Uchaguzi 2020 Kwa hii hotuba ya Tundu Lissu Segerea, amepotosha

Uchaguzi 2020 Kwa hii hotuba ya Tundu Lissu Segerea, amepotosha

Nimesikiliza hotuba ya Lissu leo Segerea, naona lissu ana improve safi sana, tatizo bado iko palepale japo limepungua kidogo katumia muda mwingi kumshambulia jpm kulipo kuelezea yeye na serikali yake watafanya nini, machache aliyo yaelezea nayo ni kama ifuatavyo.

1. Ujenzi wa barabara ya Salender Bridge; anashangaa hizo pesa nyingi hivyo zinatumika kwa ajili ya watu wachache, kwanza sio kweli kuwa salender bridge hutumiwa na matajiri na vip only, hiki ni kiungo cha kutokea mwenge mbezi ununio mbweni hadi bagamoyo, kusema ni pesa nyingi ni mawazo ya kimasikini tu

Sweden wanajenga barabara ya US$47B barabara ya chini ya maji leo sie kamchepuko tu mtu anaona aghali eti fedha zingetumika kuchimba mitaro vingunguti, naona huyu hakuwepo nchini muda mrefu sasa hivi vingunguti ni lami tupu sivyo alivyo acha.

2. Kuhusu country credit rating; Hivi ni vipimo vya unyonyaji vinavyotumiwa na wazungu kupima urahisi wa kunyonya, hatuwezi kujisifu eti sisi ni watu rahisi kunyonywa rasilimali zetu hapana hata yeye Lissu anajua ngosha hayuko hivyo, hizo FDI sio hela za shangazi zetu hawaji kuwekeza eti sisi ni masikini wanataka watuinue tuendelee kama wao hapana.

Sasa hivi chini ya JPM tunakaa tunazungumza biashara kama hailipi tunaachana nayo, kwa taarifa yako billionea tajiri wa kwanza duniani Jeff Bezos kanunua hisa Barrick za usd 686m na sehemu ya hizo pesa zitawekezwa Tanzania kupitia ubia wetu wa Twiga hayo aliyotumiwa kwenye whasap aka google apate ukweli

3. Kelele za uwanja wa chato; hivi jamani kuna tatizo gani kujenga ka uwanja ka kutua home, kwa taarifa yake hivi viwanja kanda ya ziwa viko vingi kipo Mugumu Serengeti Musoma Mwadui Ibadakuli Nyashimo mission GGM Bulyanhulu Buzwagi Tulawaka Rwamgasa, hiyo runway isimtishe Lissu, nimkumbushe uwanja wa kwanza kujengwa africa mashariki ulikuwa wa Williamson Diamond Mwadui na ndege ya kwanza kutua ilimleta mwana mfalme wa uingereza haya ni mambo ya kawaida sana yasimpe presha.

Na kwanini ujengwe chato? chato ni tambarare ukilinganisha na Geita Bukombe na Katoro ni Giographia tu ndiyo inaruhusu, isitoshe hiyo pesa angeweza kuitumia kuzurura ulaya kama kwenda WEF davos sullivan UN EU AU au hata kwenda kunywa chai na trump ka serve hela na sehemu ya hiyo hela kajijengea kakiwanja shida iko wapi? Kuna waziri mkuu aliwahi kusafiri na msafara wa watu 70 kwenda kwenye graduation ya mwanae marekani na huyuhuyu Lissu akiwa mbunge hakuhoji.

4. Kuhusu bei ya ndege huyu bwana anamatatizo gani? alishaenda atcl akauliza bei ya ndege akakosa jibu? alishaenda Boeng kuuliza bei ya ndege akanyimwa? anauliza bei ya ndege mbona haulizi bei ya nguzo za umeme? mbona haulizi bei ya Youtong za Shabiby? mbona haulizi bei ya mabehewa ya SGR? atcl ina management yake ina muundo na taratibu za uendeshaji tuiache ifanyekazi zake. kwahiyo anataka wabunge waanze kwenda boeng airbus beachcraft jumbojet kukusanya quotation?

5. Uhuru wa kuamua, kwahili bora angeanza kutuambia ruzuku ya chadema ya miaka mitano iko wapi, atuambie zile 500m kila mwezi wanazopokwa wabunge wa chadema ziko wapi? Kila mbunge wazamani analia hana hela za kampeni na juzi wamelipwa 200m kilamtu wamepeleka wapi? kama ni unyanganyi basi basi upo cdm.

