Kwa hali ya Corona na kimbunga Jobo, nimeamini Tanzania inalindwa na Mungu

Kwa hali ya Corona na kimbunga Jobo, nimeamini Tanzania inalindwa na Mungu

Eti Mungu anatulinda sana wakati Biblia na Quran zote zinakiri mvua,upepo, n.k vinatoka kwa Mungu!! So ina maana Mungu anatulinda dhidi ya kitu alichoumba mwenyewe? So anafaham kuwa ni kibaya?
...ndugu,nimekubali kutokukubaliana na wewe.

Mchana mwema.
 
Hivi mimi ni nani hadi nisishuhudie maajabu ya Mungu kwa Nchi yetu!

Kwa sisi tunaosafiri hasa Nchi za wenzetu kwa namna wanavyohangaishwa na Corona na ukiringanisha na namna tunavyoishi hapa kwetu Tanzania hakika mapenzi ya Mungu kwa Nchi yetu ni mema sana.

Hilo la kimbuga Jobo pia kutokuleta athali zozote kama ilivyotarajiwa hakika mkono wa Mungu ni wa kipekee kwa Taifa letu.

Kama Watanzania na pasipo kujali tofauti zetu za kiimani na kisiasa yatupasa sasa tumshukuru mwenyezi Mungu kwa mapenzi mema kwa Nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania!
Mibalaa inaondoka na mwendazake.
 
Halafu either kuna tatizo katika vyombo vya habari au katika system za kutabiri(forecasting) majanga duniani.Nakumbuka CNN iliripoti kuwa Tanzania itapatwa na kimbunga ambacho haijawahi kukipata tangia miaka 80 iliyopita.Sasa najiuliza,ina maana vituo vya kufanya forecasting ya hali ya hewa vilishindwa kujua kuwa hicho kimbunga hakitafika Tanzania?

Ni sahihi kuwa wanasayansi wa kufanya utabiri wa hali ya hewa hawana uwezo wa kujua kwamba kutokana na sababu fulani fulani kimbunga fulani hakiwezi kufika sehemu fulani?Au CNN ndiyo wana tatizo katika kuripoti taarifa zao?
Wewe ni pinga pinga mtu wa kuangalia makalio ya akinamama. Angalia mwenyewe
 
Attachments

  • Chura.mp4
    15.3 MB
Stuka wewe, hiyo stori inaweza kuwa ilikuzwa kutengeneza njia ya kupitisha mzigo ilipobumba ndio zinakuja taarifa kimeyeyuka kwa nguvu za maombi.chezea tani mbili nini ?
Mzigo wa tani moja ule
 
Kwahiyo nchi zingine ambazo wametupita sana kimaendeleo wao wanalindwa na shetani? Akili zenu hazina akili
 
Pale yanapodhihirika matendo makuu na ya maajabu, sifa na heshima na hata utukufu unapaswa kurudi kwa Mungu na Muumba wetu. Wacha Mungu huomba kila siku kwa bidii naye Mungu wao huwasikia na kujibu maombi yao.

Tatizo lipo kwa wale wasio amini uwepo wa Mungu na ukuu wa matendo na kazi zake. Hiyo kwa hakika ni kwa hasara yao wao wenyewe. Lipo jina moja lipitalo majina yote mbinguni na dunia ambalo hakuna kitu ambacho kinashindikana endapo watu wa Mungu wataomba kwa dhati kupitia kwalo.
 
Wewe ni pinga pinga mtu wa kuangalia makalio ya akinamama. Angalia mwenyewe
Kwa hiyo wewe nikikupa huyu utakataa na kusema kuwa hutaki?
17474316520.jpg
 
Halafu either kuna tatizo katika vyombo vya habari au katika system za kutabiri(forecasting) majanga duniani.Nakumbuka CNN iliripoti kuwa Tanzania itapatwa na kimbunga ambacho haijawahi kukipata tangia miaka 80 iliyopita.Sasa najiuliza,ina maana vituo vya kufanya forecasting ya hali ya hewa vilishindwa kujua kuwa hicho kimbunga hakitafika Tanzania?

