Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Zamu ya rais muislam kama ilivyo akitoka mkristu ni muislam hivyo hizo ni ndoto
Prof mbarawa kapotezwa sasa hao watatu wataweza labda mwinyi arudi bara kule zanzibar amuachie mwingine kama alivyofanya baba yake
 
Video yenyewe sijaiona abachozungumzia mimi
 
Kwani Dorothy ni Msukuma? Aweso, Byabato, Nchemba,Lukuvi, Mkuchika,Ndumbaro, Mkande, Ummmy, Jaffo, Kitila , Bashungwa, Pinda just to mentioned the few
Waislam ndio wakutafuta kwa tochi katika mawaziri 23 sidhani kama waislam wanafika wa5
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli

Kwani nyie mmeahirisha mazima kuchukua nchi ile 2025? Au ndo Mr Mzungu harudi tena kuja kugombea??
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
Watanzania ,watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Wakati wa muislam JK ulifaidi Nini?
Ulizia wengi watakuambia.
.Ajira tele
. Biashara zilitoka
. Nyumba za nyasi zilikuwa zikifutika kwa Kasi ya 4 G nchi nzima mng'ao wa mabati ulishamiri.
.kilimo kililipa
.
.
.
.
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
acha hizo habari huu utendaji unaujua wewe peke yako.Binafsi ndio ninamfahamu sasa hivi.
 
Na alivifanya vyote hivi kwa sababu ni muislamu?

Amandla...

Waislamu uthamini utu uthamini maendeleo ya watu kuliko vitu.
Dini imewashape na kuwapa hekima na busara.Viongozi wa Kikristo wameacha wajibu wao thus asilimia 90% ya madikteta wote ni Wakristo fanya research.
 
Old perceptions mi kwangu uwezo ndio uwe msingi mkuu.Mama anakuongoza toka zero to 100% anashindwaje kuongoza tena katika mafanikio.kigezo kiwe ni uwezo sio jinsia
 
Mwanamke for President!I am sorry,mwananke hapaswi kumuongoza mwanamna.That is Biblical.Nipigeni madongo na mawe,lakini huo utabaki kuwa ukweli,sitapepesa macho ng'o.We man were created to be leaders,not women.Hii dhana ya wanawake kuongoza wanaume imetoka kuzimu jamani,tuwe makini.

Kwa bahati mbaya sisi bila kujua tumeikumbatia.Halafu mianaume mingine nayo,noma sana, bila aibu inaipigia chapuo.Sijui imelambishwa nini na Wazungu.Shameful indeed.

NGOs hizi zinatuletea vitu vya ajabu sana,mara mfumo dume,mara tohara kwa wanaume,aibu tupu.Mfume dume ndio mnyama gani?
Lakini nchi yetu ni secularist state, hii mitazamo ya kibiblia inachomekwaje hapa? Au ndio mfumo kristo! By the way huko nyuma wametajwa kina Bikra Maria ndani ya bible au chambilecho mama rwakatale hivi kipi bora kuwa na kiongozi shupavu na uanamke wake au kuwa na jianaume goigoi na udume wake '

Huyu Dorothy ni goal oriented ukienda kwenye profile yake utajifunza mengi kwa hiki ninachosema
 
ANAANDIKA PROFESA IDINDILI(CLINICAL EPIDEMIOLOGY AND PUBLIC HEALTH)

Dr. Dorothy,Waziri Mpya wa Afya ni mnyiramba kamilifu. Ni mchapa kazi sana. Alianzia kazi Wilaya ya Bagamoyo, kama ilivyo ada ya wabongo. Juhudi zake zilimponza hakupendwa kabisaa na watumishi wazembe. Akiwemo Daktari wa Wilaya wa wakati huo ( jina kapuni). Ili kupumuzika majungu allikwenda Denmark kusoma masters.

Huku nyuma wauwaji wa maono wakampiga danadana akapelekwa wilaya ya Iramba kama DMO. Kwa kifupi alitupwa porini. Mungu wa Yusuf alikwenda naye huko. Clinton foundation wakaanzisha project ya Solar powering health facilities zisizo na umeme na Wilaya yake ya Iramba ikachaguliwa. Aliusimamia mradi kama mali ya baba yake.

Huku akiikataa rushwa kama ukoma. Enzi za kutesa kwa zamu hizo, yeye alisimama ktk imani yake. Ili kuponya kipato chake. Alijiongeza kwa kilimo cha alizeti. Msimu mmoja alivuna gunia 500. Akfurahia maisha ya Gerezani ( according to Bagamoyo tyrants). Indicators za child survival ambazo zilikuwa kipao mbele kwenye millennium Development Goals zilipaaa kuliko Wilaya yoyote Tanzania,

Viongozi wakampandisha cheo na akawa RMO singida. Akiwa RMO aliendelea kujituma. Alishawishi kuanzishwa ujenzi wa hospital ya mkoa yenye hadhi ya mkoa. Na ikaanza kujengwa law awamu. Wakati hayo yakiendelea alilima ekari 100 za alizeti. Kwa bidii hii viongozi wakampandisha cheo akaletwa wizarani kama associate Director health services.

Kazi ambayo hakuipenda maana haina maamuzi na watu wizarani ni goigo. Halafu Dar hakuwa na shamba. Kwa kifupi alisoteshwa kwa miaka kadhaa. Ashukuliwe Mungu serikali kuhamia Dodoma. Ikamsogeza shambani kwake. Alifufuka kiutendaji na ndipo alipoteuliwa kuwa naibu katibu mkuu baada ya mabadiriko yaliyo mpeleka Dr.Mpoki ubalozi.
Kwa haki bin haki Dorothy amepata uwaziri kwa performance.
Mungu amubariki na kumufanikisha kutuongoza. Naami wizara anaifahamu sana.

-By Prof.Idindili..professor of Clinical Epidemiology and Public Health.
 
Back
Top Bottom