Una kichwa kizito. Familia ya 'ke inapotoa binti yao aolewe ni kama 'wanapoteza' rasilimali. Wakati upande wa pili wanavuna matunda na juhudi ya ulezi waliyofanya wazazi na ndugu wa binti
Mwanamme anapoteza nini? Au wazazi wake wanapoteza nini? Atazaliwa watoto wataoitwa kwa jina lake Na kuendeleza ukoo wa mwanamme
Nilijua tu utakuja na hoja nyepesi ambazo hazina uzito wowote wa kimantiki.
Eti
familia ya KE inapotoa Binti yao aolewe ni kama wanapoteza rasilimali... Kwa dunia hii ya leo? Hii hoja yako ingeweza kuwa na mashiko kama tungekuwa Bado tuko miaka ya 1970s huko lakini sio leo hii, yes, zamani Binti akiolewa alikuwa anaenda kuwa chini ya umiliki wa mume wake kwa maisha yake yote yaliyobaki na mume wake huyo atamtumia kwenye shughuli za uzalishaji Mali kadri anavyotaka na Binti huyo akuruhusiwa kurudi nyumbani kwao haijalishi ni changamoto gani atazopitia kwenye ndoa yake.
Hebu Sasa tuangalie suala hili kwa dunia ya leo hii kama Bado mantiki yake ni ile ile... Je, Sasa hivi wanawake Bado mkiolewa mnaenda kuwa chini ya total ownership ya mumeo kana kwamba chochote unachokuwa unakifanya kinakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya mume wako kama ilivyokuwa kwa mabibi zetu?? Jibu ni
HAPANA.
Siku hizi wanawake mnaolewa mkiwa tayari mna career zenu ambazo wazazi wako wamekujengea kwa kukusomesha, licha ya wewe kuolewa ila wanakuwa wanategemea kupata misaada kutoka kwako kupitia hiyo career yako. Kwa hiyo Sasa unakuta wewe umeolewa lakini Bado una uhusiano wa karibu sana na familia yako kwa maana ya kuwapa misaada na hivyo wanakuwa hawajapoteza nguvu kazi yoyote ile.... Na kama hiyo haitoshi unakuta Kuna muda unamshirikisha mume wako kutatua shida za nyumbani kwenu na anafanya hivyo kama uwezo Yuko nao....Sasa hapa Bado unasema wewe Binti ukiolewa familia yako inapoteza nguvu kazi??
"
Mwanaume anapoteza nini? au wazazi wake wanapoteza nini?"
Wewe dada hivi kabla ya kuuliza hayo maswali ya kitoto ukifanya tafakari kwa kuangalia na uhalisia wa maisha ya leo? Au umeuliza tu kulingana na ulivyokariri maandiko?
KWa hii Karne tuliopo kwenye suala la ndoa mwanaume na familia yake wanapoteza vingi sana, wakati huo mwanamke na familia yake Wana gain vingi sana...
Mwanaume akioa kama yeye alikuwa ndio nguzo huko kwenye familia yake, itabidi apunguze majukumu na kuanza kuingalia familia yake mpya ambayo ni wewe... Yaani kama alikuwa anasomesha wadogo zake itabidi aache, kama alikuwa anatunza wazazi wake itabidi aache au apunguze, yaani kwa maana nyingine familia yake Inakuwa imepoteza nguvu kazi au rasilimali muhimu kwa ajili yako.
nimewahi kuona mwanaume aliyeacha kusomesha wadogo zake na kisha kuanza kumuendeleza kielimu mke wake mara tu alivyomuoa, halafu huyo mke baada ya kumaliza masomo yake na kupata kazi nzuri akaanza kuwasomesha wadogo zake(yaani shemeji zake na mumewe)... Sasa hapo ni familia ya nani ilipoteza?
Wanaume Karne hii wanaoa wanawake ambao wanalingana nao vipato au muda mwingine wanawake wao wanawazidi vipato, lakini pesa inayotumika kwenye ujenzi wa familia kama kununua assets, kujenga n.k kwa kiasi kikubwa unakuta ni ya mume, ila siku ndoa ikivunjika wanagawana Mali hizo 50-50, halafu bado unuliza mwanaume anapoteza nini akioa?
Hilo suala la mtoto kuitwa ubini wa baba ni hoja isiyokuwa na kichwa Wala miguu... Mtoto anaweza akabeba jina langu lakini asiwe na connection yoyote na Mimi yenye faida, angalia hata bwana Nasibu amebeba jina la Abdul.
Bado hujaleta hoja ya maana ni kwanini tuendelee kuwatolea mahari???