Kwa hali niliyoiona sitashawishika tena kupima UKIMWI

Kwa hali niliyoiona sitashawishika tena kupima UKIMWI

Baada ya condom kupasuka tukiwa tunagegedana nikamwambia tukapime akakubali alionyesha hofu lakn alijitahidi kuificha.

Tukaenda wote tulipopimwa tukatoka nje kusubiri majibu. Baada ya dakika 20 akaitwa na kuchukuliwa damu mara ya pili.

Muda wa kupewa majibu ukafika. Kweli bhana kumbe anaishi na maambukizi ya VVU.

Nikaeleza mbivu na mbichi nikapewa PEP. Nikazimeza kwa mwezi Mzima. Dawa zile ni kali mno, zinalevya mno na kuchosha. Ndoto za maruweruwe ya kutisha.

Nilipomaliza dawa nikaenda CTC pale Amana. Nikapima Nikaambiwa sina maambukizi. Nikakaa mwezi mmoja nikapima tena nikaambiwa sina.

Yule mwanamke huwezi kumdhania kabisa. Tena ni mnene na ana kalio la haja linaloweza kukudanganya. Kumbe ndani ameungua.
unaona sasa kama ungeogopa saa hizi ungekuwa na maisha mengine lakini sasa upo sawa na pia ulijifunza kutokaza hovyo
 
Siku hizi hamfanyi aisee zamani ilikuwa kabla ya kupima unapewa counselling ya maana na kabla ya kupewa majibu unafanyiwa counselling juzi nmeenda hospitali Dr kaniandikia tu kipimo cha HIV kama cha malaria vile simple bila hata kuniuliza kama niko tayari kupima

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa hata mimi nilienda kupima mwezi uliopita yaani unaandkiwa kama vile unapima ugonjwa mafya tu na majibu yanakuja unapewa kama vile taarifa ya mapato na matumizi.

Ila kipindi cha miaka ya 2006/2007 ilikuwa unapewa ushauri wa kutosha na unaulizwa kulingana na maelezo uliyopewa unahisi una asilimia ngapi za kuwa +ve au -ve . Kwa sababu unapewa na elimu jinsi VVU vinayoambukiza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine.

Sasa hivi tena wanakutoboa tu kama kipimo cha malaria ndani dakika tano unapewa jibu so ukikutwa umeambikizwa na haukuwa tayari kupokea taarifa ya hivyo unaweza kuzimika kwa pressure.
 
Hahahaaaa!
Anakuwa kakipata alichokuwa anakitafuta!
Ila mkuu kupima ni bora zaidi ujue.

Kwa sababu unapopima na kujua huwa ndio mwanzo wa kujitunza na ukipima na kuambiwa unao poa ndio mwanzo wa kuanza kupata huduma na kusogeza siku zako za kuishi.
 
u
Siku hizi hamfanyi aisee zamani ilikuwa kabla ya kupima unapewa counselling ya maana na kabla ya kupewa majibu unafanyiwa counselling juzi nmeenda hospitali Dr kaniandikia tu kipimo cha HIV kama cha malaria vile simple bila hata kuniuliza kama niko tayari kupima

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi,hii nimekutana nayo mara kadhaa,madaktari wamekuwa wazembe sana siku hizi.Anakuuliza nikupime na HIV unamwambia pima anakuandikia kipimo anakuacha unasubiria majibu with no councelling,ni hatari sana kwa kweli.
 
Huyo bwana alihitaji kupata ushauri wa wataalamu wa kisaikolojia baada ya kupima.

Kupima ni muhimu sana coz 'wale jamaa' wakigundulika mapema una nafasi ya kuwa control na ukaishi salama kwa miaka mingi tu.

Huyo aliyekwambia kuwa kutokuwa na vvu basi ndio tiketi ya kuendelea kuishi duniani kadri utakavyotamani ni nani?...bado kuna njia zaidi ya milioni za kuiaga dunia hata kama huna hao VVU.

Njia pekee ya kukwepa mauti ni kutokuwepo kabisa....ukiutaka uhai basi kubali kuwa utakufa tu siku moja, hata kwa kuchomwa bisibisi na teja linalokupora simu yako.

Kuna magonjwa yanatesa mpaka ungetamani tu bora uishi na hao vvu...muhimu upime ili uwa control, la sivyo wao wakianza kuku control ndio basi tena.
 
Hayo yashawah kunitokea.
Yan saiv naishi kama boya mtaani madada wananipapalikia ila hata hiyo ham sina

Pep Zinakera yan mdomo unakua haupati ladha kizunguzungu ndo usiseme

Halafu cha kushangaza docta alinambia hizo pep hazina tofauti na arv sasa nikawa nawaza mimi nimetumia mwezi tu nipo hoi vipi kwa hao wanaotumia maisha yao yote? Ukipata jibu hapo lazima jogoo alale hata kama mbele yako kapita chura

Asee mkuu sirudii tena
 
Naunga mkono hoja sipimi ng'o cha kwanza najitahidi kumcha Mungu Wangu na kumuomba aniepushe na balaa hili...waliopata tatizo sio kwamba ni waovu sanaa

carnte himself
 
Kwa maelezo yako nimegundua hili tatizo bado lipo kwa speed kubwa ndo maana sasa hivi hata ukienda unakajipu dokta atakuandikia tu upime HIV.

-Ndumilakuwili-
WAKIAMUA WANAKUPIMA KWA ILE DAMU YA MALARIA MARA NYINGINE TUNAPIMWA BILA KUELEWA WANAJUA ALAMA KWENYE MACARD YALE HASA WAMAMA WAJAWAZITO
 
Huyo bwana alihitaji kupata ushauri wa wataalamu wa kisaikolojia baada ya kupima.

Kupima ni muhimu sana coz 'wale jamaa' wakigundulika mapema una nafasi ya kuwa control na ukaishi salama kwa miaka mingi tu.

Huyo aliyekwambia kuwa kutokuwa na vvu basi ndio tiketi ya kuendelea kuishi duniani kadri utakavyotamani ni nani?...bado kuna njia zaidi ya milioni za kuiaga dunia hata kama huna hao VVU.

Njia pekee ya kukwepa mauti ni kutokuwepo kabisa....ukiutaka uhai basi kubali kuwa utakufa tu siku moja, hata kwa kuchomwa bisibisi na teja linalokupora simu yako.

Kuna magonjwa yanatesa mpaka ungetamani tu bora uishi na hao vvu...muhumu upime ili uwa control, la sivyo wao wakianza kuku control ndio basi tena.
We jamaa umeongea point tupu. Big up
 
Back
Top Bottom