Very sad. Mtu amekwenda kanisani kumfuata Yesu, lakini kiongozi badala ya kumlinda na kumjenga anamsakama kwa kutaka kulala naye. Binti amemkataa, ghafla anaanza kusambazwa kuwa ni mwizi.
Kama haya ni kweli, huu ni unyanyasaji na matumizi mabaya ya nafasi ya uongozi. Kukataliwa hakumpi mtu haki ya kuchafua jina la mwingine. Kama kuna ushahidi wa wizi, uwasilishwe wazi; kama hakuna, tuhuma hizi zisambazwe kwa msingi gani?
Sisi kama jamii hatupaswi kukaa kimya. Taka suala hili lichukue mkondo wa haki, lakini kwa ushahidi na kwa kufuata taratibu sahihi. Kanisa linapaswa kuwa sehemu ya usalama na maadili, si sehemu ya mtu kutumia cheo chake kumlazimisha au kumdhalilisha mwingine.