Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Hakuna waziri mkuu,aliwahi kuwa raisi hapa Tz ukiondoa first president
Hukusikia hotuba ya rais siku anawaapisha nawaziri kabudi na mpango, alimsifia sumaye kuvunja rekodi ya miaka 10 ktk uwaziri mkuu!! Hii ilikuwa meseji sent kuwa kasim majariwa nae atavunja rekodi ya waziri mkuu kuwa rais.

Over.
 
Kwahiyo mama yako ni kiumbe wa kuzimu?
Kitu gani kinakufanya uwe na wazo hili mkuu?Mimi nimesema kwamba wazo la mwanamke kumuongoza mwanamme origin yake ni kuzimu,kwa kuwa linakwenda kinyume na maagizo ya Mungu,and Satan always goes against Gods principles.

Unajua Mungu hakumuweka mwanamke hata kuongoza familia,alimuweka mwanamme.So kama Mungu aliona mwanamke hawezi kuongoza hata the smallest unit,a family,how can she lead a nation of more than 56million!Msifanye utani katika mambo muhimu.
 
ANAANDIKA PROFESA IDINDILI(CLINICAL EPIDEMIOLOGY AND PUBLIC HEALTH)

Dr. Dorothy,Waziri Mpya wa Afya ni mnyiramba kamilifu. Ni mchapa kazi sana. Alianzia kazi Wilaya ya Bagamoyo, kama ilivyo ada ya wabongo. Juhudi zake zilimponza hakupendwa kabisaa na watumishi wazembe. Akiwemo Daktari wa Wilaya wa wakati huo ( jina kapuni). Ili kupumuzika majungu allikwenda Denmark kusoma masters.

Huku nyuma wauwaji wa maono wakampiga danadana akapelekwa wilaya ya Iramba kama DMO. Kwa kifupi alitupwa porini. Mungu wa Yusuf alikwenda naye huko. Clinton foundation wakaanzisha project ya Solar powering health facilities zisizo na umeme na Wilaya yake ya Iramba ikachaguliwa. Aliusimamia mradi kama mali ya baba yake.

Huku akiikataa rushwa kama ukoma. Enzi za kutesa kwa zamu hizo, yeye alisimama ktk imani yake. Ili kuponya kipato chake. Alijiongeza kwa kilimo cha alizeti. Msimu mmoja alivuna gunia 500. Akfurahia maisha ya Gerezani ( according to Bagamoyo tyrants). Indicators za child survival ambazo zilikuwa kipao mbele kwenye millennium Development Goals zilipaaa kuliko Wilaya yoyote Tanzania,

Viongozi wakampandisha cheo na akawa RMO singida. Akiwa RMO aliendelea kujituma. Alishawishi kuanzishwa ujenzi wa hospital ya mkoa yenye hadhi ya mkoa. Na ikaanza kujengwa law awamu. Wakati hayo yakiendelea alilima ekari 100 za alizeti. Kwa bidii hii viongozi wakampandisha cheo akaletwa wizarani kama associate Director health services.

Kazi ambayo hakuipenda maana haina maamuzi na watu wizarani ni goigo. Halafu Dar hakuwa na shamba. Kwa kifupi alisoteshwa kwa miaka kadhaa. Ashukuliwe Mungu serikali kuhamia Dodoma. Ikamsogeza shambani kwake. Alifufuka kiutendaji na ndipo alipoteuliwa kuwa naibu katibu mkuu baada ya mabadiriko yaliyo mpeleka Dr.Mpoki ubalozi.
Kwa haki bin haki Dorothy amepata uwaziri kwa performance.
Mungu amubariki na kumufanikisha kutuongoza. Naami wizara anaifahamu sana.

-By Prof.Idindili..professor of Clinical Epidemiology and Public Health.
Alivyoanza kwa kusema "ni mnyiramba kamilifu" nimemuelewa, anajaribu kukwepesha hoja ya usukuma. Idindili ni msukuma.
Hayo mengine ni mchanganyiko wa majungu na sifa zisizohusika, mfano kuwa mkulima wa alizetiinahesabiwaje kwenye uchapakazi ndani ya wizara ya afya? kilimo cha alizeti ni mojawapo ya core businesses za wizara ya afya?
 
Waja wanaikuza kuliko uhalisia wake, tumpe mda, ummy naye did well KWA hyo wizara hasa kipindi kigumu Cha corona
Huyo mama kwa wasio mwelewa huwa anaongea vitu ambayo hata yeye usimwambia avitekeleze hawezi .kuna siku aliwaambia madmo wao wananunua computer kila mwezi ili hali anajua kuna bajet na mpango wa Manunuzi ambao hauruhusu huo ujinga
 
Usimfanannishe Dr Dorothy Gwajima na vitu vya hovyo hovyo kama UMMY Mwalimu. Dr Gwajima ni professional, ni mbunifu wa mifumo na ni mfuatiliaji mzuri kwenye malengo. Ni mchapa kazi na mwaminifu.

