Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Haiwezi ikatokea tu kila mwananchi anawaza ajira au wananchi wapende biashara za kuimport ujue kuna shida mahali kwenye mfumo
kila msomi anawaza ajira wanaowaza biashara ni watu ambao hata darasa hawalijui, mfano umesema medicine mpaka umemaliza unawaza pharmacy hujasema ndoja tutengeneze dawa alafu unategemea nn? maaana pharmacy nae anaagiza mzigo, shhida kubwa ndo ipo apo
 
Kwa miaka mingi sana, nimekuwa mfuatiliaji wa CV za Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali duniani.

Katika ufuatiliaji wangu, miaka yote kwenye mataifa mbalimbali, Magavana wa Benki Kuu wamekuwa wakiteuliwa wabobezi wa masuala ya Uchumi , Fedha au Sheria na wenye uzoefu wa kufanya kazi katika eneo la uchumi ndani na nje ya nchi zao. Pia wenye uzoefu wa kufanya kazi kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha zenye historia ya kufanya vizuri kwenye masuala ya Fedha.

Kwenye mataifa mbaimbali, nafasi ya Gavana wa Benki Kuu inahusisha kuteuliwa watu wenye PhD katika masuala ya Uchumi, Fedha na Biashara au Sheria. Hata kama asipokuwa na PhD basi anapaswa kuwa mtu mwenye rekodi ya outstanding performance kwenye masuala ya Fedha, Uchumi na Sheria.

Kwa utafiti wangu mdogo, haya hayafanyiki kwa bahati mbaya. Gavana wa Benki Kuu anapaswa kuwa kichwa cha nchi kwenye suala nyeti la uchumi. Anapaswa kuwa mshauri wa mwisho pale nchi inapokuwa kwenye crisis yeyote ya kiuchumi.

kwenye kufanya haya anatakiwa awe mbobezi sana kwenye masuala ya uchumi. Anatakiwa kuwa na exposure kubwa sana ya kimataifa na kitaaluma katika masuala ya kiuchumi.

Nakumbuka wakati Emmanuel Tutuba anateuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu niliwahi toa maoni yangu kuwa ule haukuwa uteuzi sahihi.

Kwa haya matokeo ya shilingi yetu kufanya vibaya zaidi nadhani sasa niko sahihi nikisema uteuzi wa Tutuba kuwa Gavana wa Benki Kuu haukuwa sahihi. Ni bahati mbaya sana mamlaka za Uteuzi nchi hii hazihojiwi kutokana na kuwa na Katiba mbovu.

Angalieni wenyewe biography kwa kifupi za Gavana wetu wa Benki Kuu alafu linganisha na Magavana wa Mataifa mengine.

Hii ndo Bio ya Gavana wetu Tutuba
👇- Amesoma Diploma Mzumbe na Master kwenye chuo hiko tena kipindi kinachojulikana kuwa Chuo hiko hakikuwa Chuo chenye hadhi ya Chuo Kikuu hata kwa Tanzania. Zaidi kafanya kazi public sector tu tena Tanzania.
View attachment 3282699

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Kenya👇
View attachment 3282700

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Uganda👇
View attachment 3282701

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu ya Marekani. Hana PhD ya Uchumi ila angalia rekodi yake ya utendaji kwenye sekta ya Umma na sekta binafsi hasa kwenye firms zinazotambulika vizuri Marekani kwenye masuala ya Fedha na Mitaji👇
View attachment 3282704


Mwisho.
Ni hitimisho langu kuwa Tanzania tupambane sana kupata Katiba Mpya maana tutapata watu wasiostahili kwenye nafasi za juu hadi tutajikuta tunazikwa kabisa kimaendeleo na Kiuchumi.
Kigezo kikubwa uwe ni mwana CCM na uko tayari kumtaja rais kwa kila kitu
 
Dr. Musukuma je atafaa? Maana issue kama ni U Dr hata Musukuma si Dr tu, watu wanafanya utani sana na Elimu. Just as a reminder, Elimu bora na sahihi haina alternative hadi sasa, period.
 
Cv, CV. Hao wenye CV zilishiba wameifanyia nini cha maana nchi hii? Wengi wao ni mafisadi
tu. Wizara ya Fedha ambayo Gavana yupo chini yake inaongozwa na Waziri mwenye taaluma ya Uchumi na mambo ya fedha tena mwenye Cv iliyoshiba. Ingekuwa CV iliyoshiba inasaidia, angeweza kusaidia shilingi isiporomoke.
Tutafute sababu nyingine tusisingizie mamboya CV kwenye suala hili.
Mgonjwa akifia mikononi kwa daktari bingwa isikupelekee kutafuta matibabu bucha ukiugua.
 
kila msomi anawaza ajira wanaowaza biashara ni watu ambao hata darasa hawalijui, mfano umesema medicine mpaka umemaliza unawaza pharmacy hujasema ndoja tutengeneze dawa alafu unategemea nn? maaana pharmacy nae anaagiza mzigo, shhida kubwa ndo ipo apo
Watu unafikiri hawafanyi ushawahi hata kufungua kampuni ukaona msururu wake hatuna mfumo mzuri wa kuwezeshana kiongozi, hizo dawa unaweza ukazalisha afu serikali wakanunua dawa za watu wa nje
 
izi ni political narratives ila kinachosababisha effect za pesa ni TRANSACTIONS, wananchi wananunua sana nje hakuna unachoweza kufanya ndo hali halisi, kila mwananchi anawaza ajira badala ya kufungua biashara zenye exports gavana unamuonea bure
Overly simplifying a complex subject.

Common sense tu inatuambia tupeleke best minds kutufanyia shughuli yoyote yenye umuhimu. Ndio la msingi
 
Watu unafikiri hawafanyi ushawahi hata kufungua kampuni ukaona msururu wake hatuna mfumo mzuri wa kuwezeshana kiongozi, hizo dawa unaweza ukazalisha afu serikali wakanunua dawa za watu wa nje
hakuna sehem yoyote duniani kuanzisha biashara ni rahisi, nature ya biashara ni ugumu ndo maaana mafanikio wanapata wenye uthubutu, ukwel ni kwamba wengi sisi ni wavivu
 
Overly simplifying a complex subject.

Common sense tu inatuambia tupeleke best minds kutufanyia shughuli yoyote yenye umuhimu. Ndio la msingi
ata tukikuweka wewe pale kama wananchi hawana mawazo ya kimaendeleo ni kazi bure, nature ya wnanchi wa tz ni uvivu na kupenda kurusha lawama
 
Overly simplifying a complex subject.

Common sense tu inatuambia tupeleke best minds kutufanyia shughuli yoyote yenye umuhimu. Ndio la msingi
na pia tatizo lingine kila mtu aliepo apa jamii forum ni mjuaji kila kitu tunajua, hilo ni tatizo
 
kila msomi anawaza ajira wanaowaza biashara ni watu ambao hata darasa hawalijui, mfano umesema medicine mpaka umemaliza unawaza pharmacy hujasema ndoja tutengeneze dawa alafu unategemea nn? maaana pharmacy nae anaagiza mzigo, shhida kubwa ndo ipo apo
una hoja ya kusikilizwa mkuu
 
Dr. Musukuma je atafaa? Maana issue kama ni U Dr hata Musukuma si Dr tu, watu wanafanya utani sana na Elimu. Just as a reminder, Elimu bora na sahihi haina alternative hadi sasa, period.
Hiyo dr ilipigwa chini na wizara ya elimu, so technicaly haipo
 
Back
Top Bottom