6. Hili la NHIF mfumo anaotaka kuleta sio mgeni kule marekani alitaka kuuanzisha Obama ukapewa jina la "Obama care" kama wamarekani uliwashinda na Lissu ataufanikisha basi atakuwa mtu mwnye akili sana. na kwa taarifa yake Bima ya afya sio ya bure ni huduma unalipia kama unavyokata bima ya gari kuwa litakapopata ajali liweze kutengenezwa, unaposema kila mtu awe na bima maana yake kila mtu alipie matibabu kwa lazima uwe mzima mgonjwa lipa tu, ni sawa na mtu kumwambia kila mtu alipe bima ya gari uwe huna unalo lipa tu utajiju, hapana, wenye uwezo wacha walipe bima na ambao hawana uwezo wapate huduma bure.

7. Deni la Taifa, Lissu anasema tunajenga miradi kwa pesa zetu deni linatoka wapi? kwanza hawa contractors wanalipwa pesa ya kigeni sie tunakusanya pesa za kitanzania tunahitaji dola za kuwalipa hawa wakandarasi, pesa iko bank lakini yakitanzania na hawa Arab Contractors Yepi wanataka dola, lazima tukope na kukopa sio dhambi na zipo kanuni za kukopa. Ukioa kwa msomali anakuuliza kuna mtu anakudai ukisema hapana anakufukuza maana yake kuna siku mwanae atalala njaa kisa umeogopa kukopa.
Umejibu hoja bila weledi:

1) Unaulinganisha uwanja wa ndege wa Chato na airstrips! Hopless kabisa.

2) Ile barabara ya juu ya maji inayotembea sambamba na barabara ya nchi kavu, ni ngumu sana kuitetea. Unaweza kujenga barabara juu au chini ya maji lakini barabara hiyo iwe na msingi wa kutatua tatizo fulani. Hakukuwa na haja ya barabara ile.

3) Ni lazima mtu uwe mwendawazimu hasa kudharau FDI kwenye mchango wa maendeleo ya nchi. Nchi zote duniani zinatafuta FDI. China inapokea FDI kiasi cha $80 billion kwa mwaka kutoka Ulaya na America. Ni FDI ndiyo iliyoibadilisha China kwa kiasi kikubwa. Nchi za Uarabuni na nchi nyingine za Asia na America Kusini, zote, kila nchi inapigania namna ya kuvutia FDI. Halafu usivyoelewa hata unachoongelea - huku unaponda FDI huku unashangilia FDI kutoka Barrick!!

4) Kuhusu ndege - mtu mwenye akili, unapokuwa na limited resources, unaangalia kwanza uwekeze kwenye nini. Mwenye akili atawekeza kwenye projects zenye quick returns. Uwekezaji kwenye usafiri wa anga, kwa ujumla hauna tija. Hii ni miradi ya kuwekezwa zaidi na mataifa yenye surplus. Uwekezaji kwenye ndege, kwa hakika, hautatupatia faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tanesco wanaponunua nguzo mikataba unaenda bungeni? Tanroad wanaponunua mizani mikataba unaenda bungeni? Ukarabati wa mv victoria mikataba ulienda bungeni? Au ndege ndio mumeona nyara ya serikali? Hivi Ni njaa tu zinawasumbua
Pumbavu kwani tanesco hawakaguliwi na CAG?
 
Uongo huo Joka kuu. Mimi ninaishi hapa Canada hakuna kitu kama hicho.

..wewe utakuwa ni illegal immigrant huko Canada ndiyo maana huna bima ya afya ya serikali ya huko


All Canadians and permanent residents can apply for public health insurance. This means that you will not have to pay for medical expenses as this cost is covered by public tax. All Canadians and permanent residents can apply for public health insurance.

eddy
 
a kwanini ujengwe chato? chato ni tambarare ukilinganisha na Geita Bukombe na Katoro ni Giographia tu ndiyo inaruhusu, isitoshe hiyo pesa angeweza kuitumia kuzurura ulaya kama kwenda WEF davos sullivan UN EU AU au hata kwenda kunywa chai na trump ka serve hela na sehemu ya hiyo hela kajijengea kakiwanja shida iko wapi? Kuna waziri mkuu aliwahi kusafiri na msafara wa watu 70 kwenda kwenye graduation ya mwanae marekani na huyuhuyu Lissu akiwa mbunge hakuhoji.
Kuna kitu hukijui. Uwanja wa Chato ulichepuliwa na Magufuli kutoka uwanja uliokuwa umepangwa kujengwa Omukajunguti, Kyaka Bukoba kwa ajili ya kuhudumia biashara ya kilimo cha mboga mboga na maua kutoka DR Congo Mashariki, Rwanda, Uganda kusini na mkoa wa Kagera kwenda soko la Ulaya.

