Kwa kauli hii ya rais Samia ni dhahiri awamu ya tano ilikuwa 'One Man Show'

Kwa kauli hii ya rais Samia ni dhahiri awamu ya tano ilikuwa 'One Man Show'

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Rais amesema " upigaji ulifanyika awamu ya tano lkn jumba bovu inaanushiwa awamu ya sita. Sitakubali".

Kama angekuwa mshiriki mkuuktk uendeshaji wa serikali ya awamu ya tano rais SSH asingekubali hata awamu ya tano idhalilike.

Lkn anaona ni sawa kwakuwa hakuhusika kwa chochote. Alikuwepo kama picha tu. Mambo yote yalikuwa yakiamuliwa na kuendeshwa na JPM pekee. ....one man show.
 
Wakati anawatoa waliokua viongozi wa awamu iliyopita yeye atakua wapi wakati huo?
Yaani sympathizers wa mafisadi ni wajinga sana. Yaani wana akili finyu sana. Yaani badala ya kujua kuwa Dkt Magufuli aliogopwa na watandaji kiasi kwamba waliogopa kufanya ufisadi na baada ya kufa walishangilia wakijua mkali kaondoka ili waibe wanadhani mama hana akili za kulijua hilo.
 
Kumbe ufisadi mkubwa ulianzia awamu ya tano ya Mungu wa Chato😁😁😁
 
Kama kuna kitu alikosea raisi SSH ni kurith viongozi wa magufuli.
Yaani hujuma lazima itokee
kabisa. Magufulli aliteua watu wenye itikadi na misimamo kama yake. Ambao ni kuwa ikiwa una madaraka basi kauli yako haipingwi na kila unachoamua ni sahihi (rejea wateule wake katika nafasi za ukuu wa mkoa na wilaya). Ni dhahiri SSH hana mtazamo huo, ila kwa vile amerithi wale ambao walikuwa na mtazamo sawa na wa Magufuli, haiepukiki na yeye aidha kuonekana anaelemewa na kiti ama hana jema analofanya.
Kurithi viongozi wa Magufuli kwa SSH kunamithilikia na kuziba bati linavuja kwa kutumia karatasi halafu uje kustaajabu kwanini maji bado yanaingia ndani.
 
Hoja na falsafa za Magufuli ni kaa la Moto aisee ukicheza nazo unakutana na mazingira magumu kabisa mpk utulie uziache ukiendelea kuzipinga unapoteza kabisa ushawishi
Sasa Cha ajabu kuna wasiasa wengi bado hawajagundua hiki kitu hapo ndo naamini kweli tuna wanasiasa weupe mno kichwan

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kitu inaitwa organisation vs re organisation??? Embu tumia muda wako kidogo kusoma hapo

Bwana wee, hizi lectures tumeshazisikia sana nilikua namjibu huyo niliyemnukuu aliyesema Mama alitakiwa asiwachukue waliokua kwenye awamu iliyopita.

Sasa kama yeye mwenyewe alikua sehem ya hiyo awamu iliyopita na mtoa hoja point yake ni kwamba wote waliokua awamu iliyopita, una muenguaje Mama?

Hapo hoja ilitakiwa iwe Mama aweke wazi nini anataka na apate watu anaona watamsaidia kutimiza anachotaka.
 
Rais amesema " upigaji ulifanyika awamu ya tano lkn jumba bovu inaanushiwa awamu ya sita. Sitakubali".

Kama angekuwa mshiriki mkuuktk uendeshaji wa serikali ya awamu ya tano rais SSH asingekubali hata awamu ya tano idhalilike.

Lkn anaona ni sawa kwakuwa hakuhusika kwa chochote. Alikuwepo kama picha tu. Mambo yote yalikuwa yakiamuliwa na kuendeshwa na JPM pekee. ....one man show.
Basi atakuwa mmoja ya viongozi wa hovyo kuwahi kutokea kama unayosema ni kweli. Yaani awe makamu wa rais halafu anyimwe nguvu alizopewa kikatiba halafu abaki kusifu na kutukuza tu kila kilichokuwa kinatokea? Kwa nini hakujiondoa?
 
Hajasema awamu ya tano ila awamu zilizopita. Acha propaganda za kishamba
 
Back
Top Bottom