Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo kama alivyotahadharisha Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.

Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki. Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.

Inatisha.
 
Hofu yangu ni moja tu; isije ikawa kuna vita ya kupromote Migebuka kutoka Kigoma kwa VP, na kuangamiza biashara ya sangara na sato kutoka Mwanza.

Na kama haya mambo yanafanyika kweli, basi Serikali inatakiwa kuchukua hatua mara moja kupambana na huo uhuni, badala ya kutoa tu angalizo.
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo.Kama alivyotahadharisha makamu wa raisi dkt Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi...
hakika....nimetishika sana ukizingatia sipendi red meat na broiler
 
Na wanatumia hayo maji pia hili samaki wasiharibike,hii ni kweli halina ubishi,,,wavuvi wenyewe wanasema,,

Na walaji wa kuku wa kisasa pia si salama.

Bora Dr alinikatazaga kula masamaki ya masafa/kwenye mafriji[emoji23]
 
Endeleeni kula samaki, hakuna utafiti wowote wa kitaalamu kuthibitisha hayo maji ya maiti hata kama kweli yanatumika kwamba yana uhusiano wowote na kupata magonjwa ya kansa, hii ni sawa na story ya kijiweni.

Matatizo ya saratani huko ni kutokana na mazingira ya migodi kuchafua vyanzo vya maji kwa kemikali, labda kwa kiasi fulani kemikali za viwandani na yale madawa ya kilimo yanayotumika karibu na vyanzo vya maji.

Mwisho wa siku hizi kemikali huishia ziwani. uchunguzi ufanyike kama kuna viashiria vya kuwepo kiwango kikubwa cha kemikali hatarishi kwenye maji ya ziwa na kwenye samaki wanaopatikana ziwani hasa ukilenga kujua kiwango cha heavy metals kama mercury, lead nk.​
 
Itasikitisha sana endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo.Kama alivyotahadharisha makamu wa raisi dkt Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.
Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki.Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.Inatisha.
Ndio umejua Leo,maji Yana siri kubwa, hivi mv bukoba ilipozama miili ilikwenda wapi, samaki walijilia
 
Back
Top Bottom