Kwa hili la Mbowe Marekani na Umoja wa Ulaya wamejitia aibu, ni rasmi sasa kuna kitu wanakitafuta Tanzania


Umeandika maneno mengi na kuchanganya changanya ila kupoteza mantiki, na sikushangai maana ni kawaida ukiandika kwa kupanick. Narudia tena kuwa wazungu wako juu yetu sana, na ni wastaarabu kuliko sisi, hili wala sio la mjadala bali ndio facts. Wao kuwa juu yetu haimaanishi wako perfect, jaribu kutenganisha hayo.

Inaonekana hujui chochote kuhusu CCTV cameras zinafanyaje kazi, ndio maana unasema ziko ndani kwake hivyo azitoe, na tatizo ni kwakuwa ww ni bendera fuata upepo, na huna lolote ujualo. Ni kweli kesi zote zinafanyiwa uchunguzi na polisi, lakini boss polisi ni moja ya taasisi za umma zinazotumikia siasa chafu. Hili wala sihitaji kutumia nguvu kubwa kulieleza. Mimi kama mimi sitegemei chochote serious toka kwenye jeshi hili la polisi zaidi ya aibu.

NB: una uwe mdogo sana wa uandishi, ndio maana huna mtiririko mzuri wa hoja. Paragraph ya Kwanza umeanza na mimi kusifia ubora wa wazungu, kisha paragraph iliyofuata ukarukia ushahidi wa CCTV cameras tena kwa kuchanganyachanganya, huku ukiwa na uelewa mdogo wa CCTV cameras. Halafu ukarudi kwa jazba kuhusu ubora wa wazungu. Katika mazingira hayo ya uelewa mdogo, sishangai ulipokuja na bandiko lililojaa hisia, utoto na propaganda mfu. Unajadili na mtu makini, hilo ulijue.
 
Okay kwahiyo wewe unataka kunambia kuwa police wa huko kwao huwa hawaui majambazi au??

Mimi siwezi kutetea majambazi kama unavyotaka wewe, hata wale maharamia wa kibiti walitetewa hivi hivi lakini sasa hawapo tena.

Vipi ushawahi kusikia ubalozi wa Tanzania huko kwao wametoa matamko ya nje ya kanuni za kidiplomasia kuhusu Jambo lolote huko kwao??

Vipi na wewe unaamini kuwa hujastaarabika kama huyo ndugu yetu anavyosema hapo.??
 
Ubalozi wa Marekani unayo video ya shambulizi la Mbowe ( nimeiona ) , ukiwekewa utakuwa tayari kuomba radhi ?
Marekani haifanyi kazi kimaandazi kwa hivyo huwezi ona hiyo video unless uwe mhusika wa pale. Wewe kwenye ubalozi wa Marekani una wadhifa gani wa kukufanya upate access ya sensitive information kama hiyo.
 
Kwa technology ya mambo ya ulinzi na usalama waliyonayo mabeberu kama mnavyowaita, tayari walishajua ukweli kabla ya polisi kutoa vioja.

Kama wanaweza kuelekezwa tu tukio na kupita eneo husika, kisha kuchora mchoro mpk kumchora muhusika bila kumwona, hawataahindwa kujua ukweli wa hili
 
Nitaendelea kuamini taarifa za Marekani na Ulaya kuliko hizi za kupikwa
Endelea kuamini maana hata Iraq kulikua na sialaha za maangamizi ambazo hazijaonekana mapaka Leo.
Kifupi Jamaa ukiwanyima wanachokitaka wanakuandama na ukiwapa hawana shida na wewe hata uwe na mapungufu kiasi gani.
 
ngoja siku na wewe ukamatwe, uteswe ndo uone MATAGA sio watu
 
Unaamini maigizo yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upi unaoutaka kwamba wapinzani hawakuzuiwa kufanya shughuli zao ?! Unatokea nchi gani wewe ?!

