Kwa kweli Bongo bado sana

Nimefikia kwenye kibanda changu nilijenga kigamboni kizota huku lakini hata huku bado naona ni maporini tu niludhani daraja litabadilisha kukuza kigamboni bado sana
Kisota unaijua vizuri lakini? Hebu jipe muda utembelee baadhi ya mitaa
 
Hahaha wazungu choka mbaya.

Mkuu hao wamejaa kigamboni huku sijui hata wanatoka nchi gani.
Wengine wamepanga kabisa mtaani huku asubuhi tunakutana nao kwenye mihogo.
Kuna wazungu nilipanga nao nyumba moja wale wanaokopesha vyombo enzi hizo ndo wanaanza hizi mishe

Aisee, wale jamaa sijui wanaishi vipi,
Wamepigika kinomanoma,
Wanalala chini,
Wanavuta fegi hatari
Hela hawana hata ya kununulia chai
Ukiwaona viwanja sasa
Wanatamba balaa
Watu full kuwa shobokeA
 
Sema bongo Bado sana kama jamaa anavyosema, kuna ka mji sijui ni mkoa gani kanajengwa naona ilo eneo wamepaita "Satellite City " nikashangaa nikaasema satellite city wakati matundu ya choo bado wanajenga mpaka leo, hivi wanajua maana ya neno satellite
 
Mkuu,

Weka mapicha basi na wewe tuone Bongo ilivyochoka.

Mimi nilirudi hivyo hivyo nikashangaa barabara zina mashimo mpaka Oysterbay shuleni.

Bongo lile jua tu linapausha vitu, ukipaka rangi leo, miei sita pashanyauka.
Aisee Mkuu
Nitafanya hii project uone mwenyewe
Obey kuna mitaa mixhache sana tu ndio inebakia poa kwa utulivu
Zile nyumba zote za vigae zimegeuzwa pubs na vibar mshenzi
 
Wazungu choka mbaya nao wamekuja kudanga huku kwa wadada na wakaka masikini wale kitu cha moto nachuro sio wale kitimoto wenzao wanaowakimbia huko
Ndio wanapita na boda mpaka kuzimia kwa mujibu wa JF news. Yani wazungu choka mbaya wanakuja kutuf#@ria watoto wetu ?
Hao wazungu wafukuzwe mara moja.
 
Wachache watakuelewa bongo ni ya kifala sana. Huitaji kwenda ulaya kulijua hilo, nenda tu pale Nairobl ukae mwezi mmoja afu urudi Bongo kudadeki utakubaliana na wazungu wanaosema Dar ni kijiji pembezeno mwa bahari ya hindi.

Sisi mipamgo miji yetu ni ya kimaskini sana. Afu serikali haijengi miundombinu ya maana kupendezesha miji. Badala yake watu binafsi ndiyo wanaojijengea migorofa huku mitaani
 
Satellite ni kifaa kilichowekwa kwenye obiti kuzunguka Dunia kwa sababu za kisayansi, kijeshi au mawasiliano
Mimi nafikiri hapo valid objection labda ilikuwa kwenye neno city, si kwenye neno satellite.

Satellite ni kitu kinacho zunguka, inacho orbit, au kwa miji, sehemu iliyo nje ya mji mkubwa.

Neno "satellite city" linapotumiwa, hiyo "satellite" haiwakilishi maendeleo makubwa ya kiteknolojia.

Mji hauitwi "satellite city" kwa sababu una maendeleo ya kiteknolojia kwa kushabihiana na satellite.

Mji unaitwa "satellite city" kwa sababu mji unakuwa umekaa pembeni ya mji mkubwa kama satelite ilivyokaa kwenye kitu inachokizunguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…