Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Hofu yangu ni moja tu; isije ikawa kuna vita ya kupromote Migebuka kutoka Kigoma kwa VP, na kuangamiza biashara ya sangara na sato kutoka Mwanza.

Na kama haya mambo yanafanyika kweli, basi Serikali inatakiwa kuchukua hatua mara moja kupambana na huo uhuni, badala ya kutoa tu angalizo.

Pengine tumerudia zama za wananchi wanalalamika na viongozi nao wanalalamika. Accident kila siku, panya road, haya na hilo la sangara, hakuna kauli yoyote ya maana.

Badala ya kusema tu tabia hii ikome kabisa. Kwa kauli ambayo wataiheshimu na kuitii. Ndiyo maana siku zote nitamkumbuka JPM.
 
Pole ya nini shemeji mawardat ? Tunakula miaka na miaka sato, leo kisa mtu mmoja kaja na bla bla zake tuache kweli? Kama kufa ingekuwa tayali shem. Acha nile jicho la sato huwa tamuuu [emoji4][emoji4][emoji4]
Mmmmh aisee hapana,

Kuleni tu[emoji23]

Sasa basi huku ziwani kwetu itakuwa hawatumii hayo maji eeeh,

Maana Mbufu ni mtamu[emoji8]
 
Na wanatumia hayo maji pia hili samaki wasiharibike,hii ni kweli halina ubishi,,,wavuvi wenyewe wanasema,,

Na walaji wa kuku wa kisasa pia si salama.

Bora Dr alinikatazaga kula masamaki ya masafa/kwenye mafriji[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa mbna hukuwahi nambia.
 
Mfanyabiashara wa TANZANIA anajali pesa yako na sio afya yako
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa mbna hukuwahi nambia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]tunakula uchafu balaa, jiulize samaki anatoka mwanza hadi songea[emoji23]
 
Kama watu watatiwa hofu kutokula samaki, tusije kujilaumu baadaye kwa kupata tatizo la utapiamlo hasa kwa watoto kudumaa na kwa akina mama wajawazito na wanaonyonyesha kupungukiwa viini lishe muhimu. Tujifunze kupima kauli zetu hasa pale ambapo hakuna utafiti wenye kuondoa shaka umefanyika.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]tunakula uchafu balaa, jiulize samaki anatoka mwanza hadi songea[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tatizo huwa silagi, ko nipo salamaaa.
 
Hofu yangu ni moja tu; isije ikawa kuna vita ya kupromote Migebuka kutoka Kigoma kwa VP, na kuangamiza biashara ya sangara na sato kutoka Mwanza...
Migebuka imezuiwa lini kuingia sokoni?

Nadhani uzalishaji wa migebuka ni Mdogo kuliko mahitaji, demand ni kubwa kuliko supply.
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo.Kama alivyotahadharisha makamu wa raisi dkt Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.
Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki.Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.Inatisha.
Mimi nawaunga mkono mgome kula Sato na Sangara ili soko liyumbe bei zishuke sisi wapenda sato na sangara tufaidike kununuwa Kwa bei ya chini, maana hao Samaki bei imepanda sana.
 
Endeleeni kula samaki, hakuna utafiti wowote wa kitaalamu kuthibitisha hayo maji ya maiti hata kama kweli yanatumika kwamba yana uhusiano wowote na kupata magonjwa ya kansa, hii ni sawa na story ya kijiweni...​
Maji ya ziwa sio kama ya bahari. Ni rahisi kuchafuka.Kama hatua hazikuchuliwa kuzuia sumu kuingia humo basi ni janga kubwa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tatizo huwa silagi, ko nipo salamaaa.
Kama mie [emoji23]

Niliumwaga sana so dokta akaniambia nisitumie hao samaki wa masafa marefu,,,,,nile nyama ya kuku wa kienyeji tu na mayai ya kienyeji,
 
Back
Top Bottom