Yawezekana una uelewa mkubwa wa chanjo za UVIKO-19 hadi kudai hivyo. Kwa faida ya kina Thomas (katika Biblia hakuamini aliyewatokea ni Yesu hadi aliporuhusiwa na kuweka kidole chake kwenye majeraha ya misumali), tuweze kuamua kuchanjwa, tupe majibu ya maswali haya:
[emoji830]︎ nguvu ya chanjo kumkinga aliyechanjwa inakaa muda gani mwilini? Ulaya waliochanjwa kwa sasa wanapewa "booster vaccine" mithili ya "computer updates"; na
[emoji830]︎ Ni muda sasa tangu nchi iletewe chanjo ambazo hazijamalizika:
• uhai wa chanjo (shelf life) ni muda gani?
• Na zihifadhiwe kwa jinsi gani zisiharibike?
• Je, uwezo huo wa kuhifadhi chanjo tunao nchini?
Chanjo hazijamalizika kivipi? Mamilioni wamepokea, vifo vimepungua.
Ni kawaida, tena tangu zamanbi kwamba
chanjo mbalimbali zinahitaji nyongeza baada ya muda.
Mfano: Tetanus na diphteria (dondakoo) kila baada ya miaka 10; kichaa cha mbwa kila baada ya miaka 3-4
Virusi vya Korona kwa jumla hubadilika haraka zaidi (hata kama Polepole alikana habari), na
influenza ni mojawapo. Wanafanya update ya chanjo kila baada ya miaka 1-3 wakishauri watu wenye hatari (wazee na wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa) huko Ulaya kuirudia mara aina mpya ya virusi ile ya influenza imegunduliwa na kusambaa.
Kuhusu
Covid unaweza kujielimisha, si vigumu: chanjo inasababisha
kutokea kwa antibodies mwilini; utafiti umeonyesha idadi ya hizo antibodies inapungua baada ya miezi kadhaa (kwa hiyo inawezakana kuambukizwa tena) lakini
hali gumu haitokei tena kwa 90%. (hakuna 100% maishani, isipokuwa kifo).
Kwa hiyo pendekezo
(si kote, wataalamu bado wanajadiliana) katika nchi kadhaa ni kwa ajili ya wazee (juu ya miaka60, 70) na wenye kinga kilichodhoofishwa; mfano mtu mwenye presha, usukari, walio na na ukimwi.
Na
hapa umesema kweli: ingawa chanjo imekamilika, utathmini wake bado unaendelea. Ni kitu kipya (tena kwa kutumia teknolojia mpya kabisa, hii sababu ya kufanikiwa haraka)
Kutunza chanjo ni changamoto; Pfizer ni gumu zaidi maana inahitaji kutunzwa chini ya -70, baada ya kutolewa inaweza kukaa kwenye jokofu ya kawaida hadi wiki nne. Nje ya jokofu saa 2 pekee.Johnson & Johnson ni afadhali - inatunzwa miaka 2 kwenye -15/-25; miezi mitatu kwenye jokofu (=hadi +8°), halafu saa 3 nje ya friji. Inawezekana mahali pengi nchini, si kote.
Hayo yote si siri (hata kama Polepole alisema kinyume). Hivyo chanjo inahitaji uangalifu, maana kama umeme umekatwa kwa siku na jokofu haiwezi kutunza halijoto ya duni, basi ni lazima kutupa yote. Sijasikia inaleta hasara lakini haisaidii kitu.
Ninaye rafiki aliyepokea chanjo ambayo haikutunzwa vema, basi alipata covid kali baada ya chanjo. Namshukuru Mungu amepona.
Ila kwa jumla shabaha si kuchanja watu wote, lakini
a) wafanyakazi wa mfumo wa afya (wanahitajika)
b) wazee
c) wenye magonjwa yanayodhoofisha kinga cha mwili.
Wengine (ambao ni wengi TZ) si lazima sana kama uwezo haupo; wachache wao watakufa lakini si idadi itakayokwamisha hospitali na uchumi.