Hata niliko mimi bado internet inasumbua sana mpaka watu wanabubujikwa na machozi wanapoona muda unakwenda na wanashindwa kufanya chochote mtandaoni,wakati wengine vifurushi vyao vinakwisha muda wake bila kutumia. Mimi nafanya kazi ya kuwatia moyo na kuwapa matumaini tu kuwa wawe wavumilivu na wenye subira wakati serikali yao kupitia Tcra ikiendelea kufuatilia kwa ukaribu sana suala hili.
Nimewaambia kuwa suala hilo halijasababishwa na serikali yao na wala wasiitupie lawama serikali.nashukuru wamenielewa lakini wameomba mamlaka ziangalie namna ya kuwapatia watu MB za bure kama sehemu ya kuwafidia walau kidogo tu kwa wale waliopoteza mabando yao kwa kuisha muda bila kuyatumia. Nimewaambia serikali yao ni Sikivu na watafutwa machozi yao.