Kwa dunia ya leo, sishauri mwanaume aoe mwanamke asiyekua na elimu ya walau diploma

Kwa dunia ya leo, sishauri mwanaume aoe mwanamke asiyekua na elimu ya walau diploma

Muombe Mungu akujaalie m.ke mwema

Kazi ya kuchagua mke mwachie Mungu ww omba dua tu Mungu atakujulisha kwa njia usiyoitarajia
Usisahau, Mungu ampe wa kufanana nae 😂😂
Sio mtu aombe mke mwema ilhali yeye sio mwema.
 
Huyo aliyesoma wengi wako wakiwa chuo wanaingia Kwenye ndoa isiyo rasmi, hivyo Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mume mdogo.
 
Kulea Watoto hata kuku analea vifaranga.
Sasa itategemea mtoa post anataka Watoto wake wakuzwe vipi.
Malezi sio tuu kumpa mtoto chakula na kumvalisha, kuna ishu ya mtizamo/attitude, falsafa, maarifa n.k.
Kama Mama hana Elimu na uelewa mzuri atawakuzaje Watoto katika mtazamo anaoutaka Mtoa Post?

Mama akiwa poyoyo kuna uwezekano wa asilimia 90% Watoto wakawa vivyohivyo.
Kwa sababu malezi yanatoka Kwa Mama.
Kuna tofauti kubwa kati ya elimu na akili. Wapo wengi wenye akili kubwa walioishia la saba kuliko wenye PhD. Mtu akiwa na akili hata kama hajaenda darasani ni rahisi sana kuweka misingi mizuri ya kulea familia katika namna unavyopenda
 
Achana na mama zetu wale wa miaka ile ya zamani ambao wengine hawakusoma kabisa ila maisha yalikua poa tu kwa upande wao.

Nazungumzia hawa wanawake wa kizazi hiki wasiokua na elimu ya walau Diploma, yani wana reasoning capacity ndogo sana kiasi kwamba huwezi kukaa nao ukajadili core issues za maendeleo.

Nimejaribu kudate nao kama watatu hivi ila nilichoambulia ni kero tu, uelewa wao wa Mambo uko chini kiasi kwamba unajiuliza huyu ukimuoa ukaishi nae ndani atakua na mchango gani katika maisha yako ya kila siku zaid ya kuwa mzigo tu?

Wanaume wenzangu siwashauri muoe mtu ambae hana shule kichwani aisee.
Utopolo mtupu. Kwanini? Ukishindwa wewe usidhani wote ni kama wewe. Kila mmoja anapaswa kuoa mwanamke amtakaye na siyo wa kushauriwa nawe. Hakuna mpumbavu atakayekubaliana na himitimisho mjumuisho kama hili lisilo na ushahidi wala mashiko
 
Back
Top Bottom