Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

busara yako umeipeleka wapi? Kama wewe DIAMOND anaweza akayumbisha msimamo wako kisa tu kaamua chamgua upande wake tena KIDEMOCRASIA ni ujinga mkubwa.

Angevunga tu kwa msanii mkubwa kioo cha jamii pale ni kua anaipigia debe ccm c kua kaonyesha upande wake na kuna hela anapata c bure. Kitu kingine m namkubali sana ila ajue athari za kutumika na wanasiasa ni mbaya sana kwa muziki wake mfano Marlaw Tz Jaguar Ke wakwapi hiv sasa.
 
Na Mimi nilikuwa nampa shavu sana humu ndani lakini amenionyesha kwamba yeye ni dizaini zilezile za wasanii wajingajinga.

Kwanzia Leo wala sitomtetea humu maana hajielewi.[emoji16] [emoji16]

Mkuu mm mpaka nawish zile kura zng nilizompigia afrimma ningeacha tu" nimemshusha sana mondi, Mtu kashatengeneza brand yake kubwa thn anakua cheap kutumika na wanasiasa utafikiri anatafuta shavu lakua mkuu wa wilaya bwana.
 
Unaposema Diamond kwamba kakosea kumshabikia Magufuli basi unakuwa hujui vinzuri historia ya Diamond. Hao watu watakaomchukia sasa eti kisa anamshabikia Magufuli basi walipaswa waanze kumchukia tangu alipokuwa akisaidiwa na serikali ya CCM.

Diamond ndiye msanii aliyefaidika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Rais Kikwete katika maisha yake ya kimuziki. Mheshimiwa Rais na serikali yake wamekuwa msaada mkubwa sana kwa Diamond. Katika mahojiano na baadhi ya vipindi vya media mfano XXL - Clouds, EFM, Sporah show, na magazeti Diamond amekuwa akieleza wazi kuwa rais JMK amekuwa akimpigia simu mara kwa mara ili kumtia moyo katika kazi zake. Hata JK kwenye hotuba ya kuvunja Bunge hakusita kumtaja Diamond.

Sasa tunapomuona Diamond anakosea, tunapaswa kwanza tujiulize, je huyo mnayemuona anafaa aliwahi kumsaidia kitu gani Diamond katika safari yake ya muziki? Diamond amepata tuzo nyingi tu, je alishawahi hata kumpa hongera kwa tuzo? Au mahaba yenu kwa Lowassa ndiyo mnataka yamuendeshe Diamond katika maisha yake?

Tuache kuingilia uhuru wa watu. Diamond ana kila sababu ya kumshabikia Magufuli na chama chake. Hawa watu wamekuwa msaada mkubwa sana kwa Diamond. Binafsi sijawahi kuona chama chochote cha upinzani kikitoa hata pongezi za kinafiki kwa Diamond. Leo mnataka Diamond aushabikie upinzani, kwa lipi hasa walilomsaidia?

Kama kura za tunzo zinatolewa kwa ushabiki wa vyama basi waache na wasimpigie kabisa. Hii nchi ina watu wa kinafiki sana, eti mnaacha kumpigia kura kisa anamshabikia Magufuli, so what? Ndio maana watu wengi tunaogopa kuchagua upinzani kwa sababu ya visasi vya kijinga kama hivi kwa watu wasiokuwa wafuasi wao. Siasa za chuki namna hii hazitatufikisha popote. Diamond hawezi kushuka kisanii eti kisa watu wa upinzani hawatampigia kura kwenye tunzo. Haitatokea, na kamwe haitaweza kutokea kila mtu ashabikie upinzani, never.

b.jpg


diamond%2Bakiwa%2Bna%2Braisi%2Bkikwete%2Bikulu.jpg




Well said_nail it on them kabisa
 
Mkuu mm mpaka nawish zile kura zng nilizompigia afrimma ningeacha tu" nimemshusha sana mondi, Mtu kashatengeneza brand yake kubwa thn anakua cheap kutumika na wanasiasa utafikiri anatafuta shavu lakua mkuu wa wilaya bwana.
Yaani ametuudhi sana sisi mashabiki wake Mara kumi angebaki kimya.

Tulikosana watu humu ndani sababu ya kumtetea yeye .Halafu Leo anafanya mambo ya mtu Mpumbavu.

Hivi anaogopa nini kama angekaa kimya tu .Yaani anaogopa kauli za ruge.

Naamini hapo alipofika ndo itakuwa climax ya muziki wake.

Asije kulialia kuwa kuna watu wanataka kumshusha wakati ni yeye mwenyewe kwa mambo ya kipuuzi anayofanya bila kufikiria.

Atajibeba mwenyewe.
 
Nilikuwa na mfollow insta ila tangu juzi nilim block kabisa, ndo maana anaambiwa mtoto sio wake
 
Kwa jinsi CCM ilivofanya maisha ya watanzania wengi kuwa mabovu, mtu akii'support automatically namchukia,
Au kisa yeye anapata maji 24/7.....akienda hospital anatibiwa vzur, hajui km kuna wakulima hawana uhakika wa masoko ya mazao yao licha ya kulima kwa shida na ukosefu wa pembejeo, watt wao wankaa chin na walimu hawana, hata walimu waliopo migomo kila siku kwa kuidai hiyo serikal ya CCM...
Mwambien I was supporting him 100%......ila kwa saiz naona km 15% hiv....na sidhan km nitakuja kumpigia kura kwa tuzo zozote zile atakazokuwa nominated!

