Kwa haya yanayotendeka ya mauaji ya watanganyika kwa kuwateka, sababu ya katiba ya UFALME, aliyoiacha Nyerere, siyo baba wa Taifa na si mtakatifu

Kwa haya yanayotendeka ya mauaji ya watanganyika kwa kuwateka, sababu ya katiba ya UFALME, aliyoiacha Nyerere, siyo baba wa Taifa na si mtakatifu

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Nyerere alijua kabisa na alisema hadharani kuwa katiba hii ni mbovu, akiingia RAIS mpumbavu anaweza kuwa dikteita wa kufa mtu! Na bado akaiacha hivyo hivyo na sasa inazalisha madikiteita!

Rais-Mfalme
quotes
Tangu angalau tuwe Jamhuri mwaka 1962, Rais wa nchi yetu amekuwa na mamlaka makubwa sana kikatiba, kisheria na kisiasa.

Kwenye hili, Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusema, mwaka 1967 na akarudia tena mwaka 1978, kwamba alikuwa na mamlaka, kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu za wakati huo, ya kuwa dikteta.

.......... Katiba hii ya mwaka 1977 pia ina tatizo kubwa ........ si jingine bali ni lile linalohusika na kumpa Rais wa nchi mamlaka ya kifalme.
. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema kuwa angetaka, angeweza kuwa dikteta kwa Katiba hii.
 
na akastaafu Kwa kusoma alama za nyakati kwa kile walicho mfanyia mwenzake caucescu wa Romania- Kwa maneno ya prof. Kabudi akinukuu hotuba ya mwal. Nyerere huko Berlin alipoenda kumzika Will Brand…
 
Nyerere alijua kabisa na alisema hadharani kuwa katiba hii ni mbovu, akiingia rahisi mpumbavu anaweza kuwa dikteita wa kufa mtu! Na bado akaiacha hivyo hivyo na sasa inazalisha madikiteita!

Rais-Mfalme
quotes
Tangu angalau tuwe Jamhuri mwaka 1962, Rais wa nchi yetu amekuwa na mamlaka makubwa sana kikatiba, kisheria na kisiasa.

Kwenye hili, Mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kusema, mwaka 1967 na akarudia tena mwaka 1978, kwamba alikuwa na mamlaka, kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu za wakati huo, ya kuwa dikteta.

.......... Katiba hii ya mwaka 1977 pia ina tatizo kubwa ........ si jingine bali ni lile linalohusika na kumpa Rais wa nchi mamlaka ya kifalme.
. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema kuwa angetaka, angeweza kuwa dikteta kwa Katiba hii.
Ukweli Mtupu!
Ni ukweli mchungu sana.

Endapo kama Watanzania walio wengi zaidi wamekuwa na akili timamu sawa sawa kabisa, basi kwa Sasa tungeelekeza nguvu zetu zote kabisa na uwezo wetu wote katika suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya tunayoitaka.
Masuala haya ya Raia kutekwa, kuuliwa na kupotezwa ingekuwa ndio kitu au kigezo Cha kuweza kutuunganisha wote pamoja bila ya kujali tofauti zetu tulizonazo.
 
Ingekuwa ni nchi ya kidhalimu isingewezekana kwa mh.Mbowe kuwa na "PC" na ya kuyasema aliyoyasema......

Ni baba wa taifa hayati JKN aliyetuambia kuwa :

1)Binamu wote ni sawa,
2)Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

#Tanzania daima dumu[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nani kawakataza msiibadilishe mpaka muanze kumshambulia Nyerere aliyestaafu 1985. CHADEMA wakisema katiba mpya mnawatukana, huku Tena mnamtukana Nyerere. Acheni unafiki. Nyerere ataendelea kuwa Baba wa Taifa.
 
1)Binamu wote ni sawa,
2)Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
ACHA SHALLOW THINKING, MTU AMBAYE YUKO SERIOUS, ANAWEKA NA MODALITIES ZA KUTEKELEZA HAYO!
 
Back
Top Bottom