Kwa dunia ya leo, sishauri mwanaume aoe mwanamke asiyekua na elimu ya walau diploma

Kwa dunia ya leo, sishauri mwanaume aoe mwanamke asiyekua na elimu ya walau diploma

Muombe Mungu akujaalie m.ke mwema

Kazi ya kuchagua mke mwachie Mungu ww omba dua tu Mungu atakujulisha kwa njia usiyoitarajia
Munatumia vibaya Sana hili andiko kwahiyo unaposema Mungu atakujulisha kwahiyo Mungu atakufata na kukuonesha huyu n mwema You need to hustle kuweka standard zako na kuwa strategy huku unaomba Mungu maisha ya sasa kiuchumi yanahitaji uwe smart Sana ndio uwe na uchumi wakueleweka kwenye familia jitahidi uwe na taleast aliye na elimi ya certificate
 
Kweli kabisa suala la kuoa linahitaji mke mwema kwanza hicho ndo kitu cha awali kuliko vyote, diploma yake haitakusaidia kitu kama siyo mwanamke anae jitambua
Munachanganya mambo Sana, hili awe mke mwema means inabidi kwanza awe mke ndio awe na sifa ya mke mwema first time unavyo meet mwanmke huwezi jua ni mke mwema au sio mwema You see ila Kuna criteria zako za mwanzo muoneoano, mavazi, rangi nk ndipo Happ jamaa kashauri pia zingatia na Elimu Kama sifa ya mwanzo nafikiri baada ya kuanza nae mahusiano huyu mwanamke ndipo utajua je Ni mwema au sio mwema lakini hizi sifa za mwanzo ushapitisha.
 
Dogo kaangalie sinema zetu movie za kibongo zimeshakuharibu
 
Me na mwalimu wangu ana certificate tu inamtosha.
Certificate huyo ana elimu yofauti na darasa la saba ukweli darasa la saba wa huku mitaani Hali sio nzuri kabisa utaelewa ukiwa unaishi uswazi
 
ninaona wanaume wanahitaji mwanamke anayejitambua na anataka mwanaume wa aina gani kwenye ndoa.
ndoa haihitaji elimu kubwa maana unaweza oa mwanamke anaelimu ila elimu ya maisha ya kawaida hana au social skills hana au hata hajui namna ya kutumza watoto wake.

kikubwa wanaume tafuteni wanawake wanaojitambua na wanaoweza kujisimamia mengine hayo jamani mutapeana semina kwenye ndoa kuhusu elimu ya darasani
Mwanamke aliueishia lasaba anakuwa na Social Skills gani??
 
Hapa tupo wote mkuu,..mwenye AKILI, japo njia rahisi ya kumpata mwenye akili ndio hiyo shule.
Nilitaka nimjibu jamaa nikaacha, Anaandika kumuomba Mungu kupata kitu X bila hata ya kujua inabidi yeye mwenyewe ajue njia yakuoata hiko kitu X ndio Mungu aingize neema zake ....JF imekuwa na watu wenye Reasoning ndogo Sana sikuhizi
 
Uko sahihi kabisa kwamba mwenza angalau awe na uelewa wa kuchakata na kusaidia akili ya mwanaume kukabiliana na changamoto za maisha .
Lakini naweza sema haupo sahihi unaposema angalau awe na diploma na kuendelea.

Hoja yangu ya msingi imelala hapo kwanza unatakiwa ujue kuna tofauti ya kati ya kuwa na elimu na kuwa na akili (uelewa wa kuchanganua mambo).
Ukichukua Sample zako huku wanawake 10 wenye Certificate na huku wanawake 10 walioishia lasaba ninauhakika upande wa Certificate utapata wengi walio na akili na uwelewa ambao wanaume wengi tunayaka wake zetu wawe nao tatizo mjadara umegeuka kushambulia Degree na Kutafuta huruma kwa Mungu Kama kunakufuru fulani.
 
Unaweza pata huyo mwenye diploma halafu kukawa hakuna amani ndani na hizo core issues za maendeleo ukawa unajadili bar na walevi wenzio.

Kuna jamaa yangu alikuwa kaoa graduate mwenzie,kila akimshirikisha wazo la kubuni mradi wa maendeleo wa familia ili wote wachukue mikopo wawekeze anaulizwa,"Je tukiachana?".
 
Ukichukua Sample zako huku wanawake 10 wenye Certificate na huku wanawake 10 walioishia lasaba ninauhakika upande wa Certificate utapata wengi walio na akili na uwelewa ambao wanaume wengi tunayaka wake zetu wawe nao tatizo mjadara umegeuka kushambulia Degree na Kutafuta huruma kwa Mungu Kama kunakufuru fulani.
Hakuna anaeshambulia degree hapa tunaweka mambo sawa, issue ya kuoa ni hisia ambayo inagusa tokea ndani ya moyo wa mtu kwa wawili kushibana, na ndio maana utasikia msemo usemao mapenzi hayana formula.
Ukiingia kitaa utakuta kuna wenye elimu na wasio na elimu wote hawaja olewa.
Suala la kumpata mwenza inabidi umuombe Mungu akuchagulie ila macho yako ndio yaone usije jutia baadae.
 
Wewe wewe wewe!
Ungejua wala hata usingesema hayo.
Wacha niishie hapo tu.
 
Mwanamke ambaye hana hata kadiploma Kwa kweli ni changamoto. Wengi wanashindwa vitu vidogo vidogo tu.
Mfano, wanashindwa hata kusupervise watoto kukamilisha homework, mpaka baba urudi.

Mara kabonyeza remote sehemu asiyoijua, haelewi lugha anapoteza hela kumuita fundi, maelekezo madogo madogo tu ya bidhaa (mfano dawa) hawezi kusoma na kuelewa mpaka upigiwe simu.

Hata ukitaka kutoka naye kumeet na rafiki zako ambao si wazungumza Kiswahili anaogopa kwenda, anazugazuga tu kumbe confidence sifuri.
Changamoto zao ni nyingi.

Na Kwa Tanzania ya leo kama mtu hana hata kadiploma basi amekulia mazingira hatarishi (most likely ana fixations kibao au traumas za utotoni) au ni juha. Haelewi a wala be na utalipa sana walimu wa tuition za nyumbani.
Point!
 
Back
Top Bottom