Kwa hali hii siwezi kuiamini VAR inayoongozwa na binadamu. Goli la Iran ni halali kabisa

Kwa hali hii siwezi kuiamini VAR inayoongozwa na binadamu. Goli la Iran ni halali kabisa

Mimi huwa siwaelewi kabisa, egypt ni afrika, iran ni Asia ila hapo mleta mada unaonekana upo upande wa iran na kumkana mwafrika mwenzio, je! Wangekutana Iran na senegal au timu yoyote ya weusi halafu iran ikanyimwa hilo goli je ungekuja kuongea👇

Goli la Iran ni halali kabisa????​

Hilo balaa lingekua kubwa au Iran na nanchi yoyote ya wazungu nathan haliingekua tofauti kabisaa
 
Da.... siyo kweli unachosema. Mchezaji anatakiwa awe hajazidi angalau mchezaji mmoja wa timu pinzani (ondoa golikipa). Hajazidi namna gani? Sehemu yoyote ya mwili wake isiwe mbele, unachora mstari uliyonyooka, wakati pasi inatolewa.
Sivyo mkuu. Kama kipa kaenda kucover akaacha beki wake mmoja na goli, basi huyo beki anahesabika kama goal keeper. Ikitokea umetokea hapo katikati yao, obvious utakuwa offside sababu utakuwa umewazidi wote ukabaki na huyo beki aliyechukua nafasi ya keeper kwa wakati huo.

Iliashatokea kwenye game kama mbili za ligi kuu uingereza, sikuwa najua kabla ila zote zilihesabika ni offside mkuu
 
Ungekuwa unaongelea utata wa Ile mistari ningeelewa wewe ni mtu wa mpira,ila kuongelea namba ya watu walobaki nyuma Ili iwe offside au lah,hapo nimekuweka kundi la wachambuzi vitambi wa bongo,hata danadana hamjawahi kupiga, michezo ipo mingi na kwenye mpira wa miguu Ile ni offside!!!
 
Inaonekana hujui sheria za offside. Sheria ni kuwa anayepokea pass (huyu mchezaji wa Iran in this case) siku zote anatakiwe awe na wachezaji atleast wawili, ambao hajawazidi. Hapa yuko mmoja, hivyo ni offside.
Jamaa ana msimamo mkali halafu hayupo sahihi. Angekuwa anatazama games nyingi hii isingekuwa issue maana ni scenario ya kawaida
 
Mchezaji anayeoneshwa hapo kwa mshale ndio wa Mwisho. Chukulia mfano huyo ndio angekuwa kipa wa Misri. Sheria inataka, wakati Mpira unatoka mguuni kwa mpasiaji kwenda kwa mpokeaji, kuwe na wachezaji wawili wa upinzani mbele ya mpokeaji. (Mara nyingi huwa beki mmoja na goalkeeper ) Hapo kwa vile kipa ametoka, ilipaswa kuongezeka mchezaji mwingine wa Misri kuzuia, hiyo ingeua offside.

Kuona mijadala sehemu tofautitofauti hata kama ni ya wachambuzi maarufu hakubatilishi Sheria hiyo ya Mpira, wachambuzi nao ni binadamu, wapo wasiojua Sheria(makanjanja) lakini pia wapo wazuao taharuki kwa maslahi Yao binafsi. Wasikupotoshe ndugu.
 
Ni kusema kwamba hapo mfungaji alibaki yeye na keeper wakati pasi inatoka mguuni mwa mpasiaji. Clear offside.
 
View attachment 3617283
Kwenye duana hapo mchezaji wa timu gani?
Ila we jamaa unanongwa binafsi nahaya mashindano haya Trump namarekani yake mbona umeshaelekezwa VAR haiongopi hasa kwenye mashindano makubwa kama haya ambayo kila mtaalam anafatilia....unaleta ubishani eti media zimepinga off side halafu media yenyewe mwanasport
 
Uyo alieanguka chini na kuugusa Mpira haikuzingatiwa, Mpira ndo ulifuata mkono wake alipodondoka chini tusipotoshe na Hilo: ila Iran kufuzu niaombee Algeria afungwe na Austria au congo wasishinde dhidi Uzbekistan hivyo! Maana hao ndo wamebaki na wnywe wanasiklzia mchongo wa best loser
Katika soka, hakuna kitu kinachoitwa mpira kuufuata mkono. Hizo ni stori tu za vijiweni. Tumeshuhudia wachezaji wajanja wakiwanawisha mpira oppositions kwa makusudi na faulo inawekwa. Ukiushika mpira na ukaonekana umeathiri mpira kuchezeka katika njia zake, hiyo ni faulo, hata kama mpira ndio ulikufuata
 
Mpira kuufuata mkono, ni Mpira kugusa mkono wakati mkono upo katika natural position, yaani mikono Iko mbavuni na kusiwe na jitihada zozote za kuusukuma huo Mpira kwa mkono.
Hapo ni kama unaulizwa Mpira, 'Je, ulitaka niingie uwanjani bila mikono? Nimeingia nayo na IPO katika nafasi yake sawa na masikio na pua' Ni sawa tu na Mpira unavyomgonga mtu tumboni.
 
Kwa hiyo yeye ni kama kipa? 😂😂😂 Kipa akienda kupiga kona uwezekano wa kuoiga kaunta hakuna sababu itakuwa offside au sio?
Umejibiwa, unabishana !

Bongo nyoso mtu akishaamini lake humtoi 😂😂😂😂
 
Mpira kuufuata mkono, ni Mpira kugusa mkono wakati mkono upo katika natural position, yaani mikono Iko mbavuni na kusiwe na jitihada zozote za kuusukuma huo Mpira kwa mkono.
Hapo ni kama unaulizwa Mpira, 'Je, ulitaka niingie uwanjani bila mikono? Nimeingia nayo na IPO katika nafasi yake sawa na masikio na pua' Ni sawa tu na Mpira unavyomgonga mtu tumboni.
Kama umerefer hivyo, ni sawa. Lakini natural position ya mkono ni ile ya kujibana mwilini kuanzia begani ukinyooka hadi katikati goti na kiuno. Mkono usipojibana tu ukatanuka na mpira ukazuiwa, hiyo sio natural position na ni foul
 
Back
Top Bottom