Ni sahihi kuwa wanasayansi wa kufanya utabiri wa hali ya hewa hawana uwezo wa kujua kwamba kutokana na sababu fulani fulani kimbunga fulani hakiwezi kufika sehemu fulani?Au CNN ndiyo wana tatizo katika kuripoti taarifa zao?
Hapana utabiri au hata ukifuatilia mwenyewe kuna site inaonesha kimbunga live, sasa wanatoa hali halisi pale kinapokuwa live kuwa speed ni hii na kinaelekea wapi na hapo utakuta kiko mbali sana kwa hiyo inatembea 24 Hrs lakini wakiona speed inapungua wana kishusha grade na wakati mwingine unadhani kita land Mtwara halafu kinabadili labda kinaelekea Tanga au kinaweza kuchukuwa njia nyingine ndio maana kuna utabiri wa masaa. Mnajiandaa na ile hali inavyokuwa wakati ule huwezi kusema sasa hivi speed 200 lakini msiwe na wasiwasi speed itashuka hapana kinaweza kuongeza speed au hapana ni mambo mengi yanatokea hata hao watabiri wa Tanzania wanatumia site hizo hizo za nje maana ndio wana satelite zao angani sisi hatuna chochote, satelite za nje ndio zinanasa hii hali vinginevyo tungekuwa tunashtukizwa tu na vimbunga.
 
Halafu ukishaanza kuona hii hali ya vimbunga vinaanza haya ndio mabadiliko ya hali ya hewa ujuwe kuna siku kitakuja yalianza huko sijui Msumbiji na haya mambo hayakuwa issue kwetu ila slowly tunaanza kuyaona na Mungu atuepushe tusiombe kabisa maana na hizi nyumba zetu za bati misumari yenyewe fan tu inatingisha halafu kije kitu speed 200 tutalala paa wazi.
 
Hapana utabiri au hata ukifuatilia mwenyewe kuna site inaonesha kimbunga live, sasa wanatoa hali halisi pale kinapokuwa live kuwa speed ni hii na kinaelekea wapi na hapo utakuta kiko mbali sana kwa hiyo inatembea 24 Hrs lakini wakiona speed inapungua wana kishusha grade na wakati mwingine unadhani kita land Mtwara halafu kinabadili labda kinaelekea Tanga au kinaweza kuchukuwa njia nyingine ndio maana kuna utabiri wa masaa. Mnajiandaa na ile hali inavyokuwa wakati ule huwezi kusema sasa hivi speed 200 lakini msiwe na wasiwasi speed itashuka hapana kinaweza kuongeza speed au hapana ni mambo mengi yanatokea hata hao watabiri wa Tanzania wanatumia site hizo hizo za nje maana ndio wana satelite zao angani sisi hatuna chochote, satelite za nje ndio zinanasa hii hali vinginevyo tungekuwa tunashtukizwa tu na vimbunga.
Kwa hiyo kwa mfano kama kuna kimbunga kimetokea baharini kilomita 5000 kutoka Dar es salaam kikiwa na speed ya 200KM/H wanasayansi hawana uwezo wa kujua kwa wakati huo hatima ya hicho kimbunga?Yaani hawana mbinu ya kujua kuwa kwa wakati huo kuwa kitafika Dar au la na kama kitafika je kitafika na speed gani na kitasababisha athari gani?
 
Nimeiona mahali:

Ndugu zangu!

Kikawaida cyclones huwa hazikimbilii towards the equator. Zikifanya hivyo huwa zinakosa nguvu na kutawanyika. Kwa maana hiyo hatari kubwa kwa hii Cyclone ya Jobo ni Lindi na Mtwara (9 degrees S) na sio Dar (6 degrees S).

