Kwa hali hii; Je, Job anaweza kumuwahi boss wake kwa ile kura ya veto?

Kwa hali hii; Je, Job anaweza kumuwahi boss wake kwa ile kura ya veto?

Hana ushujaa huo alitakiwa asiombe msamaha ila kashachelewa
Ila kachambwa aseee as like watu wa uswahilini na mzee baba Kassim kadhalilishwa sana kuitwa as it jamaa wa mtaani hivi 🙁!.
 
aaha wapi? tukimsema Raisi ana nguvu muelewe, kabla hajaitisha wasiojulikana tayari watakuwa wamemchukua, alafu naibu spika anabutua chini ya mtutu
Naibu spika namuona bado sana hata hivyo hawezi fanya lolote labda kwa muongozo wa watu fulani.
 
Hapa tayari wamesha mpole pole
JamiiForums-1720157624.jpg
 
Hawezi fanya lolote lile jinga la Dodoma, alidekezwa sana, Ebu mwambie ajaribu kutumia kura ya veto? Kwani anayo? Rais anaweza kuvunja bunge wakati wowote, mbili bunge haliwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, bali waziri mkuu. Hivi wewe unajua wabunge wapo upande gani? Ebu kasome katiba acha uvivu.
Mkuu ulivyo andika nikadhani unafahamu kipengele chochote cha katiba kinachosema bunge haliwezi kupiga kura kutokuwa na imani na presida, kumbe nothing!.
 
Unadhani veto wanairukia tu ? Ninekosa Mimi nimekosana Sana .
 
Msitukane kwasababu ya ugogo wangu.. mimi ni mshauri wa askofu na hata kapernaun nimewahi fika kwa mke wa ....
 
Kwa nafasi aliyonayo dhidi ya ule muhimili anaousimamia japo tayari yupo under control, je anaweza kutumia ile kura ya veto na kusema liwalo na liwe akapindua meza kwenye kikao kijacho cha bunge?.

Na ukapigwa 🎶wimbo hatuna imani naye?.🎵
Hawezi, he is finished!, kwishney finito!.
P
 
Hali si shwari kwa wanaofuatilia siasa za nchi hii toka camarada Legendary Pombe alipotoweka dunia.

Pamoja na kuwa katika wakati mgumu kufuatia kushusha siraha nchini na kuonyesha udhaifu kwenye mhimili mwingine.

Kwa nafasi aliyonayo dhidi ya ule muhimili anaousimamia japo tayari yupo under control, je anaweza kutumia ile kura ya veto na kusema liwalo na liwe akapindua meza kwenye kikao kijacho cha bunge?.

Na ukapigwa 🎶wimbo hatuna imani naye?.🎵
Kura ya veto ipi? Speaker hana kura ya veto.
 
Hawezi, he is finished!, kwishney finito!.
P
Kwanza hana hiyo kura ya turufu (veto). Najua unajua kwamba kwa mujibu wa Ibara ya 46A ya Katiba ya JMT, 1977 Bunge linaweza tu kumshitaki Rais ambapo mlolongo wake ni mreeefu ambao naona kuwezekana kwake ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano! Sijaona Speaker akiwa na kura ya turufu kwenye huo mchakato.
 
Kura ya veto ipi? Speaker hana kura ya veto.
Kura ya kutokuwa na imani na rais, pamoja na kuwa na mlolongo mrefu but ndiyo hiyo tunayosema kura ya veto ambayo inampa spika jeuri endapo tu itafanyika.
 
Kura ya kutokuwa na imani na rais, pamoja na kuwa na mlolongo mrefu but ndiyo hiyo tunayosema kura ya veto ambayo inampa spika jeuri endapo tu itafanyika.
Nadhani mkuu hufahamu maana ya kura ya veto! Jishughulishe kusoma mkataba wa UN uone jinsi kura ya turufu/veto inavyofanya kazi kwenye Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa.
 
Back
Top Bottom