Kwa kipato cha Tsh. 200,000/- kwa mwezi naweza kujenga nyumba?

Shukrani sana Poker nimeichukua hii ila mawe kwa mkoa wa pwani sidhani kama yapo
 
Chakarika, kuna aliyeanzia na kuuza karanga na akajenga. Ni akili tu kichwani. Ila nidhamu ya pesa ni muhimu.
 
Mwanzo tu ndio huwa mgumu, ukishatia nia, ukaamua kuanza... utafikia lengo na utamaliza nyumba hata kama itakuchukua miaka 8 lakini utamaliza!

2006 naanza kazi (17yrs) (ajira kampuni binafsi) nikiwa napokea nett pay(take home) 230,000 sikuwa na familia bado, nilijibana miezi miwili nikanunua uwanja 400,000 nikaanza ujenzi hata sijui nitakuja kumaliza lini!...

But I can assure you niliimaliza 2008 ...by the way UJENZI HAUNA MWISHO(TIMELINE)

Note: nilijiongezea mwaka mmoja kwa hr...ili niwe nimetimiza umri rasmi wa kuajiriwa... maana nilikuwa nakatwa paye na nssf...na mpaka leo huo mwaka(wa nyongeza)uko unasoma rasmi kwenye kitambulisho cha nida
 
Umenipa nguvu kumbe inawezekana
Shukrani sana.
 
Kujenga nyumba inawezekana kwa 100% ila unapaswa kabla ya kuamua kujenga ujue unahitaji nyumba ya aina gan muda utakaotumia mpaka kumaliza hii itakupa nguvu ya kutokata tamaa kuwa na nidhamu ya pesa matumizi ambayo sio ya muhimu yaache
 
Kama una hisa, vyama unaweza kukopa mkopo ukafanya unachotaka kufanya kw amara moja hata kama ni nusu yake, marejesho ya laki mbili kwa mwezi mkopo wake huwa mkubwa ! Jaribu kuliangalia hili..
Hapana sina na hua naogopa sana mikopo kwa kweli.
 
Kujenga nyumba inawezekana kwa 100% ila unapaswa kabla ya kuamua kujenga ujue unahitaji nyumba ya aina gan muda utakaotumia mpaka kumaliza hii itakupa nguvu ya kutokata tamaa kuwa na nidhamu ya pesa matumizi ambayo sio ya muhimu yaache
Nahitaji nyumba ndogo, chumba kimoja, sebule, jiko na choo, sina mambo mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…