PostGE2025 Kwa hapa tulipofika; Ya Oktoba 29 tungeyaacha, tuendelee na mambo mengine

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Comrade hatuzungumzii takwimu za uchaguzi hapa, tunazungumzia chanzo cha yaliyotokea Oktoba 29.
Takwimu za uchagumzi mm na ww hatuna namna yoyote yakuzithibitisha, tumwachie Mwenyekiti wa tume ndiye anayejua alikozitoa.
Chanzo cha maandamano ya 29 October ni wizi katika uchaguzi. Ni kweli unaweza ushindwe kudhibitisha, lakini ww sio mjinga wa kuamini siku wapiga kura siku ile walifika 32+m, labda kama umeamua kujivika ujinga wa lazima.
 


Kwani kulikuwa na uchaguzi?
 
Wewe nae ni mpumbavu, Serikali inasamee au yenyewe ndiyo iwajibike? Yaani Bunduki iliyotumika kuuwa watu then walioua watu ndiyo inatoa misamahaa.
Punguza mizaa na chukizo kwa watu waliokaa kimya ukidhani ni wajinga.
Punguza mizaa ndugu, yaani Serikali inasamee watu ila yenyewe haiwajibiki then unajiita Daktari.

Kinyaa tupu, ndiyo nyie mnajiita wasomi.
 
Matusi yako hayatatutoa hapa tulipo. Tunaomba utupe njia ya kuwawajibisha watuhumiwa na mkakati wake wa utekelezaji.
Mm na wenzangu wenye mtazamo kama wangu tumeng'amua hakuna political will ya kuwawajibisha watuhumiwa, tunaona bora mjadala ufungwe tufanye mambo mengine.
Hata hivyo tungependa kujua kutoka kwa nyie wenzetu waweza mambo yote mna suluhisho gani?
 
Unajiita Dr hakafu kichwa chako ni FUVU tu, badala ya kutumia LOGIC na AKILI, unatafuta WATU WA KUWAAMINI??

Nenda ka Mwamposa, basi.
 
Suluhisho lao ni Matusi, kashfa na uzushi mitandaoni
 
Kama uwezo wako wa kufikiri na kuchakata mambo yamefikia hapo ni bora ukae kimya siyo kusumbua watu na maandishi yaliyojaa upotosha kwa lengo la kusafisha upande fulani huku ukikandamiza upande uliokandamizwa siku zote.

Wananchi wameshachutama vya kutosha, kama Serikali I inadhani wao hawaruhusiwi kuchutama basi wananchi tunasema ...
1. Penye fujo na wewe endelea kutia fujo wenda Amani ikapatikana
2. Aliye juu na wewe mfuate juu
 
Hayo mambo ya kusamehe samehe sometime ni unyonge. Aisee hivi uzike nguo harafu ukiangalia sababu ya ndugu yako kuuliwa huioni unaanzaje kusamehe..hao wauaji wanajilia mahela na kucheka na familia zao sisi tusamehe...big nooo
 
Mimi naona ambayo aliyasema mama kwa Tume wakati ameichagua ndo hayohayo yamerudi kama yalivyo. Swala la vijana kununuliwa wamelirudisha kama lilivyo. Yaan wamepita mlemle sasa sijui walienda kufanya kazi gani.
 
Masuala ya haki na kuwajibishana tumwachie Mungu, sisi yaneshatushinda.
Hii ndiyo sababu watu hawataki Sana kujihusisha na dini.
Kufanya hivi ni kukubali unyonge na umasikini hadi kifo chako.
Wewe ungefiwa na mtoto wako au nduguyo wa kuzaliwa tumbo moja ungesamehe na kusahau?
Una waona wafiwa au waliopata ulemavu kwa hizi vurugu wajinga na maisha yao hayana thamani kuliko ninyi kutawala?
 
Wewe unaona yalikuwa ni maandamano au fujo ?
 
Una akili ya kipuuzi sana wewe mtu; kama walivyo wengine wote wanaotegemea manufaa toka kwa waovu hawa wanaolitingisha taifa hili.

Unatoa wapi ujasiri wa kuwaambia waTanzania wakubali kuendelea kuwa wanyanyaswaji ndani ya nchi yao wenyewe!.

Ni maslahi yapi ya taifa yatakayolindwa kwa kuendelea kuwa na wahalifu/majambazi wakiendelea kunajisi taifa hili?

Hiyo serikali imewasamehe vipi iliowaua; itawarudisha toka kwenye makaburi ya pamoja?

Hakuna mtu wala kundi lolote linalostahili lawama isipokuwa Samia Suluhu Hassan na Genge lake walioamua kung'ang'ania kukaa madarakani kwa nguvu. Hilo ndilo lililosababisha maafa yote haya, na litaendelea kusababisha maafa wakati wote kundi hili likiwa madarakani.
 
Limekushinda wewe; halijawashinda waTanzania.

Haya unayotaka wewe ni kutafuta tu njia ya kuwanusuru wahalifu; upumbavu huo waTanzania hawautaki.
 
Wewe ni miongoni mwa member wajinga kabisa hapa JF. Halafu unajipachika title ya 'Dr'. Hujui ni kwa nini kila kilichotokea 29/10 kinatakiwa kijulikane na hatua zichukuliwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…