Kwa hasara ambayo huyu mtoto ameniingizia: Nashauri Sheria itungwe iwe ni shuruti watoto kusaidia Wazazi uzeeni

Kwa hasara ambayo huyu mtoto ameniingizia: Nashauri Sheria itungwe iwe ni shuruti watoto kusaidia Wazazi uzeeni

black sniper,
sawa mkuu nimechungulia kidogo nimepata mwanga ndarudi kusoma kwa kina.
Fimbo huondoa upumbavu, sasa nasita kukatia stick maana hakajajitambua vzr, ila mara moja moja anakula stiki moja.

Ila ukiacha fujo zake, akiwa nje ya maeneo ya home, yuko cool sana, anakuwa anaobserve tu, saana labda aone Baiskeli au Mpira ndio ataulilia kama wake

Watoto wa hivyo huwa wana kitu special pia

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna mahali mnafeli wewe na mke wako, usisahau kuwa kukemea na kuwafundisha watoto ni jukumu letu. Muadhibu mtoto kulingana na umri wake, hata kama ana miaka miwili, mpe adhabu inayoendana na umri wake.

Ashike simu kwa ruhusa yako, laptop kwa ruhusa na vitu vingine vya thamani.
 
Wakuu nimemsomea mama yake comments zenu zote, nyingine akicheka kadogo nako kanacheka sana hadi machozi.

Hasa jamaa aliyosema eti turudi kisemvule Kwa Babu hahaha.
 
Mda si mrefu ataanza kuingia jikoni kupika na kupakua ila mara nyingi tabia za utundu hurithiwa kwa wazazi embu waulize wazee wako ulikuwaje wewe wakati mtoto
 
Mda si mrefu ataanza kuingia jikoni kupika na kupakua ila mara nyingi tabia za utundu hurithiwa kwa wazazi embu waulize wazee wako ulikuwaje wewe wakati mtoto
Jikoni huwa anamuiga mama yake kupika chapati. Anachukua matope nje anaweka kwenye kochi na kopo anaanza kuzungusha. Ukimktaza anasema "Baba mimi pika papati".
 
Back
Top Bottom