Kama walishahakikishiwa usalama wao nao wakawa tayari kurudi wakikamilisha mambo yao, sioni sababu kwao ya kuogopa kurudi nchini.
This life is too short, waje kuungana na ndugu, jamaa, na marafiki zao waendeleze harakati zao. Kuogopa kurudi nyumbani ni sawa na kuogopa kufanya siasa.
Siasa ni mapambano lazima ukubali kwa lolote litakalo kutokea Jambo la muhimu ni ile dhamira yako uliyonayo ni kutoiacha labda kifo kikutenganishe na dhamira yako .hata harakati za kudai Uhuru duniani kote hazikuwahi kuwa nyepesi Kuna wengine walikufa katika safari ya mapambano walio hai waliendeleza mapambano mpaka dhamira yao ya kudai Uhuru ikatimilika.
Kwa hiyo wao wasihofie chochote Jambo la muhimu Kama wamekubali kuipigania Tanzania kweli kutoka mioyoni mwao basi wasikate tamaa ya kurudi nchini na kuendeleza mapambano yao Ila Kama hawana dhamira yoyote mioyoni mwao basi watakata tamaa na watakuwa na hofu itakayo pelekea wao kuto kurudi nchini.
Shujaa haogopi kufia kwenye uwanja wa Vita/mapambano. Na uwanja wa mapambano ni Tanzania na wala sio huko ughaibuni walipo jihifadhi. Ni hafadhari mara mia moja kufa katika ardhi ya mapambano [ Tanzania ] na kuhesabika Kama shujaa kuliko kufia ng'ambo na kuhesabika Kama mkimbizi wa Kisiasa maana halisi ya mapambano yao haitaonekana wala kuthaminika.
- Hata Mandela alikimbia kwao S.A na kuja kuomba hifadhi kwetu, Mwalimu akahaidi kumpa hifadhi lakini kadiri muda ulivyokuwa una zidi kwenda Mandela aliamua kurudi nyumbani kwao kwenye uwanja wa mapambano [ S.A ] na kuendelea mapambano licha ya kufungwa miaka 27 Ila dhamira yake ya ukombozi nchini mwake haikukoma bali aliiendeleza mpaka ikatimilika .
- Vivo hivyo kwa Kenneth Kaunda , Samora Machel, Robert Mugabe na wengine wengi tuliwapa hifadhi na mafunzo hapa kwetu ila mwisho wa siku hawa kuendelea kuwa wakimbizi wa Kisiasa nchini mwetu bali walirudi nchini mwao kwenye viwanja vya mapambano na kupambania zile dhamira zilizomo mioyoni mwao mpaka ukombozi ukakamilika.
#SHUJAA WA KWELI HAKIMBII UWANJA WA MAPAMBANO BALI ANAFIA UWANJA WA MAPAMBANO.
#MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA FUNGUA FIKRA ZA WATANZANIA WAJIPAMBANIE WENYEWE KUTOKA MIKONONI MWA WANYANG'ANYI.
* ISHI MILELE TANZANIA MAPAMBANO WACHA YAENDELEE✊🇹🇿