Sina uhakika kama mheshimiwa rais Samia anafahamu taswira anayojijengea mbele ya umma wa Watanzania kwa kuendelea kumpa Paul Makonda nafasi katika serikali yake.
Kwa kipindi kifupi tu cha wiki moja tangu Makonda ateuliwe kuwa RC wa Arusha, mtizamo wa watanzania kuhusu rais Samia umebadilika sana, umekuwa mbaya mno!
Paul Makonda anamchonganisha rais Samia sio tu na viongozi wengine wakubwa serikalini bali pia na wananchi walio wengi.
Hulka ya Paul Makonda imekuwa ni kama ya mtoto mdogo ambaye kila wakati anatafuta attention ya mama yake, na kujiona wa maana kuliko mwingine yeyote yule. Uongozi unahitaji ukomavu wa kiakili na kisaikolojia, hayo yote bado hayajaonekana kwa Paul Makonda.
Kama rais Samia ni msikivu kwa wananchi na kama amedhamiria kubadilisha staili mbovu ya uongozi tuliyonayo, basi aachane na Paul Makonda sasa hivi kabla mambo hayaharibika zaidi.