Magufuli alichepua uwanja huo na kuujenga Chato pasipo mipango ya kiuchumi yoyote zaidi ya kumhudumia yeye na familia yake. Ni ubinafsi wa ahali ya juu. Ni kosa la matumizi mabaya ya madaraka (ofisi) ya urais.
 
JPM kama rais anayo ndege yake ya Rais ni kama RC au DC anavyokuwa na gari lake, na akistaafu atapewa hadhi sawa na rais aliyeko madarakani kwa 70% na anataka akaishi chato kuna tatizo gani akiwa na uwanja wa ndege wake? mnataka akae mikocheni kama warioba kila siku kwenye makongamano mwishowe anaanza kupigwa mitama,

GGM wana ndege na wana uwanja wao, Buzwagi wana ndege wana uwanja wao, kesho Lissu anaenda kahama ataenda kupiga show kama zuchu atatua uwanja wa mtu binafsi wa Buzwagi, shida iko wapi? Hivi unaujua uwanja binafsi wa Trump? Cyril Ramaphonsa? Tuache roho ya umasikini hata Bhakresa akinunua ndege tutamjengea uwanja. Grumet game reserve wana uwanja wao, hata kule nzela Geita upo uwanja wa missionary Woolworth, kule murwagwanza ngara upo uwanja wa ndege wa wa missionary wa ki Anglicana.

Mnaongelea mtu kuwa na uwanja wa ndege ni jambo la ajabu ni mawazo ya kimasikini tu, zamani tulikuwa tunaambiwa usijenge nyumba ya bati kijijini utarogwa. Leo tunataka kumroga JPM kisa uwanja wa ndege, mbona tunadhalilisha nchi hivi? Hata world bank wakisikia tunabishania uwanja wa ndege watatucheka.

" hivi jamani kuna tatizo gani kujenga ka uwanja ka kutua home".

Angejenga kauwanja wala tusingesemezana nae mkuu, ila kajenge uwanja wenye hadhi ya mwaliu NYERERE kitu ambocho ni ufujaji wa pesa.

JPM kama rais anayo ndege yake ya Rais

Mkuu sasa yeye ni Raisi na anandege na akistaafu ndege inakuwa sio yake na atakuwa mstaafu kama alivyo Jakaya Kikwete, umewahi jiuliza kiwanja kitatumikaje baada ya yeye kustaafu?

GGM wana ndege na wana uwanja wao, Buzwagi wana ndege wana uwanja wao, kesho Lissu anaenda kahama ataenda kupiga show kama zuchu atatua uwanja wa mtu binafsi wa Buzwagi, shida iko wapi? Hivi unaujua uwanja binafsi wa Trump? Cyril Ramaphonsa? Tuache roho ya umasikini hata Bhakresa akinunua ndege tutamjengea uwanja. Grumet game reserve wana uwanja wao, hata kule nzela Geita upo uwanja wa missionary Woolworth, kule murwagwanza ngara upo uwanja wa ndege wa wa missionary wa ki Anglicana.

Angetaka na yeye angesubili astaafu ajenge kiwanja chake kwa pesa zake na sio kwa pesa zetu sisi walipa kodi, hivyo viwanja unavyozungumzia vimejengwa kwa kodi za walipa kodi wa Tanzania?

Mnaongelea mtu kuwa na uwanja wa ndege ni jambo la ajabu ni mawazo ya kimasikini tu, zamani tulikuwa tunaambiwa usijenge nyumba ya bati kijijini utarogwa. Leo tunataka kumroga JPM kisa uwanja wa ndege, mbona tunadhalilisha nchi hivi? Hata world bank wakisikia tunabishania uwanja wa ndege watatucheka.

Tatizo sio mtu kuwa na kiwanja cha ndege mkuu, tatizo linakuja mtu kutumia pesa za uma kujinufaisha yeye mwenyewe binafsi
 
Back
Top Bottom