TANZANIA KWANZA, BURUDANI BAADAE.
 
Kuanzia Leo Mimi sio shabiki wa Daimond najivua gamba navaa gwanda..

Diamond sio mama yangu wala Baba yangu, amepata pesa kawa na kiburi kasahau alipotoka anajifanya hajui CCM ilivyotunyoosha na inavyoendelea kutunyoosha ye anaishabikia na kuweka sababu za kipuuzi.. Zari kajifungulia hospital nzuri aje aangalie huku hospital za kawaida watu wanavyohangaika, hakuna huduma,hakuna madawa, vifaa hakuna, hakuna ajira, maskini tunakandamizwa kwa kulipa kodi, vijana wanasoma lakin ajira hazipo.

Kuitwa Ikulu, Kula Dina sijui wamepewa na nini wamevimbiwa, wanahamasisha tuchague CCM kasahau alivyokua anauza mitumba, CCM ingekua nzuri angesomeshwa bure, elimu ya sekondari ingekua bure nae angeipata.

Yote hiyo ni tunalaumu CCM kwani ndio iliyoshikilia madaraka, na wengine mkome kusema Lowassa ana uchu wa madaraka anaizidi CCM? Mbona nayo haitaki kutoka?

Tunataka mabadiliko kama Baba yako ni Kinana shabikia CCM, kama mama yako ni Tibaijuka shabikia CCM.

CCM tumewachoka!

Cc heaven on desert, TeamLowassa
 
Fanya kazi kwa juhudi utaishi maisha bora tu!!!! Hata kulima nayo ni kazi, kufuga ni kazi nk, Unalalamika maisha magumu lkn wenzako wanajaza barabara kwa magari yao, foleni haziishi tena ndani ya serikali hii hii ya ccm!!

Ninalima pesa inaishia kwenye matumizi hakuna akiba,
Dola ipo juu all imported goods lazima ziwe ghali!
Mfumo wa masoko nao ni mbovu bado unaamini serikali haina mchango katika individual development?
 
Fanya kazi kwa juhudi utaishi maisha bora tu!!!! Hata kulima nayo ni kazi, kufuga ni kazi nk, Unalalamika maisha magumu lkn wenzako wanajaza barabara kwa magari yao, foleni haziishi tena ndani ya serikali hii hii ya ccm!!

na madawa hospital zote ununue wewe sawa unadhan kua na gari ndio kua na maisha mazuri sijasema serikali inipe pesa tunataka social service ziwe nzuri,au we unaishi USA mwrnzetu
 
nimeanza kumkubali tena nassib!dangote!bin laden...hili toto la tandale mang'aa sana linajua kwenda na move!janja sana hili toto...watu wamepanic mara sijui watamunfollow mara sijui hawatopiga kura!..mnyama dangote hana habari!sifa bila mshiko ni ubwege na hilo dogo analijua!...nyie msimpe support wapeni support wasanii wenu wazee kina mkoloni mgosi sijui tumbo tumbo J
 
Fanya kazi kwa juhudi utaishi maisha bora tu!!!! Hata kulima nayo ni kazi, kufuga ni kazi nk, Unalalamika maisha magumu lkn wenzako wanajaza barabara kwa magari yao, foleni haziishi tena ndani ya serikali hii hii ya ccm!!
Kujaza foleni sio indicators za development huduma muhimu ka shule afya hospitali hazina dawa wanawake wanajifungulia chino,shule watoto wanakaa chini pamoja na misitu iliyopo nusu nchi.
Hata kama ufanye kazi twenty four seven kama serikali haiwezeshi wananchi kupunguza ukali wa maisha ni bure. Sasa hivi hela haina thamani hata ukipokea million huwezi Ku save chochote. Fikiria vizuri next time
 
Mkivyoshangilia team domo huyo mond kupiga picha na Rais Ikulu leo mnamgeuka...? Hata hivyo diamond amepata mafanikio kipind cha kikwete rejea kauli yake Siku ile Mlimani city. Mbona cku ile alivyoenda kwa Lowassa hamkuongea acheni wivu nyie au angeenda Ukawa mngembeza kama ambavyo mnafanya akiwa Ccm...? Kwani Sugu au prof. Jay sio wasanii mbona hatusikii mkiwapa hizo kauli...?
 
Baada ya uchaguzi utarudi tuu...

Diamond nae ni mtanzania, ana haki kikatiba, kidemokrasia kushabikia chama chochote akitakacho.
Ushabiki ni kushabikia muziki wake, misimamo yake ya kisiasa mwachie mwenyewe....

#team dangote

Ana haki lakin aangalie wao wenyewe kazi zao zinaibiwa,hawana hatimiliki,wanadanganywa na dinner ya ikulu,basi angeuchunaa,yaan hivi kaniudhi kanitoka puuuuu
 
Fanya kazi kwa juhudi utaishi maisha bora tu!!!! Hata kulima nayo ni kazi, kufuga ni kazi nk, Unalalamika maisha magumu lkn wenzako wanajaza barabara kwa magari yao, foleni haziishi tena ndani ya serikali hii hii ya ccm!!

Hivi umeshawahi kulima na kwenda kuuza mazao sokoni au unasema tu?hata kiranja mkuu siku moja alisema"beba mihogo yako upeleke sokoni bila dalali uone,utabaki unaonjesha watu wee mpaka ikuozee",sio rahc kihivyo no pain no gain.
 
Back
Top Bottom