Kwa kweli Bongo bado sana

Kwa kweli Bongo bado sana

Nimefikia kwenye kibanda changu nilijenga kigamboni kizota huku lakini hata huku bado naona ni maporini tu niludhani daraja litabadilisha kukuza kigamboni bado sana
Kisota unaijua vizuri lakini? Hebu jipe muda utembelee baadhi ya mitaa
 
Hahaha wazungu choka mbaya.

Mkuu hao wamejaa kigamboni huku sijui hata wanatoka nchi gani.
Wengine wamepanga kabisa mtaani huku asubuhi tunakutana nao kwenye mihogo.
Kuna wazungu nilipanga nao nyumba moja wale wanaokopesha vyombo enzi hizo ndo wanaanza hizi mishe

Aisee, wale jamaa sijui wanaishi vipi,
Wamepigika kinomanoma,
Wanalala chini,
Wanavuta fegi hatari
Hela hawana hata ya kununulia chai
Ukiwaona viwanja sasa
Wanatamba balaa
Watu full kuwa shobokeA
 
Mkuu,

Weka mapicha basi na wewe tuone Bongo ilivyochoka.

Mimi nilirudi hivyo hivyo nikashangaa barabara zina mashimo mpaka Oysterbay shuleni.

Bongo lile jua tu linapausha vitu, ukipaka rangi leo, miei sita pashanyauka.
Aisee Mkuu
Nitafanya hii project uone mwenyewe
Obey kuna mitaa mixhache sana tu ndio inebakia poa kwa utulivu
Zile nyumba zote za vigae zimegeuzwa pubs na vibar mshenzi
 
Wazungu choka mbaya nao wamekuja kudanga huku kwa wadada na wakaka masikini wale kitu cha moto nachuro sio wale kitimoto wenzao wanaowakimbia huko
Ndio wanapita na boda mpaka kuzimia kwa mujibu wa JF news. Yani wazungu choka mbaya wanakuja kutuf#@ria watoto wetu ?
Hao wazungu wafukuzwe mara moja.
 
Baada ya kukaa nje ya nchi bila kutembelea nyumbani kwa takbirani miaka 10, juzi nimetua bongo kwa matarajio mengi ya kuona yake mapichapicha ya mitandaoni, lakini nilichokikuta ni hakina tofauti yeyote kuonyesha miji wa Dar es Salaam kuwa umejengeka

Kwanza nimechoshwa na uwingi wa watu bila mpangilio, yaani watu wapowapo tu wamekaa na kusimama kila sehemu ya Mji bila shughuli, hata kama baadhi ya barabara zimejengwa lakini watu wakaakaa pembezoni na kazi Yao kuvuka upande huu na ule wa barabara kutwa nzima na wachuuzi wametanda barabara nzima mpaka barabara zinakosa mvuto.

Ile mitaa ilikuwaga ya utulivu na kishua sio tena hivyo ni makelele ya bodaboda na wapiga debe usiku kucha.

Katikakati mjini uhindini kila nyumba imegeuzwa restaurant viti vimejaa maeneo ya watembea kwa mguu.

Halafu pia mji umejaa wazungu choka mbaya sijui wanatokea nchi gani?

Yaani nimesikitishwa na nimetapeliwa na mapicha ya mtandaoni
Kwa kweli Bongo bado sana na Tena sana.

Povu ruksa!
Wachache watakuelewa bongo ni ya kifala sana. Huitaji kwenda ulaya kulijua hilo, nenda tu pale Nairobl ukae mwezi mmoja afu urudi Bongo kudadeki utakubaliana na wazungu wanaosema Dar ni kijiji pembezeno mwa bahari ya hindi.

Sisi mipamgo miji yetu ni ya kimaskini sana. Afu serikali haijengi miundombinu ya maana kupendezesha miji. Badala yake watu binafsi ndiyo wanaojijengea migorofa huku mitaani
 
Satellite ni kifaa kilichowekwa kwenye obiti kuzunguka Dunia kwa sababu za kisayansi, kijeshi au mawasiliano
Mimi nafikiri hapo valid objection labda ilikuwa kwenye neno city, si kwenye neno satellite.

Satellite ni kitu kinacho zunguka, inacho orbit, au kwa miji, sehemu iliyo nje ya mji mkubwa.

Neno "satellite city" linapotumiwa, hiyo "satellite" haiwakilishi maendeleo makubwa ya kiteknolojia.

Mji hauitwi "satellite city" kwa sababu una maendeleo ya kiteknolojia kwa kushabihiana na satellite.

Mji unaitwa "satellite city" kwa sababu mji unakuwa umekaa pembeni ya mji mkubwa kama satelite ilivyokaa kwenye kitu inachokizunguka.
 
Back
Top Bottom