Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Na wanatumia hayo maji pia hili samaki wasiharibike,hii ni kweli halina ubishi,,,wavuvi wenyewe wanasema,,

Na walaji wa kuku wa kisasa pia si salama.

Bora Dr alinikatazaga kula masamaki ya masafa/kwenye mafriji[emoji23]
Rafiki labda useme chemical ya fomalin lakini sio yale maji
 
Formalin mnapima kwa inzi 🤣🤣🤣🤣 finally nzi nae amepata pakutokea
 
Hapo sasa tunaongelea fomalin na sio maji ya kuoshea maiti
Ishu ya formalin nimeisikia toka kitambo, hata kwenye nyama lala buchani.
Hivi huko visiwani wanapokaa wiki Kukusanya samaki plus siku za njiani kusafirisha hadi mjini aje tena akae kwenye friza dukani kwa umeme usio na uhakika hii chain yote kuna uaminifu gani hapa.
Mfanyabiashara ujali pesa yako na sio afya yako
 
hivi ile mv bukoba ilizama ziwa gani? vipi kuna watu walipotea mazima na maiti zikazaga ziwa zima vipi watu waligoma kula samaki? lete Sato lete sankara kazi iendelee kufa kufaana
 
Hahaha maisha haya
Jana nimesikia tusile maini ya kuku (broiler) .
Mkuu sisi wafrika maisha yetu ni kumuachia mungu tu, ndiye ajuaye, Huku kwenye kuku kumbe wafugaji sasa wanatumia anti bayotic, kwenye filigisi wamekuta mabaki ya tetesaklini!!!hapo utaponea wapi?!!na serikali kudhibiti haya itaanzia wapi haiwezi.
 
bora ule sembe kisha jaziliza virutubisho kwenye mboga na matunda uokoe ini na figo yako.
 
Huyo makamu wako naye amepuyanga tu hamna logic hapo, hayo maneno yalipaswa kusemwa na Mwijaku na si mtu mwenye hadhi ya makamu wa Rais. Jiulize hayo maji ya maiti yana chemicals zipi zinazoweza kukaa kwenye minofu ya Sangara mpaka kumfikia mlaji? Maiti inahifadhiwa kwa kutumia fomarin, inaoshwa kwa maji na sabuni.
Aaache kuwakumbatia wachimba madini ambao ndo wanatiririsha maji yenye mabaki ya Mecury na Zebak kwenda mitoni na hatimaye ziwani. Hamna watu wapuuzi duniani kama wanasiasa. Siku zote wanaangalia matumbo yao tu.
Ndo maana si ajabu kumsikia Pro aliyesoma kwenye chuo maarufu German na kukaa UDSM kwa takribani miaka arobaini alafu anaesema ametolewa jalalani. Ndo maana mnadanganywa eti samaki mto Mara wamekufa kutokana na kinyesi na mikojo ya ngómbe.
Upuuzi kama Upuuzi mwingine serikali inapaswa kuchukuwa jitihada za makusudi kunusuru wakazi wa Kanda ya ziwa na siyo kuleta siasa ambazo hazina kichwa wala miguu. Inashangaza makamu wa Rais naye anapogeuka mpiga ramli chonganishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…