Kwa kweli ni wakati muafaka wa rais Samia kuachana na Paul Makonda, taswira ya rais wetu inaharibika kwa kasi sana.

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Sina uhakika kama mheshimiwa rais Samia anafahamu taswira anayojijengea mbele ya umma wa Watanzania kwa kuendelea kumpa Paul Makonda nafasi katika serikali yake.

Kwa kipindi kifupi tu cha wiki moja tangu Makonda ateuliwe kuwa RC wa Arusha, mtizamo wa watanzania kuhusu rais Samia umebadilika sana, umekuwa mbaya mno!

Paul Makonda anamchonganisha rais Samia sio tu na viongozi wengine wakubwa serikalini bali pia na wananchi walio wengi.

Hulka ya Paul Makonda imekuwa ni kama ya mtoto mdogo ambaye kila wakati anatafuta attention ya mama yake, na kujiona wa maana kuliko mwingine yeyote yule. Uongozi unahitaji ukomavu wa kiakili na kisaikolojia, hayo yote bado hayajaonekana kwa Paul Makonda.

Kama rais Samia ni msikivu kwa wananchi na kama amedhamiria kubadilisha staili mbovu ya uongozi tuliyonayo, basi aachane na Paul Makonda sasa hivi kabla mambo hayaharibika zaidi.
 
Mh. Rais wetu Samia hana independent thinking, deep independent thinking! Kwamba hili silitaki katu! Akalikataa kwa dhamira safi! hana uwezo huo na thinking yake haiendi huko!. Kitendo cha kumrudisha makonda kinamnyima sifa ya kuwa na rational thinking,rational thinker, independent one!
Makonda anajulikana kwa maovu aliyoyafanya na magufuli, leo anamuweka tena utumishi wa Umma. Ni dharau, ubabe, dhihaka aliyo nayo Samia!
 
Hakuna kinachoweza zuia "uchawi wa kizungu" ........
 
Afanyie kazi ushauri wako, itafika wakati watu wataona bora hata Group lao la WhatsApp lina heshimika kuliko ikulu.

Eti mama yangu....mama yangu, so what?! Inakuwa kama watu wanajipikilisha bana
 
Ndio wanasemaga "Fitna kwao mwiko?!" Chama kimejaa Majungu hivyo...
 
Kwa makonda hangaya kayakanyaga ange mdump faster aendelee na mambo mengine.

Hawezi kumsaidia kama ilivyokuwa kwa magu mwishowe alimchinjia baharini.

Lakani akishupaza shingo bashite ata tita kwenye viganja vya hangaya.
 
Umesema ukweli kabisa mwamba! Makonda amefanyiwa uchunguzi na FBI na CIA na kuonekana ni mhalifu!!
 
Koma bro..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…