasawa?!

Mbona Mwinyi aliwahi kujiuzulu akiwa waziri halafu akaja kuwa Rais baadaye?
Kujiuzulu inawezekana likawa jambo jema, lakininsi qualification ya kuwa kiongozi.

Enzi za Mwinyi hazikuwa za siasa za uwazi na ushindani kama sasa, ni enzi ambazo mtu mmoja aliweza kutawala miaka 24. Ni enzi tofauti kabisa.
 
It's not necessarily lazima ni JK!, sometimes wahafidhina wana nguvu kuliko rais!, ila mkubwa ni jalala!.

Ni kweli kwasababu JK alikuwa mjamaa, EL ni bepari tayari!.

Sina uhakaki kama makubaliano haya yalikuwepo!

Sii kweli, jina la Lowassa lilichinjiwa baharini hata kwenye CC halikujadiliwa, ila akina sisi tuliisha muandaa kisaikolojia Elections 2015 - Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Sii kweli, jina la EL halikutoka hata CC, hivyo halikuingia hata NEC, ule wimbo wa "Tunaimani..." ni uliimbwa NEC!

Sii kweli!, wanaoamua nani awe ngombea wa CCM, sio wana CCM, ni kitu kinachoitwa "the inner circle" angalia tarehe ya bandiko hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Sii kweli!, kura zote mpaka za urais zimehesabiwa vituoni na kila msimamizi alipewa copy ya matokeo!, TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia! ila kwa upande wa Zanzibar, kule ndio kweli EL alimbwaga JPM Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Hii sii kweli, Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! makarateka yalifanywa uchaguzi wa 2020!.

Sii kweli, ni wahafidhina!

ukitenda wema mwingi kuliko ubaya karma inarekebisha "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Baada ya ushauri huu, Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!

Amen
Umeweka links nyingi mno, hembu summarize.
 
Katika upumbavu ambao sijawahi kuukubali ni ile kauli ya marehemu pale Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha kwamba yeye na Kikwete walishaongea kuwa akitoka JK ni zamu yake kuwa Rais kama vile walikuwa na hatimiliki ya hii nchi. Wewe Bams umeandika ushuzi mtupu. Tanzania ni ya watu wote. Kama una vigezo vilivyowekwa kikatiba ruksa kuutaka urais. Hakuna dhuluma yoyote aliyofanyiwa marehemu Lowassa. Na hata kama alidhulumiwa basi ilikuwa sahihi kabisa kwasababu alishakufuru kwa kudhani yeye tu ndo anastahili kuwa Rais. Hayo mambo ya laana hakunaga kwenye siasa.

Tatizo unachangia bila kuelewa hoja.

Hayo mambo ya urafiki kati ya marehemu na Kikwete yamewekwa tu ili kuonesha mmoja alivyomsaliti rafiki yake.

Jambo la msingi ni ushetani wa Jakaya:

1) Kwa katiba ya CCM, Lowasa na mwanaCCM mwingine yeyote, wote walikuwa na haki ya kugombea nafasi ya Urais na kisha kupigiwa kura na wajumbe. Lakini Kikwete kwa kujua kuwa Lowasa lazima angeshinda kama jina lake lingekuwemo katika watu wa kupigiwa kura, akaamua kulikata jina la Lowasa.

Jambo la pili, ni ule ushetani wa siku zote wa CCM. Lowasa kagombea kupitia chama kingine, lakini kwa kutumia madaraka yake ya Urais akapora ushindi wa Lowasa na wa Maalim Seif.
 
Sina chochote kumlaumu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuhusu Marehemu Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Vyote vilivyofanyika ndivyo vinatufanya leo hii kuwa huru kutoa maoni.
Tumshukuru Mungu Kwa Maisha ya wote wawili,ingawa mmoja katangulia mbele za haki.
Nina hakika siku Mzee Kikwete naye akiondoka kuna watu watasema tena kama ambavyo leo tunasema.
Mwenyezi Mungu mpumzishe mpendwa wetu mahala pema na uwajaaliwe Viongozi wengine na sisi kwa ujumla tuishi maisha marefu yenye fanaka.
 
Kikwete ana damu mikononi mwake ya watu wengi sio Edward Lowassa tu bali hata yule mwandishi wa Habari MWANGOSI aliyeuawa huko Iringa na polisi kwa amri ya Kikwete! He will have to pay for all his evils kama sio hapa duniani basi huko kungine![emoji24][emoji24]

Nakubaliana nawe. Kikwete ni mtu wa kuuma.na kupuliza lakini lengo lake ni kuuma.
 
JK anamiaka 70 huko sasa una taka afe na miaka mingapi? Ukiona amekufa ujue ahadi yake ilishafika ndio maana yupo hadi Leo maana angeweza kufa hata na miaka 20.

Kikwete 73 years as to date.

Lowasa 71 years
 
Kwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?

Cha ajabu wanaolia Lia na hili na Chadema...kama Lowassa aliona Ccm wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema unawajua sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?

Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Kuwaelewa watanzania walio wengi ni ngumu na ugumu zaidi ni kuwa wanaamini wanaelewa kila kitu kilichotokea kuliko wahusika wenyewe na hivyo hata Mzee JK angesema nini bado wangeendelea kuamini wanachoamini.Sina baya na Mzee Lowassa ila alikuwa binadamu mwenye mapungufu yake na mazuri yake. Huu ukamilifu watu tunaompa na ustahili unatufanya tusijifunze kwake na mchakato mzima wa hicho anacholaumiwa Mzee JK. Kuna yaliyositiriwa ambayo umma haujui na kwahiyo lawama zote zitaelekezwa kwa mtu.
 
Hayo mambo ya kuwa Rais kwa kupitia urafiki wao, siyo hoja ya msingi. Hoja ya msingi, ni roho ya dhuluma aliyo nayo Kikwete.

Hata kama tukisema kuwa Lowasa alipojiuzulu ilimkera Kikwete, lakini kwa nini Kikwete aamue kudhulumu haki yake? Alitumia madaraka yake kulikata jina la Lowasa licha ya kwamba wajumbe wengi na wanachama wengi wa CCM walikuwa wakimtaka Lowasa.

Hiyo haitoshi, umemkata jina kwenye chama ambacho wewe ni mwenyekiti wake, ameondoka, amepigiwa kura na wananchi, ameshinda uchaguzi, bado unadhulumu umma wote wa Watanzania kuongozwa na mtu waliyemtaka. Hivi wewe ni mtu wa namna gani? Zanzibar nako akamtumia Jecha kudhulumu haki ya Maalim Seif. Halafu leo, kwa unafiki mkubwa anasema eti marehemu aliendelea kuwa rafiki yake siku zote. Wewe unayaamini hayo?
Unajuaje Kikwete alimkata jina Lowassa kwa kudhulumu haki yaje na si kwa kuifanyia Tanzania haki kwamba alijua Lowassa ni kiongozi dhaifu ambaye kashindwa hata Uwaziri Mkuu na kwenye urais angeleta shida kubwa zaidi?

Lowasss alijuwa na haki ya kugombea urais, lakini si haki ya kushinda urais.

Na kugombea urais katimiza hiyo haki yake, nje ya CCM, lakini bado hakushinda urais.
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Kikwete ni mnafiki mkubwa.
Maradhi alopata lowasa yaliasisiwa na kikwete.
Mungu atamlipa
 
Unajuaje Kikwete alimkata jina Lowassa kwa kudhulumu haki yaje na si kwa kuifanyia Tanzania haki kwamba alijua Lowassa ni kiongozi dhaifu ambaye kashindwa hata Uwaziri Mkuu na kwenye urais angeleta shida kubwa zaidi?

Lowasss alijuwa na haki ya kugombea urais, lakini si haki ya kushinda urais.

Na kugombea urais katimiza hiyo haki yake, nje ya CCM, lakini bado hakushinda urais.
Lowassa anaweza kuwa na matatizo yake ila sio la kiongozi dhaifu, alikuwa ni mtu mwenye maamuzi na pia mchapakazi tukiangalia alivyosimamia mpango wa shule za kata na mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka mikoa kadhaa.

Sidhani kama kuna mawaziri wakuu waliowahi kuwa na nguvu kuliko Sokoine na Lowassa.
 
Sasa kama kashfa haikuwa ya Lowassa, ilikuwa ya serikali nzima, Lowassa kutaka kujiuzulu yeye ni kimbelembele.

Na mtu kimbelembele anaweza kuleta matatizo katika uongozi.

Ni hivi, ingekuwa Kikwete kamtuma Lowassa ajiuzulu, kamwambia "Edward, haya maji ni marefu, inabidi tumtoe mtu hapa ili kuinusuru serikali, tena mtu mzito, nakuomba kama rafiki yangu ujiuzulu ili kuinusuru serikali, halafu hapo baadaye mambo yakipoa, tutakurudisha ugombee urais nikimaliza mimi".

Halafu Lowassa akasema "Kweli? Serikali inaweza kuanguka? Na mimi kujiuzulu kwangu ndiko kutainusuru? Mnanitaka nijiuzulu halafu nitakuwa rais baada yako? Hapo hakuna shida, najiuzulu"

Halafu Lowassa akajiuzulu.

Halafu baadaye, alipotaka kuwa rais, Kikwete akamruka. Akamkata.

Hapo sawa, ungeweza kusema Kikwete mtu jahili na laghai, kamuhadaa mwenzake ajiuzulu, kwa ahadi kuwa atamfanya awe rais, mwenzake akajiuzulu, na urais akamkata.

Lakini mambo hayakuwa hivyo. Kwa maelezo yako, Kikwete hakutaka Lowassa ajiuzulu. Hata Lowassa alivyotaka kujiuzulu, Kikwete alikataa, Lowassa akalazimisha kujiuzulu.

Sasa hapo mpango wa Kikwete wa Lowassa kuendelea kuwa Waziri Mkuu umekataliwa na Lowassa.

Aliyemsaliti mwenzake kati ya Kikwete na Lowassa ni nani hapo?

