Kwa hali hii naamini maneno ya Askofu Gwajima kuwa viongozi wamehongwa ili chanjo ije

Kwa hali hii naamini maneno ya Askofu Gwajima kuwa viongozi wamehongwa ili chanjo ije

Ukimwi ni ugonjwa kwa ajili ya watu wajinga kama wewe

It's a disease for gullible people

Ukimwi ni kiini macho kama ilivyo corona

Endelea na ujinga wako wa kuamini kila unacholetewa na mzungu
Kumbe simu yako imebuniwa na nani? Hayo ni kitoto. Ukila ugali wa mahindi - nani ameileta Afrika? (inaitwa Mahindi kwa sababu Wahispania na Wareno waliamini asili yake Amerika ni Uhindi..)
 
Ni Wapumbavu wakubwa kwa sababu duniani billions of people they got vaccinated and they are just doing fine healthy wise with exception of few.

Yawezekana una uelewa mkubwa wa chanjo za UVIKO-19 hadi kudai hivyo. Kwa faida ya kina Thomas (katika Biblia hakuamini aliyewatokea ni Yesu hadi aliporuhusiwa na kuweka kidole chake kwenye majeraha ya misumali), tuweze kuamua kuchanjwa, tupe majibu ya maswali haya:
[emoji830]︎ nguvu ya chanjo kumkinga aliyechanjwa inakaa muda gani mwilini? Ulaya waliochanjwa kwa sasa wanapewa "booster vaccine" mithili ya "computer updates"; na
[emoji830]︎ Ni muda sasa tangu nchi iletewe chanjo ambazo hazijamalizika:
• uhai wa chanjo (shelf life) ni muda gani?
• Na zihifadhiwe kwa jinsi gani zisiharibike?
• Je, uwezo huo wa kuhifadhi chanjo tunao nchini?
 
Jinga wewe, kila kitu ni kwa mkakati na muda. Umeshaniuliza kwanini kunaongezeko kubwa la wagonjwa wa tezi dume siku za hivi karibuni?

Fuatilia utajua kitu. Mzungu hata kama amepanga kufanya jambo, huenda na time frame.
Pamoja na kuwa sina mpango wa kuwa vaccinated dhidi ya Covid19 lakini huu upumbavu wa conspiracy theories sikubaliani nao kabisa, Wazungu wangekuwa na nia ya kutuangamiza(kutumaliza) wasingetumia njia ambayo iko obvious kama kutumia chanjo.
Kuna dawa nyingi hata za mifugo au mazao, au imported food products au hata lab equipments zitumikazo moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu yaani the list is endless na tungepukutika kama kuku. Argument ya kueleweka ni ya kwamba hakujafanyika research ya kutosha hasa kwenye kufahamu long term effects za chanjo husika, Kibongobongo chanjo ni 'hiari' kwa sasa lakini amini usiamini baadaye kutakuwa na restrictions nyingi kwa wasiochanjwa kama ilivyo kwenye baadhi ya nichi 'zilizoendelea', hii 'hiari' itakuwa ikibadilishwa styles kadri muda unavyokwenda.
Mbele ya safari ni giza nene.
 
Yawezekana una uelewa mkubwa wa chanjo za UVIKO-19 hadi kudai hivyo. Kwa faida ya kina Thomas (katika Biblia hakuamini aliyewatokea ni Yesu hadi aliporuhusiwa na kuweka kidole chake kwenye majeraha ya misumali), tuweze kuamua kuchanjwa, tupe majibu ya maswali haya:
[emoji830]︎ nguvu ya chanjo kumkinga aliyechanjwa inakaa muda gani mwilini? Ulaya waliochanjwa kwa sasa wanapewa "booster vaccine" mithili ya "computer updates"; na
[emoji830]︎ Ni muda sasa tangu nchi iletewe chanjo ambazo hazijamalizika:
• uhai wa chanjo (shelf life) ni muda gani?
• Na zihifadhiwe kwa jinsi gani zisiharibike?
• Je, uwezo huo wa kuhifadhi chanjo tunao nchini?
Chanjo hazijamalizika kivipi? Mamilioni wamepokea, vifo vimepungua.
Ni kawaida, tena tangu zamanbi kwamba chanjo mbalimbali zinahitaji nyongeza baada ya muda.
Mfano: Tetanus na diphteria (dondakoo) kila baada ya miaka 10; kichaa cha mbwa kila baada ya miaka 3-4

Virusi vya Korona kwa jumla hubadilika haraka zaidi (hata kama Polepole alikana habari), na influenza ni mojawapo. Wanafanya update ya chanjo kila baada ya miaka 1-3 wakishauri watu wenye hatari (wazee na wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa) huko Ulaya kuirudia mara aina mpya ya virusi ile ya influenza imegunduliwa na kusambaa.
Kuhusu Covid unaweza kujielimisha, si vigumu: chanjo inasababisha kutokea kwa antibodies mwilini; utafiti umeonyesha idadi ya hizo antibodies inapungua baada ya miezi kadhaa (kwa hiyo inawezakana kuambukizwa tena) lakini hali gumu haitokei tena kwa 90%. (hakuna 100% maishani, isipokuwa kifo).

Kwa hiyo pendekezo (si kote, wataalamu bado wanajadiliana) katika nchi kadhaa ni kwa ajili ya wazee (juu ya miaka60, 70) na wenye kinga kilichodhoofishwa; mfano mtu mwenye presha, usukari, walio na na ukimwi.
Na hapa umesema kweli: ingawa chanjo imekamilika, utathmini wake bado unaendelea. Ni kitu kipya (tena kwa kutumia teknolojia mpya kabisa, hii sababu ya kufanikiwa haraka)

Kutunza chanjo ni changamoto; Pfizer ni gumu zaidi maana inahitaji kutunzwa chini ya -70, baada ya kutolewa inaweza kukaa kwenye jokofu ya kawaida hadi wiki nne. Nje ya jokofu saa 2 pekee.Johnson & Johnson ni afadhali - inatunzwa miaka 2 kwenye -15/-25; miezi mitatu kwenye jokofu (=hadi +8°), halafu saa 3 nje ya friji. Inawezekana mahali pengi nchini, si kote.

Hayo yote si siri (hata kama Polepole alisema kinyume). Hivyo chanjo inahitaji uangalifu, maana kama umeme umekatwa kwa siku na jokofu haiwezi kutunza halijoto ya duni, basi ni lazima kutupa yote. Sijasikia inaleta hasara lakini haisaidii kitu.
Ninaye rafiki aliyepokea chanjo ambayo haikutunzwa vema, basi alipata covid kali baada ya chanjo. Namshukuru Mungu amepona.
Ila kwa jumla shabaha si kuchanja watu wote, lakini
a) wafanyakazi wa mfumo wa afya (wanahitajika)
b) wazee
c) wenye magonjwa yanayodhoofisha kinga cha mwili.

Wengine (ambao ni wengi TZ) si lazima sana kama uwezo haupo; wachache wao watakufa lakini si idadi itakayokwamisha hospitali na uchumi.
 
Kumbe simu yako imebuniwa na nani? Hayo ni kitoto. Ukila ugali wa mahindi - nani ameileta Afrika? (inaitwa Mahindi kwa sababu Wahispania na Wareno waliamini asili yake Amerika ni Uhindi..)
Tumia hiyo simu masaa 24 kila siku uone kama haijakudhuru macho hadi saratani

Kutumia simu ya mzungu haina maana kila anacholeta ni kizuri

Halafu kuchanja ni hiyari, anayetaka achanje ila mimi sichanji.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
😂😂😂 Chanjo za TB, ndui, pepo punda, polio, yellow fever na madawa chungu nzima ya MABEBERU Waafrika tumemeza au kunywa kwa miaka mingi. MABEBERU wangetaka kutuua mbona kungekuwa hakuna hata Muafrika mmoja duniani? Baadhi ya Watanzania wana ufinyu mkubwa wa akili.
Kwa a,klk yako unachani ni watanzania wanaopinga tu ndio wanaopinga chanjo! Pole sana!! Kwa taarifa yako upinzani mkubwa wa chanjo uko marekani na ulaya !
 
Back
Top Bottom