Huyo UMMY Mwalimu ndiye alikuwa msimamizi Mkuu wa MSD. Jiulize mpaka yule Mkurugenzi Bwanakunu anatakatisha fedha, je Waziri alikuwa hajui?
UMMY na Bwanakunu anatakatisha fedha kupitia Bahari Pharmacy ambaye walimpa zabuni nyingi za dawa ikiwapo delivery kits.

Najuwa kuwa Rais anajuwa kuwa UMMY ni fisadi ndiyo maana kampeleka kwenye Wizara ambayo siyo nyeti.
Huyo mama kufanya nini cha maana zaidi ya kumsifia raisi kila anapoenda na ndio maana pia ya huu uteuzi .yeye badala kuwa mifumo ya uwajibika anahimiza watu wajaze makaratasi
 
Usipinge tu in three minutes za hiyo video mama kawafundisha hospital inventory management ya dawa, kawapa tips za kufanya audits wakurugeni vitu vingine ni commonsense ata kama wao sio medics, kazungumzia succession planning; halafu yeye ni daktari wa binadamu.

Alichoonyesha sio kwamba yeye ni M.D tu but she is well aware on the management side of things, very very broad anaonekana kwenye health management pia..

Uwezi kumfananisha Ummy Mwalimu na huyo mama wala katibu Mkuu wizara ya afya ambae nae ni M.D by trade, mama anaonekana ni level nyingine.

But then inabidi uwe na ufahamu wa health management ili uone how broad she is.
Sasa yeye alikuwa dmo sijui rmo anaweza kuonyesha hata auditing aliyowahi kuifanya
 
Gwajima Ni msimamizi nzuri,Wala sio kiongozi nzuri....subirini mtaona!
kazi ya waziri katika wizara ni kusimamia wizara na kuhakikisha inatekeleza yale yote yaliyopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu, mtendaji katika wizara ni katibu, hivyo basi kama unajaribu kupotosha watu ukidhani gwajima atafeli kwenye uwaziri umebugi kwani tayari majibu unayo kua yeye ni msimamizi mzuri na sio mtendaji
 
Wewe kweli ni Profesa? Unatuambia kuwa huyu unaemsifia alipandishwa cheo kuwa associate Director kwa sababu alilima ekari 100 za alizeti? Seriously. Kwa jinsi ulivyoandika mhusika alistahili zaidi kuwa waziri wa kilimo.

Amandla...
Ndio ujinga mwingine huo yeye alikuwa analima alizeti ekari 100 sijui huo muda wa kusimamia indicator ilitoa wapi .huku yeye anataka watumishi wafanye kazi kwa masaa 18 ili potelea mbali kwa mishahara ile ile
 
Sasa yeye alikuwa dmo sijui rmo anaweza kuonyesha hata auditing aliyowahi kuifanya
Nyakati hizo alikuwa ni M.D tu ukisoma CV yake utaona kuna miaka alichukua break ya kazi na kwenda kufanya masters ya ‘public health’ much to do with managerial side of things na chances ukute ata Phd yake ni ya mambo hayo hayo ya health management.

Kwa ivyo huo uelewa wake inaonekana umekuja baada ya kutoka kwenye operation levels alipoenda kujiongeza (hizi ndio sababu baadhi ya watu for some time tumekua tukipiga kelele kuendesha afya inabidi Kiongozi awe walau na managerial skills).

Sitegemei atatue kila kitu besides mambo mengine yanataka investment in human capital. Ila sina shaka with full control powers kutakuwa na mabadiliko however training is required to add skills at floor level, implementation of systems anazozinadi with control na regular performances appraisals. But huyu mama ni knowledgable hilo halina ubishi.
 
Huyu ndio atakuwa Waziri wa Kwanza Kutumbuliwa.

Wizara ya Afya haitaki Waziri alie Somea mambo ya Afyaa Lazima Atapishana na Muheshimiwa
 
Huyo mama kwa wasio mwelewa huwa anaongea vitu ambayo hata yeye usimwambia avitekeleze hawezi .kuna siku aliwaambia madmo wao wananunua computer kila mwezi ili hali anajua kuna bajet na mpango wa Manunuzi ambao hauruhusu huo ujinga
Dah hajui hata procurement procedures zilivo
 
Kwani Dorothy ni Msukuma? Aweso, Byabato, Nchemba,Lukuvi, Mkuchika,Ndumbaro, Mkande, Ummmy, Jaffo, Kitila , Bashungwa, Pinda just to mentioned the few
Mkuu, hivi Kitila ni kabila gani? Natafuta wenye asili ya majina hayo wanatokea mkoa gani lakini sijapata elewa
 
Ukweli mchungu ni kwamba hao mawaziri ni geresha tu,mtu mmoja ndiye Rais na waziri wa wizara zote!
1178909.jpg
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
Hakuna msomi atakayetumia elimu yake katika utawala huu ,kuna wasomi walijaribu wakaishia kutumbuliwa....Hao walioteuliwa ni kwa ajili ya kupokea maelekezo kutoka kwa jeshi la mtu mmoja.
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
Mnataka kufanya nchi ya WASUKUMA peke yao, bila haya kabisa, !!!
 
Back
Top Bottom