Aisee dada nakushuru sana kwa huu mtazamo ulionao.Mimi huwa nawaambia wanaume humu kuchukua actions, mnatakiwa kuadvocate mambo yanayomkandamiza mwanaume na kuyafanyia kazi . Kulalamika hakusaidii sana.
Wanawake tulipochoka tulikutana Beijing😂😭
Kitendo tu Cha wewe ku-realize kwamba Kuna ukandamizaji wa kimfumo(systemic marginalization) anaofanyiwa mwanaume ni uungwana wa Hali ya juu mno... Wanawake wenzako wengi wa sasa hawaamini kabisa kwamba zama hizi hata mwanaume pia anakandamizwa, Sasa wewe kulitambua hili inaonesha ni mtu wa Mungu sana na mpenda haki wa kweli.
Kuhusu kuongelea au kuchukua actions dhidi ya male systemic marginalization na gender biases ni jambo ambalo linafanyika sana lakini kwa bahati mbaya yeyote anayefanya hivyo anaishia kudharuliwa,kupuuzwa na kuonekana ni mjinga aliyekosa kazi ya kufanya na hakuna anayempa attention.
Canada Kuna watu wanaitwa MRA(Male Rights Activists) Hawa ni kundi la watu wanaotetea haki za wanaume, mara nyingi huwa wanatarget mambo kama male child molestation, unfair divorce laws,child custody laws, domestic violence against men, sexual harassment, spousal settlements etc...
Sasa nini huwa kina wakuta Hao MRAs kwenye hizo harakati zao za kumtetea mwanaume? Wanaambiwaga wao ni watu waliokosa kazi za kufanya na ni maadui wakubwa wa wanawake(misogynists) na zaidi ya hapo hata podcasts zao huwa hazipewi airtime kwenye mainstream medias na ndio maana hata hawajulikani, na mbaya zaidi wanaongoza kuwapiga vita ni wanaume licha ya kwamba agenda waliyonayo ni beneficial kwa mwanaume..!!
Ukitaka kumkomboa mwanaume ni kujiingiza kwenye vita Kali sana
Nafikiri unajioneaga hata humu jamvini jinsi gani kijana wetu Natafuta Ajira anavyokutana na upinzani mkali kwenye threads zake.
Inahitaji mtu mwenye open-mindedness na hofu ya Mungu hili kuona social injustice anayofanyiwa mwanaume miaka hii... Na ndio maana wewe dada nimekupa heko sana na kwanzia leo nitakuwa follower wako.