Na kama Lowassa alikataa mpango wa Kikwete kuendelea kuwa Waziri Mkuu, kwa nini unafikiri ni sawa Kikwete kukubali mpango wa Lowassa kuja kuwa rais?
kiukweli Masai yero kazingua mzee wa Msoga hana baya kumpa shavu la uwazirii kazingua mwenyewe alf then anataka Uraisi JK akaona wee bhana acha kuzingua...
 
Wewe mzenj mambo ya huku Tanganyika huwezi kuyajua! Bila Lowassa Kikwete asingepata Urais; mipango yote ya kampeni iliratibiwa na Lowassa!
Nyie wazenj pambaneni na hali yenu kuamua kama Rais wenu Hussein Mwinyi ni Mzanzibari au sio!
Alipewa nafasi ya uwaziri mkuu amelipwa chake JK hana baya
 
Kuwaelewa watanzania walio wengi ni ngumu na ugumu zaidi ni kuwa wanaamini wanaelewa kila kitu kilichotokea kuliko wahusika wenyewe na hivyo hata Mzee JK angesema nini bado wangeendelea kuamini wanachoamini.Sina baya na Mzee Lowassa ila alikuwa binadamu mwenye mapungufu yake na mazuri yake. Huu ukamilifu watu tunaompa na ustahili unatufanya tusijifunze kwake na mchakato mzima wa hicho anacholaumiwa Mzee JK. Kuna yaliyositiriwa ambayo umma haujui na kwahiyo lawama zote zitaelekezwa kwa mtu.

Halafu kama alidhulumiwa huko CCM mbona alisamehe na kurudi...
Nongwa imebaki Kwa hawa wafuasi uchwara ambao hata alipokuwa Ccm walimwita fisadi...Leo ghafla Eti kadhulumiwa
 
Lowassa anaweza kuwa na matatizo yake ila sio la kiongozi dhaifu, alikuwa ni mtu mwenye maamuzi na pia mchapakazi tukiangalia alivyosimamia mpango wa shule za kata na mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka mikoa kadhaa.

Sidhani kama kuna mawaziri wakuu waliowahi kuwa na nguvu kuliko Sokoine na Lowassa.

Kutokuwa dhaifu na kuwa na nguvu hata Hitler ana sifa hizo. That does not mean Hitler was good for Germany or the world.

Sokoine alikuwa na maamuzi sana lakini alikuwa na papara. Kuna siku Nyerere alitania tu akisema barabara zetu hususan vijijini ni mbovu sana, inaonekana kama tutahitaji wakuu wa wilaya wajifunze kupanda farasi ili kufikia wananchi.

Kesho yake Sokoine akaanza maongezi ya kuagiza farasi. Balozi Raphael Lukindo akatoa tahadhari, jamani farasi wanataka maandalizi, wanataka mipango, mkiwaleta kwa pupa watakufa tu. Sokoine akatumia turufu ya Uwaziri Mkuu kunyamazisha hoja za balozi Raphael Lukindo, akaagiza farasi tu kutoka Argentina. Mwishowe farasi wale wakafa kama alivyotabiri balozi Raphael Lukindo.

So much for being a strong lrader.

Whether Lowassa ni kiongozi mzuri au si kiongozi mzuri is debatable, what is not debatable, ni kwamba, Lowassa kujiuzulu, against Kikwete's advice per Bams, ilikuwa fatal mistake, ilikuwa shooting oneself in the foot before starting a marathon, and hoping to win.

Na kumtegemea Kikwete am support Lowassa baada ya Lowassa kujiuzulu kwa scandal, against Kikwete's wishes, is pure naivette.
 
Sasa hapa mnatoa stories zinazogongana.

Wengine mnasema JK hakutaka Lowassa ajiuzulu ila Lowassa akalazimisha, wengine mnasema JK alimshauri Lowassa aandike barua ya kujiuzulu ili aikatae, ika JK hakuikataa.

Habari hii watu wanaojua ukweli wake wa ndani ni wachache sana na hapa tutabishana kwa speculations tu kuhusu mambo ya details kama hizi.

Kibaya zaidi, viongozi wetu hawaandiki vitabu vya maisha yao, na hao wachache wanaoandika mambo muhimu mengi hawayaandiki.
Na JK kutoikataa hiyo barua, ndio hofu kwake ikaanza akiamini kama Lowassa angekuwa Rais, basi angekuja kulipa kisasi.

Pia, uchafu wa Ridhiwani wakati wa utawala wa baba yake, JK akaamua kumtosa Lowassa, ndio maana Ridhiwani akaropoka "Rais hatatoka Kaskazini", kwasababu ya hofu ya kisasi.

Walijua angekuwa Membe ili awalinde, bahati mbaya mambo yakatibuka bahati ikamuangukia Magufuli, hapo tena ikabidi waliokuwa na dili chafu waanze kujisalimisha kwa Magufuli, akiwemo Home Shopping Centre na GSM.

Makubaliano yao yaliitwa; Gentleman's Agreement.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom