Ndugu zangu wapendwa naomba tutafakari kwa kina kuhusu kauli zilizotolewa na Magufuli kwamba hayupo tayari kuacha taifa likaangamia, liingie mikononi mwa matapeli na waongo.
Kwa kauli hizi inaonyesha wazi, kwamba Magufuli yeye tu ndio mtakatifu na mwaminifu, ila wagombea wengine ni matapeli na waongo. Sasa swali langu ni hili je hao matapeli na waongo wakichaguliwa na wananchi yeye atakubali kuachia madaraka?
Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ndugu yetu anaamini peke yake ndiye anayestahili kuliko wananchi wengine wote. Kama wananchi wameona hao ni watu sahihi wewe ni nani hata useme ni matapeli? Je hii siyo dalili ya kubaki madarakani kwa nguvu? Nini maana ya Uchaguzi? Kwani taifa linakuwa tu salama likiwa mikononi mwake?
Je hili taifa siyo mali ya Mungu? Ni nani anayeweza kulifanya taifa liwe salama zaidi ya Mungu?
Naomba tujadili maana hii kauli imenishitua sana.