Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe mpuuzi waliotangaza nia walikuwa 38 na majina yalihitajika matano. Kwanini unamuongelea mtu mmoja tu?Tatizo unachangia bila kuelewa hoja.
Hayo mambo ya urafiki kati ya marehemu na Kikwete yamewekwa tu ili kuonesha mmoja alivyomsaliti rafiki yake.
Jambo la msingi ni ushetani wa Jakaya:
1) Kwa katiba ya CCM, Lowasa na mwanaCCM mwingine yeyote, wote walikuwa na haki ya kugombea nafasi ya Urais na kisha kupigiwa kura na wajumbe. Lakini Kikwete kwa kujua kuwa Lowasa lazima angeshinda kama jina lake lingekuwemo katika watu wa kupigiwa kura, akaamua kulikata jina la Lowasa.
Jambo la pili, ni ule ushetani wa siku zote wa CCM. Lowasa kagombea kupitia chama kingine, lakini kwa kutumia madaraka yake ya Urais akapora ushindi wa Lowasa na wa Maalim Seif.
Nawe tumia akili.Halafu kama alidhulumiwa huko CCM mbona alisamehe na kurudi...
Nongwa imebaki Kwa hawa wafuasi uchwara ambao hata alipokuwa Ccm walimwita fisadi...Leo ghafla Eti kadhulumiwa
Hiyo stori ya Sokoine na kuleta farasi inaonyesha jinsi gani alikuwa kiongozi anayejali hali za raia wa chini, kama mpango wake huo wa kuwapa wakuu wa Wilaya farasi ungefanikiwa( na kama pia haukuhujimiwa ukizingatia farasi ni mmojawapo ya wanyama wanaovumilia mazingira magumu sana) huenda viongozi wangejibidiisha na leo hii vijiji vyote vingekuwa na lami kuepuka kuendelea kutembelea farasi.Kutokuwa dhaifu na kuwa na nguvu hata Hitler ana sifa hizo. That does not mean Hitler was good for Germany or the world.
Sokoine alikuwa na maamuzi sana lakini alikuwa na papara. Kuna siku Nyerere alitania tu akisema barabara zetu hususan vijijini ni mbovu sana, inaonekana kama tutahitaji wakuu wa wilaya wajifunze kupanda farasi ili kufikia wananchi.
Kesho yake Sokoine akaanza maongezi ya kuagiza farasi. Balozi Raphael Lukindo akatoa tahadhari, jamani farasi wanataka maandalizi, wanataka mipango, mkiwaleta kwa pupa watakufa tu. Sokoine akatumia turufu ya Uwaziri Mkuu kunyamazisha hoja za balozi Raphael Lukindo, akaagiza farasi tu kutoka Argentina. Mwishowe farasi wale wakafa kama alivyotabiri balozi Raphael Lukindo.
So much for being a strong lrader.
Whether Lowassa ni kiongozi mzuri au si kiongozi mzuri is debatable, what is not debatable, ni kwamba, Lowassa kujiuzulu, against Kikwete's advice per Bams, ilikuwa fatal mistake, ilikuwa shooting oneself in the foot before starting a marathon, and hoping to win.
Na kumtegemea Kikwete am support Lowassa baada ya Lowassa kujiuzulu kwa scandal, against Kikwete's wishes, is pure naivette.
Kwa sababu kwenye kinyang'anyiro muhimu alimpitisha Membe akamuacha Lowassa.JK inawezekana ana matatizo yake, mengi tu.
Lakini, kwenye hili la Lowassa.
Mimi sielewi kwa nini JK analaumiwa kwenye hili.
Lowqssa kuiandika hiyo barua alijimaliza mwenyewe.Na JK kutoikataa hiyo barua, ndio hofu kwake ikaanza akiamini kama Lowassa angekuwa Rais, basi angekuja kulipa kisasi.
Pia, uchafu wa Ridhiwani wakati wa utawala wa baba yake, JK akaamua kumtosa Lowassa, ndio maana Ridhiwani akaropoka "Rais hatatoka Kaskazini", kwasababu ya hofu ya kisasi.
Walijua angekuwa Membe ili awalinde, bahati mbaya mambo yakatibuka bahati ikamuangukia Magufuli, hapo tena ikabidi waliokuwa na dili chafu waanze kujisalimisha kwa Magufuli, akiwemo Home Shopping Centre na GSM.
Makubaliano yao yaliitwa; Gentleman's Agreement.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hiyo story ya Sokoine inaonesha Sokoine alivyokuwa kiongozi aliyefanya maamuzi kwa papara, bila kujipanga vizuri wala kusikiliza wenzake.Hiyo stori ya Sokoine na kuleta farasi inaonyesha jinsi gani alikuwa kiongozi anayejali hali za raia wa chini, kama mpango wake huo wa kuwapa wakuu wa Wilaya farasi ungefanikiwa( na kama pia haukuhujimiwa ukizingatia farasi ni mmojawapo ya wanyama wanaovumilia mazingira magumu sana) huenda viongozi wangejibidiisha na leo hii vijiji vyote vingekuwa na lami kuepuka kuendelea kutembelea farasi.
Hiki pia ndicho Lowassa alikuwa akikipigia kelele, kwamba watu wafanye maamuzi katika nafasi badala ya kujizungusha zungusha tu. Akiwa waziri alisimama kidete kwamba tutatumia maji ya Ziwa Victoria kupelekea raia maji safi potelea pote na leo hii maji ya Ziwa Victoria yanatumiwa na mamilioni ya raia.
Sasa mtu kashajiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa, kinyume na ishauri wa rais, JK ampitishe vipi kugombea urais tena?Kwa sababu kwenye kinyang'anyiro muhimu alimpitisha Membe akamuacha Lowassa.
Sasa mbona hata aliyepitishwa na kuupata tena huo Urais baadaye mojawapo ya malalamiko makubwa zaidi kwake ni kufanya maamuzi ya papara!Hiyo story ya Sokoine inaonesha Sokoine alivyokuwa kiongozi aliyefanya maamuzi kwa papara, bila kujipanga vizuri wala kusikiliza wenzake.
Lowassa alijimaliza mwenyewe kisiasa kwa kukubali kujiuzulu, hapa asilaumiwe mtu mwingine yeyote.
This is a logical non sequitur argument.Sasa mbona hata aliyepitishwa na kuupata tena huo Urais baadaye mojawapo ya malalamiko makubwa zaidi kwake ni kufanya maamuzi ya papara!
Mada hii inaweza kuonekana ni nzuri muda huu wakati wa kuuhani msiba wa Lowassa, lakini ghafla pumzi ikimrudia hayati naamini huu uzi utakosa kabisa mashiko.Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.
Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.
Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.
Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.
Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.
Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.
Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.
Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.
Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.
Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.
Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.
Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.
Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.
Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.
Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?
Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.
Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.
Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
in politics there is no permanent enemies....Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Sijui sababu zilizopelekea JK kutoingiza jina la Lowassa katika mojawapo ya majina ya kupelekwa kwa wajumbe kupigiwa kura ila kama ni hiyo sababu ya kujiuzulu kinyume na ushauri wake basi itakuwa sababu dhaifu sana na gubu la aina yake.Sasa mtu kashajiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa, kinyume na ishauri wa rais, JK ampitishe vipi kugombea urais tena?
Mengi hatuyajui na hii mada inatokana na mahaba binafsi ya mkuu Bams kwa hayati Lowassa.Sasa kama kashfa haikuwa ya Lowassa, ilikuwa ya serikali nzima, Lowassa kutaka kujiuzulu yeye ni kimbelembele.
Na mtu kimbelembele anaweza kuleta matatizo katika uongozi.
Ni hivi, ingekuwa Kikwete kamtuma Lowassa ajiuzulu, kamwambia "Edward, haya maji ni marefu, inabidi tumtoe mtu hapa ili kuinusuru serikali, tena mtu mzito, nakuomba kama rafiki yangu ujiuzulu ili kuinusuru serikali, halafu hapo baadaye mambo yakipoa, tutakurudisha ugombee urais nikimaliza mimi".
Halafu Lowassa akasema "Kweli? Serikali inaweza kuanguka? Na mimi kujiuzulu kwangu ndiko kutainusuru? Mnanitaka nijiuzulu halafu nitakuwa rais baada yako? Hapo hakuna shida, najiuzulu"
Halafu Lowassa akajiuzulu.
Halafu baadaye, alipotaka kuwa rais, Kikwete akamruka. Akamkata.
Hapo sawa, ungeweza kusema Kikwete mtu jahili na laghai, kamuhadaa mwenzake ajiuzulu, kwa ahadi kuwa atamfanya awe rais, mwenzake akajiuzulu, na urais akamkata.
Lakini mambo hayakuwa hivyo. Kwa maelezo yako, Kikwete hakutaka Lowassa ajiuzulu. Hata Lowassa alivyotaka kujiuzulu, Kikwete alikataa, Lowassa akalazimisha kujiuzulu.
Sasa hapo mpango wa Kikwete wa Lowassa kuendelea kuwa Waziri Mkuu umekataliwa na Lowassa.
Aliyemsaliti mwenzake kati ya Kikwete na Lowassa ni nani hapo?
Na kama Lowassa alikataa mpango wa Kikwete kuendelea kuwa Waziri Mkuu, kwa nini unafikiri ni sawa Kikwete kukubali mpango wa Lowassa kuja kuwa rais?
Hapa hakuna logical non sequitur wala nini,This is a logical non sequitur argument.
Two wrongs do not make a right.
Tusiikubali papara popote.
Mseme huyo aliyepitishwa naye, tujifunze, tuikatae papara.
Na tunamsema. Tunamsema hapa. Binafsi namsema. Kwangu hii si hoja.
Usihalalishe papara ya aliyekatwa kwa sababu hata aliyepitishwa naye alikuwa na papara.
Usijitoe ufahamu ndugu. Pia Muogope Mungu. Iondoe akili yako kwenye Itikadi za vyama ndipo utakapokuwa na fikra sahihiKwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?
Cha ajabu wanaolia Lia na hili ni Chadema...kama Lowassa aliona Ccm wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema inawauma sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?
Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Mengi hatuyajui na hii mada inatokana na mahaba binafsi ya mkuu Bams kwa hayati Lowassa.
Kuongoza nchi mgombea anachaguliwa na Mungu hajichagui yeye mwenyewe, ukitumia nguvu nyingi sana kuutaka urais unakuwa na shida fulani ambayo kwa nchi za kiafrika ni hatari sana kuwa nayo.
Ikulu kuna biashara gani mpaka mtu atumie pesa kutaka kufika - Julius Nyerere Mei Mosi 1995 uwanja wa sokoine Mbeya.
Imani ya Lowassa kwa rafiki yake ndio iliyomponza.Lowqssa kuiandika hiyo barua alijimaliza mwenyewe.
Hizo nyingine zote ni detail tu.