Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Afisa tu hapo Wizara ya Fedha. Alipanda hadi kuwa Kamishna ya Bajeti kama sikosei vyeo ambavyo vinajulikana vya kupeana tu ili unyooshe vizuri masuala ya Wanasiasa hasa wizi. Baadae alikuwa Katibu Mkuu kabisa.

Pathetic Nation.
Magufuli aliyekuwa na PHD tulimzonga mpaka Saanane akapoteza maisha akiwa kijana mdogo.

Huyu gavana tunamzonga kwa kisingizio cha elimu ndogo, vipi kuhusiana na ukweli kwamba anaweza kuwa amejiendeleza akiwa hapo hapo kazini?.

Waafrika tunao ushamba wa kudanganywa na vyeti ni mgumu sana kututoka.
 
Kwa miaka mingi sana, nimekuwa mfuatiliaji wa CV za Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali duniani.

Katika ufuatiliaji wangu, miaka yote kwenye mataifa mbalimbali, Magavana wa Benki Kuu wamekuwa wakiteuliwa wabobezi wa masuala ya Uchumi , Fedha au Sheria na wenye uzoefu wa kufanya kazi katika eneo la uchumi ndani na nje ya nchi zao. Pia wenye uzoefu wa kufanya kazi kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha zenye historia ya kufanya vizuri kwenye masuala ya Fedha.

Kwenye mataifa mbaimbali, nafasi ya Gavana wa Benki Kuu inahusisha kuteuliwa watu wenye PhD katika masuala ya Uchumi, Fedha na Biashara au Sheria. Hata kama asipokuwa na PhD basi anapaswa kuwa mtu mwenye rekodi ya outstanding performance kwenye masuala ya Fedha, Uchumi na Sheria.

Kwa utafiti wangu mdogo, haya hayafanyiki kwa bahati mbaya. Gavana wa Benki Kuu anapaswa kuwa kichwa cha nchi kwenye suala nyeti la uchumi. Anapaswa kuwa mshauri wa mwisho pale nchi inapokuwa kwenye crisis yeyote ya kiuchumi.

kwenye kufanya haya anatakiwa awe mbobezi sana kwenye masuala ya uchumi. Anatakiwa kuwa na exposure kubwa sana ya kimataifa na kitaaluma katika masuala ya kiuchumi.

Nakumbuka wakati Emmanuel Tutuba anateuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu niliwahi toa maoni yangu kuwa ule haukuwa uteuzi sahihi.

Kwa haya matokeo ya shilingi yetu kufanya vibaya zaidi nadhani sasa niko sahihi nikisema uteuzi wa Tutuba kuwa Gavana wa Benki Kuu haukuwa sahihi. Ni bahati mbaya sana mamlaka za Uteuzi nchi hii hazihojiwi kutokana na kuwa na Katiba mbovu.

Angalieni wenyewe biography kwa kifupi za Gavana wetu wa Benki Kuu alafu linganisha na Magavana wa Mataifa mengine.

Hii ndo Bio ya Gavana wetu Tutuba
👇- Amesoma Diploma Mzumbe na Master kwenye chuo hiko tena kipindi kinachojulikana kuwa Chuo hiko hakikuwa Chuo chenye hadhi ya Chuo Kikuu hata kwa Tanzania. Zaidi kafanya kazi public sector tu tena Tanzania.
View attachment 3282699

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Kenya👇
View attachment 3282700

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Uganda👇
View attachment 3282701

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu ya Marekani. Hana PhD ya Uchumi ila angalia rekodi yake ya utendaji kwenye sekta ya Umma na sekta binafsi hasa kwenye firms zinazotambulika vizuri Marekani kwenye masuala ya Fedha na Mitaji👇
View attachment 3282704


Mwisho.
Ni hitimisho langu kuwa Tanzania tupambane sana kupata Katiba Mpya maana tutapata watu wasiostahili kwenye nafasi za juu hadi tutajikuta tunazikwa kabisa kimaendeleo na Kiuchumi.
Lazima achaguliwe mtu easily manipulable kufanikisha upigaji
 
Magufuli aliyekuwa na PHD tulimzonga mpaka Saanane akapoteza maisha akiwa kijana mdogo.

Huyu gavana tunamzonga kwa kisingizio cha elimu ndogo, vipi kuhusiana na ukweli kwamba anaweza kuwa amejiendeleza akiwa hapo hapo kazini?.

Waafrika tunao ushamba wa kudanganywa na vyeti ni mgumu sana kututoka.
Hivyo BOT na gavana juu ni sehemu ya kufanya on job training?
 
Tutuba hana distinguished credentials, hilo ni tatizo.

Lakini, tatizo kubwa zaidi ya hilo ni ukweli kuwa Benki Kuu haina uhuru wa kufanya maamuzi kiuchumi, inaendeshwa kisiasa kwa amri kutoka juu.

Ukichanganya hayo matatizo mawili, na tatizo la tatu kuwa aliye juu naye mtupu, unapata bomu la hatari sana.
 
Tunapokosa kazi tunaanza kuwakejeli wasomi wetu kwa kuwalinganisha na wa mataifa mengine hatujui kuwa kwa kufanya hivyo tunajitukana sisi wenyewe!. Aliyeturoga alishakufa.
Kama tunafanya mambo ya kipumbavu kwa nini tusijitukane?

Kwa akili tu ya kawaida! Tanzania tumekosa Wabobezi wa Uchumi na Masuala ya Fedha kuanzia ndani hadi nje ya nchi hadi kufanya Tutuba ndo awe Gavana wa Benki Kuu?
 
Tuseme magavana wa benki kuu za Africa mashariki wakiwa na kikao wa kwetu asiende?
Sasa mfano akienda ataongea nini?

We unaona tu anavyoongeaga kwa kutojiamini kwenye events za ndani tu hasa zinazotumia lugha ya kiingereza. Ndo akakutane na manguli huko nje? Si ataaibika???

Viongozi wa hii nchi wanatufanya Watanzania tudharauliwe sana kwa ujinga wao na kuangalia maslahi binafsi.
 
CCM na maendeleo ya kweli ni vitu visivyoshabihiana, wanapenda taifa liendelee kuwa la hovyo ili wazidi kutawala bila wasiwasi huku wakiendelea kudanganya watu na majengo ya hospitali yasiyo na vifaa na watumishi na majengo ya shule yasiyokuwa na walimu wa kutosha na matundu ya Vyoo ambalo ni hitaji muhimu Kwa binadamu
Nchi hii tuna masihara sana linapokuja suala la kupata maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom