Kwa hali ilivyo hata Lissu akigombea akiwa gerezani anaweza kushinda Urais

Muungano ufe Tanganyika idai uhuru wake
 
Mkuu,nafikiri hili ndilo kosa mojawapo Chadema na wapinzani wengine wamekuwa wanalifanya. Ni kweli tuhuma za kuibiwa kura zimekuwepo lkn kitakwimu bado CCM iko imara zaidi.
☆Kwa mujibu wa takwimu za demographic nature,asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi vijijiji ambako CCM bado imekamata sana.

☆NRNE ipo maeneo ya mijini mijini au palipochangamka. Am sure huko ndanindani Kazuramimba na Nyakintuntu hawajui chochote au wanajua kwa level ya chini sana.

☆CCM ina fanbase kubwa sana. Kwa mujibu wa takwimu mpya ni takribani wanachama 13m. Sasa hapo huoni hata nusu tu wakipiga kura,tayari ushindi unakaribia?
 
JF ni kiboko .Mtu akitaka kupata majibu ya upuuzi anaoufanya aingie JF 🤔
 
CCM iko imara kivipi?

Wangekuwa imara wangekataa reforms?

Fan base ya CCM ni watu wanaoipenda na kuishabikia kimaslahi binafsi.
 
Twende na uhalisia JF Ina wanachama registered approximately kama laki SITA..je hii ni asilimia ngapi kati ya 60m?
60M unaongelea na vichanga vilivyozaliwa leo?Chukua ratio ya idadi ya watu ya kuanzia miaka 18+(umri wa kupiga kura)
 
Huo ndio ukweli wenyewe... maajabu ni pale atakapo tolewa gerezani kwenda kuapishwa na kuwafungulia mahabusi wote wa kisiasa--- siku hiyo nchi italipuka kwa furaha sana na lazima itakuwa ni public holiday ya kipekee... Eee Mwenyezi Mungu, fanikisha hili jambo...Amen
 
Hata ukifikisha Mika 90 bado CCM itaongoza urais
 
Anapewa assist ila hana uwezo. Apa jf kuna uzi wa kura zake umefutwa siuoni.?
 
Itakua ni uhuru kamili wa Tanganyika
 
ramli nyingine za kilofa sana aise,dah 🤣
 
Tume huru ya uchaguzi ndio uchawi wote.
 
CCM ni chama kikubwa ifike kipindi sio lazima mtu kukamilisha mihula yote miwili mbona tuna watu wanakubalika sana CCM kwa wananchi mfano Athony Mtaka
 
Mimi namuonea huruma tu huyu mama. Sijui atanadi sera gani kwenye kampeni. Je ni sera ya kuteka na kuua au sera ya kufungia makanisa? Ajabu zaidi ni kuwa muda haupo. Mimi ningepewa nafasi ya kumshauri ningemshauri kuwa ni bora aamue kuungana na akina Lisu na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya. Ajiongezee miaka 2 ya kuongoza uandikaji wa Katiba mpya kisha asimamie uchaguzi wa haki aondoke kwa heshima. Atakuwa amewapiga bao mahasimu wake ndani ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…