PostGE2025 Kwa hapa tulipofika; Ya Oktoba 29 tungeyaacha, tuendelee na mambo mengine

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sasa kwanini serikali haikufanya hizo reforms chadema waingie kwenye uchaguzi? hapo ndo utaona mtuhumiwa number moja ni CCM wamezoea Siasa za ulaghai
Msimamo wa serikali ni kuwa reforms zilishafanyika. Hii ndio ilikuwa kauli rasmi ya CCM na Serikali.
Hata hivyo CCM kwenye ilani yake ilisema ikichaguliwa ndio itaanzisha mchakato wa katiba mpya.
Pengine tusubiri utekelezaji wake.
 
Damu ya Kaini inalia udongoni.

Haitanyamaza hadi ilipwe
 
Msimamo wa serikali ni kuwa reforms zilishafanyika. Hii ndio ilikuwa kauli rasmi ya CCM na Serikali.
Hata hivyo CCM kwenye ilani yake ilisema ikichaguliwa ndio itaanzisha mchakato wa katiba mpya.
Pengine tusubiri utekelezaji wake.
CCM ilichaguliwa na nani? Aya mambo ndo yanaongeza chuki kwa watanzania walio wengi
 
Hadi sasa silaha kuu ya ccm ni kutishia watu kuwatoa uhai pale wananchi wanapotoka kuongea maoni yao na hisia zao.. hili linafanyiwa kazi.

Kingine tukumbuke mauaji ya kutisha na utekaji kabla ya MO29, tukumbuke Watanzania wenzetu waliopoteza maisha kikatili, je ? nani ni mvunja amani? walioandamana ama watekaji? nani wafanya vurugu?

Lakini yana mwisho..
 
Haya yote uliyoandika, tulitegemea Tume ianze angalau kwa kuyabainisha na hatua za kuanza kuyatibu kupendekezwa.

Nini kimetokea? Tume ndio imesisitiza watu walilipwa, walifadhiliwa kufanya machafuko na mambo kama hayo.

Kiufupi kama alivyosema Dr, CCM/Serekali haina nia ya dhati kukubali na kutibu kilichotokea Oct.29.

Sasa kuliko kupoteza rasilimali kuunda sijui tume na hakuna ujasiri wa kuambiana ukweli ni afadhali tuache Ili Muda uje Kulitbu tatizo.

Wakati huo tutakuwa tushachelewa.
 
Kwahiyo ilitakiwa cdm waendelee kushiriki kama mazombie huku chaguzi zikichezewa? Tume imeagizwa kibwegwe sana. Sababu ya maandamano yale yalayopelekea na vurugu ni kuchezea uchaguzi, lakini tume imetakiwa isihoji hilo, halafu mnataka watu waone ni tume ya kutazama ukweli?

Cha ajabu na ww kwakuwa unaujua ukweli na unajua watu hawawezi kukubali huu usanii, unataka tuachane nalo tusonge mbele bila uwajibikaji! Tume ilitakiwa iseme ni wapi kura 31m zimetokea, na sio cdm kushiriki uchaguzi kama wajinga wakati hakuna uchaguzi bali maigizo.
 
Nakuunga mkono 100%

Kiufupi tumegawanyika zaidi kuliko kabla ya Oct.29. Mwenye msimano wa kuunga mkono waandamanaji msimamo ndio umekuwa mkali zaidi baada ya ripoti ya tume. Na upande wa walioua nao wamezidi kuona waliouawa ni magaidi/wahaini.

Sasa tulitegemea Tume ingekuja kuwa kama Daraja Ili misimamo ipungue watu wakae chini, ila tume ndio imechochea mpasuko.

Hakuna wa kushusha mapanga chini kwa sasa baina ya pande zote. Hakuna anayekubali kuwajibika.Tuache Tu muda utakapoamua wenyewe.
 
Ww ndio unaamini mambo ya kiama, sisi tunajua uwajibikaji. Yaani tusubiri siku ya kiama tusiyoijua, tuwaache wauaji tunaowaona kwa macho? Hakuna kuwajibishana maana viongozi ndio wahusika wa tatizo la uchaguzi, na mauaji yale.
 
Msimamo wa serikali ni kuwa reforms zilishafanyika. Hii ndio ilikuwa kauli rasmi ya CCM na Serikali.
Hata hivyo CCM kwenye ilani yake ilisema ikichaguliwa ndio itaanzisha mchakato wa katiba mpya.
Pengine tusubiri utekelezaji wake.
Reforms gani zilifanyika?
Orodhesha Reform hata moja tu iliyofanyika.
 
Ww mwananchi wa kawaida amini ukweli.
 
unadhani upo utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi wetu wa kuchukua hatua dhidi ya waliotenda vitendo hivi?
Utashi wa kuchukua hatua HAKUNA kwa sababu wanaopaswa kuchukua hatua ndo wahusika wa mauaji.
Kinachoendelea ni kumaliza pesa za walipa kodi kwa kuunda tume juu ya tume ambazo hazitatuletea uwajibikaji wowote.
Upo sahihi hapa
Kwatulipofikia tumwachie Mwenyezi Mungu aje atoe hukumu yake siku ya kiama. Sisi acha tuendelee na 4R
Kwa mujibu wa Baba wa Taifa, Mwl Nyerere, mtu akianza kula nyama ya mtu hali mara moja, ataendelea kula tena na tena. Ukitaka waendelee zamu yako itafika tu, hata Polepole hakujua kama angefikiwa
 
Iamini common sense yako!
 
Umeweka bayana ukweli mchungu!
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
 
Watu HAWAJAZIKA.

Watu hawajui ndugu zao wako wapi.

Kina Kitima.wana majeraha kichwani.

Ali kibao watoto wake hawajui kilichomkuta baba yao.

Watu wanatembea na utumbo nje.

Maisha hayawezi kuendelea kama kawaida kwa huyo bibi katili wa Unguja.
 

Mass slaughter of non-combatants is genocidal and unbearable!

Simple! Kwa kuwa serikali na madaraka hutoka kwa wananchi. Na kwa kuwa wananchi wameguswa vifo na kutoneshwa na ripoti ya ovyo kutoka kwa wazee wa ovyo... Na kwa kuwa sasa wananchi wanazidi kuhamasika ...
Ni suala la muda tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…