Ndiyo maana cyclones nyingi zinazoanzia bahari ya Hindi huwa zina gain southwards na kuishia Madagascar au Mozambique. Hii ya ku gain northwards towards the equator kwa kweli ni ajabu

Kikawaida ni vigumu kutokea cyclone/hurricane/typhoon 5 - 7 degrees South or North of the Equator sababu kuna Coriolis Effect ndogo. Dar ni 6 degrees South of Equator kwa hiyo ideally cyclone itadhoofishwa na kutawanyika inapokaribia Dar. Ndiyo maana Lindi na Mtwara (9 degrees S) makes more sense.

Huku kwetu kwenye Southern hemisphere cyclones zote huwa zinaenda clockwise, hata vimbunga n.k......kwenye Northern hemisphere huwa ni anti-clockwise. Sasa tunapo approach Equator huwa hii phenomenon inapungua na tunapoenda mbali na equator inaongezeka....na kwenye equator yenyewe hakuna hii effect......cyclones huwa hazikimbilii equator. Kwa mfano unaweza kufanya practical kidogo.....tukijaza sink maji tukiyafungulia yatazunguka clockwise sababu tupo Southern hemisphere ila kwa wenzetu waliopo northern hemisphere (mfano Uingereza) itakua anti-clockwise....na waliopo equator mfano Kenya au Uganda yataanguka tu straight down! Ndiyo maana inavyosemwa kitaenda northwards hapo ni ajabu sana.

Kinadharia....the worst that can happen kwa Dar ni mvua tu tena kwa kiasi chake. Kitakutana na mengi ya kukiresolve njiani mpaka kifike Dar. Imesahaulika tu kukumbushia oceanic currents,......maana kikiwa njiani kwa upande uliosemwa kutokea kitakutana na Mozambican current hivyo kitapunguzwa nguvu sana.

Vurugu inaweza kuwa kusini hasa Mafia, Rufiji na kwenda Lindi na Mtwara. Dar si rahisi....kikija northwards kuanzia (Dar) na kuendelea maeneo mengine northwards kweli kitakua kimefanya Job kama wanavyokiita Jobo 😅
Ahsante kwa maelezo yako . Ushahidi wa picha huu->
1619351749422.png
 
Kwani nchi gani ya Afrika(weusi) wamekufa wengi Kama Wazungu
 
Kwa hiyo kwa mfano kama kuna kimbunga kimetokea baharini kilomita 5000 kutoka Dar es salaam kikiwa na speed ya 200KM/H wanasayansi hawana uwezo wa kujua kwa wakati huo hatima ya hicho kimbunga?Yaani hawana mbinu ya kujua kuwa kwa wakati huo kuwa kitafika Dar au la na kama kitafika je kitafika na speed gani na kitasababisha athari gani?
Ningeweza kukutumia site ya hivi vimbunga satelite, wana level kama 5 na hii inakuwa kwa speed level 1 mpaka km 153, 2 mpaka 177 muhimu ikifika sasa 5 huko 252 kwenda juu huko sasa majanga. Satelite inachukuwa live speed na muelekeo speed ikipungua wanashusha category na mara nyingi kikifika ardhini speed inakuwa inapungua lakini inategemea na huko kimeanza na speed gani. wao wanaweza kukisia lakini kwa tahadhari wanachukuwa tahadhari zote ila wakiona kila baada ya masaa kina drop speed kiasi gani hapo wanatabiri mpaka kifike speed itakuwa hii wana kisia ila sababu sisi Tanzania hatujawahi kupata issue hizi sana hata kikija na speed 90 KMH kwa sisi ni kubwa sababu sidhani kama tumewahi kupata ila kwa USA mfano hiyo sio lolote maana huwa wanapata mpaka category 5 na inakuwa majanga.
 
....bado mwenyezi Mungu ni wa ajabu na anaendelea kutenda wema usioelezeka kwa Nchi yetu.

Asubuhi ya leo,rafiki yangu mmoja bwana Smith mwenyezi wa Chigago huko USA amenipigia simu huku akionyesha hali ya kutokuamini kipi kimeleteleza kimbuga Jobo kiukwepe Ukanda wetu wa Pwani jambo ambalo hata huko ng'ambo hawaamini!
Hatupo katika ukanda wa vimbunga.
Huko carrebean Mungu hayupo?
 
Back
Top Bottom