Kwa kizazi hiki inawezekana kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu?

Kwa kizazi hiki inawezekana kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu?

Kwamba zamani yaani kizazi kile ndio haya mambo hayakutokea ? Sema tu sasa hivi na wanawake wamejiunga kwenye game kwa uzaidi ila kwa wanaume hii itakuwa ni muendelezo tu..., kwanza wengine hata Imani zao zinawaruhusu....
Yalikuwepo,lakini nadhani mabadiliko hasa ya kitknolojia na malezi yamechangia kuchochea Kwa kiasi kikubwa upotevu wa maadili.
Zamani tech haikuwa imetapaka kama hivi Leo,mtu aliepo bukoba anaweza kuwasiliana na kuonana live na mtu alieko tunduma mfano Kwa video call mda wote akijiskia.je zamani?
Fikiria Sasa namnaa usaliti unavyorahisishwa na tech

Itoshe kusema sisi tumezidi
 
Mungu atusaidie kizazi hiki hali ni mbaya. Kuna muda unajiuliza tofauti ya sodoma na gomora na kizazi hiki iko wapi?

1. Wanaume kuwa mashoga imekuwa jambo la kawaida (wanajiuza mpaka kwenye mitandao) na wateja ni wengi tu.
2. Kuingiliana au kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile imekuwa kawaida na watu hawaogopi kabisa
3. Kuchepuka ndio usiseme (hata wew umeliona)
4. Watu kufanya mapenzi kwa makundi bila hata haya imekuwa kawaida wanaita 'threesome'

Mungu anaweza kukichoma hiki kizazi hata kabla ya siku ya mwisho sababu yaliyokuwa yanafanyika sodoma na gomora hata sasa yanafanyika. Tuna sababu ipi ya kutopata adhabu kama ya watu wa sodoma na gomora??
Msamaha umerahisisha mambo.Mungu wetu amejaa rehema so Kwa kustahimili tunaweza toka wachache tukatubu na kuokolewa.
 
Mwishowe mwanifu anakatantamaa, na kuwa kipanga mpya. Mwaminifu pia huwa ana weakness moja, anaamini anaweza kumbadilisha kipanga. Kipanga habadiliki moaka atakapo taka
Kipanga wa kiume hubadilika pale pesa zinapoisha😂😂
 
Yalikuwepo,lakini nadhani mabadiliko hasa ya kitknolojia na malezi yamechangia kuchochea Kwa kiasi kikubwa upotevu wa maadili.
Zamani tech haikuwa imetapaka kama hivi Leo,mtu aliepo bukoba anaweza kuwasiliana na kuonana live na mtu alieko tunduma mfano Kwa video call mda wote akijiskia.je zamani?
Fikiria Sasa namnaa usaliti unavyorahisishwa na tech

Itoshe kusema sisi tumezidi
Maadili kivipi ? Zamani kutokana na kwamba ilikuwa kwa binti wa kike kupata ujauzito anaonekana kama mchawi watu walitupa watoto (Je hayo yalikuwa maadili)?

Kuna kabila zilikuwa mtoto wa kike akijifanya anaringa wanamchukua wadau wanakaa nae huko sababu amelala nje hivyo inakuwa ngumu kurudi kwao wanamfungisha ndoa ya mkeka....

Kuna watu walikuwa wanachumbia mtoto tangia amezaliwa kwamba huyu atakuwa wa yule....

In short kuna upuuzi ulifanyika hata zamani ni kwamba tu ulikuwa unajificha..., na mimi ingawa ni mwanaume takuwa sisemi ukweli nikisema kwamba mfumo wa zamani ulikuwa ni mfumo dume ambao haukuwa rafiki kwa watoto wa kike....

By the way unapoongelea maadili wakati kuna maadili yanayosema mwanamme mmoja kuwa na wanawake mpaka wanne hapo huwezi kusema mtu kuwa na mpenzi mmoja sababu hata kuwa nao wanne bado takuwa ni mwaminifu.... Vilevile kuna tamaduni za mwanamke mmoja kuwa na wanaume zaidi ya mmoja..., au kulikuwa na tamaduni za kimasai mwenye nyumba akiondoka akija mwanaume mwingine ruksa kumiliki hio nyumba.... (morals are just how people persive them but they are not necessarily perfect)
 
Kwa dunia ya leo ingia kwenye mahusiano ukijua kwamba kila mtu anacheat, kupunguza machungu angalao tafuta ambae anajilipia bill zake mwenyewe.

Mwanamke na mwanaume kila mmoja ajilipie bill zake mwenyewe angalao cheater akishtukiwa basi mtaweza kuachana bila ugomvi kwa sababu hakuna ambae atakua amewekeza kwa mwenzake.
 
Inawezekana Sana ila Huwa ni maamuz ya mtu binafs
Kesi nyingi zinatokana na kutokubali kupitwa na baadhi ya vitu na kutoridhika na mwenza ulienae .mwisho tuoe na kuolewa na tunaowapenda
 
Back
Top Bottom