Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?

Inategemea na uongozi ulipo, ila sisi wanachama wa TLS, individually tumepigia kelele sana tuu.
P
Paskali sijawahi kuwa na imani na Uzalendo wako kwa nchi hii.

Japo huogopi kutoa maoni yako, na wala hukuhangaika kuja na ID fake, huku JF, lakini bado Uzalendo wako kwa Taifa hili, unatia shaka.

Hivi kwa nini usiwaeleze tu serikali kwamba huu Mkataba wa DP World ni kitanzi kwa uhuru wa Nchi yetu?!!
 
Paschal, sijaelewa hapo namba 10.
Serikali ilishinda au ilishindwa?
Na kama ilishinda, kwani unaliza juu ya ukimya wa TLS?
1. Serikali ilishindwa mara ya kwanza, baada Mahakama Kuu kutengua sheria batili, kakata rufaa ikashindwa tena.
2. Baada ya kushindwa, serikali ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura na kuuchomekea huo ubatili ndani ya katiba yetu.
3. Ikashitakiwa tena, ikashindwa baada ya Mahakama Kuu kuamuru mabadiliko hayo ya katiba ni batili na yamechomokewa kiubatili.
4. Serikali ikakata Rufaa, Mahakama ya Rufaa ikaipa serikali ushindi kuwa batili ikiishachomekewa kwenye katiba, Mahakama haina uwezo kuucholopoa ubatili huo bali ni Bunge lenyewe ndio liuchomoe!.
P
 
Paskali sijawahi kuwa na imani na Uzalendo wako kwa nchi hii.
Uzalendo wa kweli hukaa ndani ya mtu na sii lazima uonekane.
Japo huogopi kutoa maoni yako, na wala hukuhangaika kuja na ID fake, huku JF, lakini bado Uzalendo wako kwa Taifa hili, unatia shaka.
Huo ni mtazamo wako, na everyone has the right to h/is/or opinion na wengine wote wana wajibu wa kuheshimu mawazo yako hata kama hukubaliani nayo.
Hivi kwa nini usiwaeleze tu serikali kwamba huu Mkataba wa DP World ni kitanzi kwa uhuru wa Nchi yetu?!!
Bado hakuna mkataba wowote !. Hiyo IGA ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA, bado!. Kanisome hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
P
 
Sawa Mkuu, nimekupata.
Nitapitia hapo, maana mimi ni mfuatiliaji mzuri wa makala zako..
Ila sema tu wakati mwingine huwa unanichanganya sana Mkuu..
Huenda ndo maana hata Hayati JPM alishindwaga kukuelewa akakuita "Bwana Njaa" ( tafsiri ya Mayala).
😁😁
 
Kuna mstari mwembamba sana unaomtenganisha Pascal na Kitenge..
Tunafanana sana, wote ni watangazaji majasiri kweli kweli, tofauti ni tunatofautiana vipaji, wengine ni watangazaji wenye vipaji vikubwa wengine vidogo, pia ukitafuta CV zetu, you can see the difference.
Ajenda zote mbovu za wanasiasa huwa promoted na nyie wanahabari uchwara.
Kuniita mwanahabari uchwala ni kunitukana!, huku sio kunitendea haki!.
P
 
Alisema hasikilizi makelele! Hii ni zaidi ya kelele
 
Asante kwa ufafanuzi unaojitosheleza ingawa swali langu hukulijibu moja kwa moja.

Najua, IGA ni mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa. Kama ungebaki kwa makusudi hayo bila kumpa mamlaka DPW, nisingeendelea kuuliza. Nina maana kwamba mkataba wa IGA (kama Tanzania na Dubai haukuwepo!) ungetoa fursa kwa makampuni ya Dubai kuwekeza Tanzania na DPW ingeomba kufanya hivyo kupitia Sheria, Taratibu na Kanuni zetu za uwekezaji.

Je, kuna nini nyuma ya huo mkataba wa IGA? ndilo swali linaloibua sintofahamu kwa kuwa una vifungu, kama ulivyochambua na nivyoelewa, ambavyo vina ukakasi na ni batili.
 
Ila wakati mwingine huwa unanichanganya sana Mkuu..
Huenda ndo maana hata Hayati JPM alishindwaga kukuelewa akakuita "Bwana Njaa" ( tafsiri ya Mayala).
😁😁
It's true baadhi ya mada zangu, kama ni kichwa panzi, utaishia chaka!. JPM hakushindwa kunielewa bali... let's let him rest in peace.

Ila kiukweli kabisa, kati ya watu walionielewa ni JPM!. Mkiisha mjua mtu ni mpenda misifa, msifie kisha utupie mnofu kwenye ndoana, anameza mzima mzima mazima, hivyo kiukweli kabisa tumemsaidia sana JPM!.

Mfano mzuri ni baada ya bandiko hili Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!, uliona tena ziara za kushtukiza?.

Baada ya bandiko hili Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?! na hili Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu! mliona tena utumbuaji wa kibwege bwege?, niliuliza humu Je, inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!

Baada ya bandiko hili Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!, ulikuja kuona kikao cha CCM ikulu yetu?.

Hivyo JPM tumemsaidia sana. Sasa ni zamu ya Samia, tunamsaidia!.
P
 
Hili wasingelikubali kwasababu wangetakiwa kwanza kupewa kitu kiitwacho A CERTIFICATE OF COMPLIANCE na kusajiliwa kama kampuni la Tanzania kule BRELA. Kule Uingereza DP World wamesajiliwa kama DP World London Gateway, hivyo wanakuwa chini ya msajili wa makampuni ya Uingereza. Sisi huku kwetu hawajafanya hivyo kwasababu wanafahamu fika, wakifanya hivyo itakula kwao. Unakumbuka yale ya bwana Aliko Dangote na Mzee Chuma ???

Tanzania na Nigeria hatukuwa na BIT wala IGA, ila mzee wa watu akaja akawekeza hivyo-hivyo kwa kupewa ahadi kibao na Mzee Jakaya. Kampuni lake likapewa A CERTIFICATE OF COMPLIANCE, sasa alipokuja kukosea na kuonekana baadhi ya mambo hayakufuatwa alipigwa rungu zito mno na hakuweza kufanya lolote kwasababu hakukuwa na mkataba mama BIT/IGA ya kumlinda. Au kama unakumbuka vizuri moja ya sababu ambazo Tanzania ilitumia kule London dhidi ya Acacia ni kwamba walifanya biashara bila A CERTIFICATE OF COMPLIANCE baada ya BARRICK kuondoka.

DP World na makuwadi wao wanayafahamu haya fika ndiyo maana wamefanya walichofanya....
 
Mambo yanaendeshwa ili mradi siku ipite tu.
Nchi ya ajabu sana hii
 
Mambo yanaendeshwa ili mradi siku ipite tu.
Nchi ya ajabu sana hii
 
Sawa Mkuu, ahsante sana kwa muda wako na ufafanuzi murua ulioutoa.
Kumbe huwa huishii tu kuandika hapa jamvini badala yake huwa unawatumia nakala kabisa!
Maana najua wana majukumu mengi sana.
Hivyo kupata muda wa kusoma makala zako (ambazo mara nyingi huwa ndefu sana) ni nadra sana.
Lakini kama huwa wanapata watu wa kuwafikishia basi ni jambo jema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…