Zamani sisi (WaTz) ndiyo tuliyanyooshea mataifa ya ki dictator na ki baguzi mikono. Leo tunanyoshewa mikono na some time vikwazo . Daahh !!
Umetaja mambo mawili hapo juu, nikakuuliza upo na ushahidi? Swali linahitaji majibu mafupi wewe unaandikka majibu marefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uwezo mdogo unao usema labda ni kutokana na wewe mwenyewe kuto kugundua kuwa ni mtumwa wa fikira za kikoloni ama sivyo basi ni siasa ndio zinakupofusha macho mkuu ndio mana unashindwa kuelewa ninachokiandika hapa.
Hiyo kauli yako tu ya kujidharau na kujiona si kitu mbele ya wazungu ni uthibitisho tosha kabisa.
Nimekuuliza je wewe hujastaarabika??
Ukiitwa nyani na mzungu utakubali??

Wewe ndio uliesema kwenye comment yako hapo kuwa wao wako perfect kwenye sheria zao ila zakwetu sisi huku za kipuuzi, ukamtetea mtu aliyeua mbele ya macho ya watu tena kwa makusudi kabisa kisha anapewa dhamana ukasema wao wanasheria Bora kuliko sisi, lakini ajabu nakuona unaikana kauli yako mwenyewe hapo.

Wewe unaujua vizuri mfumo wa cctiv camera unavyofanya kazi?

Suala hapa si kwamba police wanatumikia siasa chafu bali wewe unataka police wafanyekazi na kutoa majibu kutokana na wewe jinsi unavyo amini ikitokea wakaja na majibu kinyume na Imani na fikira zako basi ni lazima tu utapingana nao kwa mantiki hiyo kwako wewe police hawawezi kuwa na jema kamwe kwasababu mara nyingi huwa wanaenda kinyume na matarajio yako na milengo ya kisiasa uliyo nao.

Usijifu kuwa makini kwa hiki unachokisema hapa hakiwezi kusemwa na mtu makini kama unavyo jinasibu mwenyewe, mtu makini unashindwa vipi kutambua madhara ya matamko ya ovyo ovyo yanayotolewa dhidi ya nchi yako bila kufata sheria za kimataifa halafu unatetea.!!
 
Majambazi saba bunduki 1 kwanini uwaue wote ?! Tunapoteza nini ?!

Ustaarabu ni pamoja na kutendeana haki . Kama hakuna haki upande moja huo si ustaarabu .
 
Bunge litaacha vipi kuongea sasa wakati tukio hilo linahusishwa na serikali kwa uzushi uzushi sasa kwanini bunge lisijadili wakati watu wanavumisha uzushi wa makusudi kuchafua nchi, tena mzushi mwenyewe ni mmoja kati ya wabunge wa bunge hilo hilo.
Ivi unajua kazi ya bunge?? Kazi ya bunge ni kuitetea serikali au mimi labda sijui??
 
Wewe akili yako ndogo saana ..mpaka sasa hujajua tu nini Jiwe anakitafuta..jambo la kusikitisha ni kwamba wewe uliyeandika huu upuuzi hata udiwani hutakaa uone....
Vipi wewe umeahidiwa ubunge viti maalumu?
 
Majambazi saba bunduki 1 kwanini uwaue wote ?! Tunapoteza nini ?!

Ustaarabu ni pamoja na kutendeana haki . Kama hakuna haki upande moja huo si ustaarabu .
Wewe ulitaka wawe na bunduki ngapi ili ndo ujue kuwa ni majambazi??
Au ulitaka wauawe police wangapi ndo ujue kuwa hiyo bunduki moja inaweza kuua??
Wangefanikiwa kufanya tukio lao la kijambazi kwa kutumia hiyo bunduki moja wangeua na kupora mali za watu wangapi??

Okay wao walio staarabika na kutendeana haki ndio pekee wenye ruhusa ya kujitoa kwenye mahakama ya kimataifa ICC ili wasiangaliwe kwa lolote ila wewe huku ambaye bado hujawa binadam kamili ndio ubaki huko.
Pia kwao wao ni ruhusa kufanya chochote nchini kwako ila wewe kwao si ruhusa huo ndio ustarabu sivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…